Sisi mashabiki wa Yanga tunasema Kaze afukuzwe

Sisi mashabiki wa Yanga tunasema Kaze afukuzwe

Naona Simba mmeamua kuanzisha nyuzi mingi kumshambulia mme wenu. Je mtamuweza?
 
Hii kansa ipo hata Simba na timu nyingi za Bongo
Kaze hana kosa hata moja. Haiwezekani Uniletee Ndizi nikutengenezee juice ya Embe.

Tatizo la Yanga 90% ya wachezaj wamesajiliwa na GSM. Ni wachache sana waliosajiliwa kwa mapendekezo ya benchi la ufundi. Hatujui walitumia vigezo gani leo unakuja kumlalamikia Kaze aliekabidhiwa lundo la Wachezaji feki. Kaze anastahili kufukuzwa endapo tu yeye ndo alieleta wachezaji otherwise Mnamuonea tu kaze kwa uongozi wenu mbovu.
 
Kocha wetu amefeli sana katika idara zote mfano.

1.Ameshindwa kabisa kuunganisha timu kutengeneza kikosi cha ushindi. Angalia beki ya timu wanakatika Hadi wanagombana mfano Lamine na Mamnyeto

2.Uwezo wa kocha umefika kikomo baada ya hizi droo kinachofuata ni kupoteza point tatu kila mechi.

3.Usajili wa Fiston, Ni usajili mbovu Hana viwango kabisa Ni kumbwela mbwela uwanjani tu.

Mpira wa Yanga hauvutii,haijulikana Ni mfumo gani wanacheza Ni kubutua tu mpira uende mbele.

Mwanayanga mwenzangu unaweza kuongezea hoja hapa ili huyu kocha aweze kufukuzwa. Nafuu Mwambusi au yule aliyetuita manyani arudi kuinoa timu yetu wananchi.

Tunapaswa kuwa na Ile falsafa ya watani zetu Simbaya kumiliki kwingi, pasi fupifupi, si mnaona lile pira lao biriani lile. Heko mtani wetu Simba, Si kwa utopolo huu yanga wanaocheza.
Huna lolote wewe ni Mkia FC
 
Kama umeaikiliza maelezo ya Kaze baada ya Game ya Mtibwa Suger utamuelewa, Kaze naye anaendelea kuimarika baada ya kuijua ligi, mashabiki, viongozi na media.
 
Back
Top Bottom