Salamu kwenu Wanyabe!
Leo nimekuja na hili suala, nimekuwa nikiliona na kusikia siku nyingi japo sikuwahi kulipa umuhimu.
Basi kijana wangu mwenye kawaida ya kuimba kiustadi kila aingiapo maliwato ‘kuoga’ sio ile shughuli nyingine, leo ametia vokali kali sana kiasi cha kumkera mgeni wangu na akashindwa kujivunga.
Sijui yeye amepokeaje, kaonesha kutofurahishwa na ‘tabia’ hiyo... na kunishauri nimkanye mtoto asiimbe eti ‘chooni sio studio’.
Ndipo nikapata wasaa kulitafakari kwa upana wake, nikakumbuka kuwa sio watoto tu wanaopenda kuimba wakiwa kuoga, wapo baadhi ya watu wazima.
Hii ina maana gani.? Ni dalili ya nini, na haya ‘makatazo’ ya wazazi huenda vipaji vingi vimezimika kwa njia hiyo.?
Hebu tushirikishane tunaoshudia hii, na pia wale ambao ni mahodari wa kuimba, au wale ambao ‘walikoma’ watatupa sababu zao.
Karibuni.