Siri za utajiri ambazo hamna mtu anayeweza kukwambia

Sawa mkuu inaonekana unafahamu mengi, hatakama kutakuwa hakuna ukweli kwenye ulicho kiandika.

Ila mimi nina swali moja tu, lakini unipe jibu lisilo na kona kona.

Mungu uliye ingia naye agano(pact), unamfahamu kwa jina lipi?
Wee mwombe akupe mchongo wa kuwa tajiri kuliko yeye
 
Daah,ujumbe mzito sana huu. Ila nikuhakikishie kwamba funguo yakitasa tumepoteza..ila! Mkiona sura ngeni kabisa, mjue funguo imepatikan.
 
 
Umeandika upotofu mtupu maana hayo ndio secret societies Masson, illuminate na occultism hufundisha hayo, unless uje na scripture references ya hoja yako.

Mwili wa mwanadamu ni hekalu la Mungu, neno linasema basi itoeni miili yenu iwe dhabihu, iliyo hai, takatifu ya kumpendeza Mungu ndio ibada yenu yenye maana (Rumi 12:1~2).
Mwanadamu ni roho, yenye nafsi inayoishi katika mwili. Hivyo basi roho ya mwanadamu mcha Mungu huwa ni sadaka (Dhabihu) kwa Mungu refer. Zaburi 51:17
Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
Baada ya Yesu kufa pale msalabani, pazia la hekalu kupasuka inampa mtu access ya kumwomba Mungu direct kutoka rohoni mwa mwanadamu kwa kupitia katiba ambalo ni neno la Mungu au upanga ukatao kuwili pamoja na AGANO la damu ya Yesu iliyomwagika pale msalabani. Kumbuka, hakuna agano lolote linalofanyika bila kumwagika damu kama ilivyoandikwa :-
Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo. Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo Waebrania 9:16-28.
Na madhabahu iliyokamilika yoyote ya nuruni au gizani lazima iwe na vitu vifuatavyo :-
1.Mungu /mungu wa hiyo madhabahu. Hapo ni either Mungu Yehova au Lucifer a. k. a joka jekundu
2.Kuhani wa madhabahu. Huyu ni mtu kabisa ambaye anasimama kama kiungo kati ya watu duniani na ulimwengu wa roho uwe nuruni au gizani.
3.Kafara ya madhabahu. Hizi ni sadaka unazo peleka mbele za Mungu au miungu yako. Inaanza na wewe, roho yako na mali zako. Vitu vya thamani tupu.Hii ipo kote, nuruni na gizani.
4.Nguvu ya madhabahu. Kila madhabahu huwa inaachilia nguvu kwa watu wanaoitegemea ila madhabahu ya nuruni huwa inanguvu isiyo mithilika hata shetani anaamini hilo na kutetemeka.
5.Wafuasi /Washirika wa madhabahu. Hawa ni wale wanaojiunganisha na kutumika pamoja kwenye hiyo madhabahu i mean waumini iwe nuruni au gizani.
Siku hizi yapo makanisa utasikia wakisema, Mungu wa hii madhabahu, au jiunganishe na hii madhabahu ukisikia hivyo kimbia mbio maana hapo unajifanyia self initiation.
Therefore, agano la damu ya Yesu kama ondoleo ya dhambi kwa wanadamu latosha kabisa kama moyo wako umeufanya kuwa dhabihu kwa Mungu.
 
Ni upotofu kwako. Mimi ndivyo hivyo vikivyonisaidi. Kuhusu secret societies, sijui kitu wala mafundisho yao sijawahi kuyasikia.

Na kama hizo zinaitwa secret societies iweje mafundisho yake yakufikie wewe?

Mafundisho ndio yamebeba siri za taasisi yoyote
 
Ohh, safi sana. Ushirikina wangu ni upi? Mnakumbana na ugumu wa mambo sababu akili zenu na fahamu zimejaa fikra hasi
Dadili za mshirikina yeyote ni kufanya mambo kwa kuficha sana. Mambo ya imani yanayofichwa ni ushirikina. Na wewe hayo mambo yako ya kufanikiwa kifedha kama unashindwa kuyaweka wazi basi inaonekana ni ya kishirikina. La sivyo basi yaweke wazi hapa.
 
Dadili za mshirikina yeyote ni kufanya mambo kwa kuficha sana. Mambo ya imani yanayofichwa ni ushirikina. Na wewe hayo mambo yako ya kufanikiwa kifedha kama unashindwa kuyaweka wazi basi inaonekana ni ya kishirikina. La sivyo basi yaweke wazi hapa.
Kwanini Bublia imeandikwa kwa mafumbo? Je na yenyewe ni ushirikina?
 
Rakims hebu sema kitu, maana nasikia na wewe kilingeni kwako pale Ilala watu wanafurika uwatajirishe
 
Kwanini Bublia imeandikwa kwa mafumbo? Je na yenyewe ni ushirikina?
Biblia haijaandikwa kwa mafumbo imeandikwa kwa lugha nyepesi ya picha ili hata watoto wadogo waweze kuelewa. Biblia inatumia sana vielelezo vya picha (pictorial language) kuelezea ukweli flani na sio lugha ya kufumba. Kwanini wewe hutaki watu waelewe namna zako za kupata fedha kama njia zako sio za kishirikina?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…