Sisi kama nchi Tumetoka kwenye mfumo wa haki na demokrasia tumeingia kwenye mfumo wa udanganyifu uliovaa uso wa kidemokrasia

Sisi kama nchi Tumetoka kwenye mfumo wa haki na demokrasia tumeingia kwenye mfumo wa udanganyifu uliovaa uso wa kidemokrasia

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
1,012
Reaction score
2,317
Tumetoka kwenye ukweli na haki tumeingia kwenye mfumo wa udanganyifu ambao ni mfumo usiokuwa na maana yoyote hali inayopelekea nchi kuonekana kama ni ya kidemokrasia kwa nje lakini ndani yake sio kama inavyoonekana kuanzia kwenye vyama hadi kitaifa kwa ujumla.

Watanzania wengi kama mimi wapo wanaopinga mfumo huu lakini hawana wazo au uwezo wa kuzuia yasitokee tunaamini kwamba kwasababu mtu akifanya udanganyifu kupata uongozi labda kwa kutoa rushwa, kwa kuuwa, kwakutisha watu ili wampitishe au kwakuiba kura huyu sio mtu mzuri ni mbumbumbu hajielewe hafai na hawezi kuwa na msaada kwa watanzania maskini.

Kwa mfumo huu zaifu uliopo hivi sasa kwenye taifa endapo atapatikana kiongozi asiemuadilifu lazima watanzania wengi mtakufa zaidi zaidi lazima rasilimali zenu zitauzwa kwasababu ya rushwa na huyo mtu ataweza kuwatawala milele na milele maisha yake yote kwasababu ya madaraka yake aliyonayo wengi mtamuogopa.

Lakini mtaweza kuondokana na mfumo huu kama watatokea mashujaa lakini naona kabisa hii nchi inapo elekea sio kuzuri watu wachache wasio jitambua wanaharibu Tanzania.
 
Back
Top Bottom