Nachoamini, katika vita hii, Irani ilianza kupata hasara kubwa lakini Israel na Marekani walianza kupata hasara pia ndiyo maana wakaomba poo ili warudi kujipanga upya. Alichopaswa kukifanya Iran ni kuendeleza vita mpaka mwisho ingawa Marekani angeweza kuifanyia Iran tukio baya.Iblisi ni kiumbe miongoni mwa majini ambaye huwapambia binadamu matendo yaliyo maovu sana akitumia fursa aliyoiomba siku alipoumbwa binadamu.
Hata hivyo Iblisi mara mtu anapotenda lile ovu alilomchochea kulitenda huwa anamdharau sana binadamu na haraka mwenyewe hukimbia na kujitenda na uovu huo,Muda huo ndio ambao binadamu aliyetenda jambo hilo chafu naye hujuta na kuanza kutaka kuziba mianya ili asijulikane na binadamu wenzake japo Mungu ameshamrekodi tayari kwa hukumu siku ya kiyama.
Tabia za Iblisi ndio tabia halisi za raisi wa sasa wa Marekani,Donald Trump ijapokuwa yeye amemzidi kidogo Iblisi kwani yeye huwa hajutiii uovu wake.Yeye ndiye aliyeichochea India kupigana na Pakistan.Lakini alipoona India inapigwa mapigo ya aibu kwa ndege zake za ghali kuangushwa ndani ya mipaka yake.haraka Trump akamlazimisha Modi kusitisha vita akijifanya yeye ni msuluhishi.
Hivyo hivyo raisi Trump alimpa silaha zote alizotaka Netanyahu ili apigane na Iran akitaraji ndio itakuwa ndio ushidi wa mwisho dhidi ya Iran.Pale Israel iliposhindwa japo walivamia na kutumia silaha nzito ndipo mwenyewe Trump akaamua kuisaidia Israel na kukiuka taratibu za kufanya maamuzi makubwa kama hayo.Akatuma ndege zenye uwezo wa kubeba silaha kali zaidi ukiondoa nyuklia kupiga vinu vya nyuklia vya Iran.
Iran ilikasirishwa sana na kitendo hicho kama walivyokasirika hata marafiki wa Trump nje ya Marekani.Hapo Iran ikarusha makombora kupiga kambi ya Marekani iliyopo Qattar inayokusanya askari 10,000 wa Marekani moja ya kambi zilizotumika kuleta maafa kwa mataifa kadhaa ya kiislamu ya mashariki ya kati,Asia na Afriaka.
Japo Qattar ilitangaza kuyadungua makombora yote 18 ya Iran lakini habari kutoka ndani ya Qattar zinaeleza kuwa balistic kadhaa zilifanikiwa kupenya na kutua ndani ya kambi hizo na kuua askari wengi wa Marekani..Wananchi wa Qattar na wameshuhudia majenenza mengi ya maiti za askari hao yakisafirishwa kurudhishwa kwao Marekani.
Kuona hivyo na akijua kile kilichotokea Tel Aviv na Haifa haraka Trump kwa taibia zake za kiiblisi akasitisha vita akijifanya ni msuluhishi na kwamba alipokea maombi kutoka Israel na Iran kwa wakati mmoja kutaka kusitisha vita.
Iran na Israel zilikanusha madai hayo ya Trump na Israel iliona ni fursa ya kusitisha maafa kwake ikawa ya mwanzo kukubali mpango huo wa kiiblisi wa Trump.
Kama Iran angekuwa dhaifu maana yake ilikuwa ni fursa kuendelea kushambulia ili kuhakikisha Ayatolah anaanguka kabisa. Kama waliweza kumwangusha Saddam kwa nini isiwe Ayatolah mpaka wasitishe vita? Maana yake, walisitisha vita baada ya kuona na wao wanaenda kupata hasara na vita ikawa ngumu baada ya kaunta ataki za Iran!