Sisi ni kundi la tatu na tabia zetu kumi

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
29,126
Reaction score
29,352
Naweza kusema tumesahaulika ila taathira yetu ni kubwa mno japo inaenda taratibu mno.

Wewe tuweke unapo taka baina ya haya makundi mawili,ukituweka wa kwanza sawa,ukituweka wa pili sawa,na ukituweka wa tatu unakuwa umepatia zaidi. Tumeamua kwa hiari yetu kujiweka mahala tunapo stahiki sababu wengi katika watu tena kuanzia juu kabisa usukani kwa Amiri jeshi mkuu,huenda hawatujui au wametu puuza. Naam hili nina uhakika nalo. Sisi ndiyo kundi la tatu.

Asikwambie mtu bwana sisi ndiyo tuko makini zaidi kuliko makundi hayo mawili. Kati ya kundi linalo dai katiba na lile lenye kuipa muhula katiba iliyopo,sisi ndiyo wakubwa wao, laiti kama wange jua. Sisi tuna maarifa kuwazidi wawili hao,japo kuwa hatusikiki kwenye vinasa wala vipaza sauti wala katika vyombo anuai vya habari katika vile vikubwa na vidogo pia. Sisi ndiyo kundi la tatu na tunafurahia kuwa wa tatu.

Hizi ndiyo tabia zetu sisi kundi la tatu.

1. Sisi kila kitu tuna kiweka mahala pake na kila mtu tuna mpa stahiki yake,na sisi ndiyo mzani sahihi kwa haya makundi mawili. Tunahakikisha haki ina tendeka kwa kile mtu hata kwa yule dhalili.

2. Sisi hatudai katiba mpya wala hatuipingi ya zamani (kwa maana hatushughuliki nazo) sababu hali zote mbili kwetu ni sawa tu. Sababu zote zipo katika msingi mmoja wa Demokrasia. Msingi ambao tunaupiga vita vikali.

3. Sisi ndiyo wazalendo wa kweli na hakuna mwenye kuipenda nchi hii kutuzidi sisi. Hili hakuna anaye pinga,sababu sisi tunaamini ya kuwa kuipenda nchi yetu tunapata swawabu kwa Mola. Hatuna makando katika hili,jambo letu ni kwa maslahi ya umma wote.

4. Sisi hatujawahi kupiga kura wala hatuna mpango huo. Sababu kiasili kiongozi wa kweli hapatikani kupitia kura.

5. Sisi hatupendi ujinga,yeyote kati ya hao wawili akikosea tuna mchapa tu,kwa hoja zenye nguvu na ubainifu wa kielimu.

6. Kwetu amani ndiyo kila kitu. Asikwambie mtu miongoni mwa mambo mazito,ni kukutana na adui yako ana kwa ana. Hatupendi vurugu wala uvunjifu wa amani. Tunaipigania amani popote tulipo.

7. Sisi tunapinga migomo na kukemea maandamano,sababu kwenye migomo huathirika hata wasio stahiki. Rejea mgomo wa madaktari. Wanaharakati na Wajiitao Wanasiasa kwetu sisi hawa wote ni wachumia tumbo,watafuta umaarufu na ni sifuri visirani,waharibifu mfano wao hakuna. Hawa wa pili ndiyo waongo kupindukia,mpaka huku kwetu tumepata msemo juu yao,tunasema "Usimuamini mwanasiasa", sababu kwake anachopinga leo kesho kwake ni halali,ndivyo walivyo watu hawa.

8. Sisi tunaamini kiongozi yeyote ni chaguo la Mola,aidha kwa wema au kwa ubaya. Kuwepo kwake ni Mola ametaka. Humuweka aidha kwa ajili ya kututia adabu au kinyume chake. Ukiona kiongozi wenu mkuu ni muovu basi kaeni mkijua ya kuwa na nyinyi mnao ongozwa mna tabia kama zake. Hivi ndivyo tuna amini sisi kundi la tatu.

9. Sisi ni wengi huku kwetu,ila kulinganisha na haya makundi mawili sisi ni wachache,na uchache umesifiwa sana kuzidi wingi,kwani kilugha wingi ni jinsia ya kike yaani wingi wao haufui dafu kwetu. Mara ngapi wachache wamewazidi wengi ?

10. Sisi mambo yetu yote tume mkabidhi Mola muumba,na tunajitahidi kutimiza maagizo yake.

Sisi ndiyo kundi la tatu na tabia zetu kumi,kwa uchache msio tujua mtujue.
 
Nyie Kundi hilo la tatu ni [emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205][emoji205]
 
Inapendeza.
 
Makini sana
 
Back
Top Bottom