Sisi Simba SC na wachambuzi uchwara tumemponza Fei Toto

kilwakivinje

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
6,184
Reaction score
9,407
Mpaka sasa hatusikii wachambuzi na vyombo vya habari vilivyokuwa vikizungumzia swala la FEI TOTO wakiwa wanamzungumzia tens saizi wapo kimya na huenda walisha sahau na siku zote vitu vya kuambiwa changanya na akili yako, Leo hii wenzake wapo Tunisia yeye yupo Dar na endapo angetumia hekima na busara hii michuano ingemfaa zaidi na angeonekana sehemu mbalimbali na klabu inayomhitaji ingekuja kuvunja mkataba na kumsajiri lakini mpaka sasa kimya.

Hata wale mashabiki,wachambuzi na media zilizokuwa zinamsapoti saizi wapo kimya mpaka sasa anapotea machoni mwa watu mpaka arudi atatumia nguvu kubwa rejesha jina lake machoni mwa watu . Namshauri arudi amalizane na Yanga achane na maneno ya watu.

Imeandikwa na Chirstopher Mlanda

Ameandika @deustanzania
 
Simba inahusika vp hapo?
Kwamba umeshahau mlivyokuwa mnamdanganya eti Fei shikilia hapo hapo. Masimba Si mlijifanya wanasheria wake mkampa na vifungu vya mkataba vinavyoruhusu kurudisha milioni 112 na awe huru, mmeanza kujitoa sasa.

Huyu dogo aliambiwa Sana awe makini akaona raha kupost post insta sasa anajikuta anabaki peke yake waandishi wanachambua wimbo wa Diamond Zuwena sasa na masimba yako bize kutetea jezi zao
 
Humu kuna thread zao za kutosha makolo kila mtu anajifanya mwanasheria na Yanga wamewaandikia barua TFF kwamba hawamuoni Fei kambini baada ya hapo kitakacho fuatia Fei atadeal na TFF.

Hivi hajifunzi hata kwa Mane hapo ,Liverpool walishindwa kumwongezea mzigo ,jamaa kusubiri mpaka mkataba wake umeisha sasa hivi anakula mema Bayern na hakuwahi kugomea mazoezi wala mechi.
 
Tatizo kubwa asilimia kubwa ya sisi mashabiki wa simba ni mipang'ang'a
 
Wanasiasa kwa kushirikiana na viongozi wa TFF ndio wamemsaliti Fei Toto.

Shirikisho la Mpira linaongozwa kihuni na wahuni kuua vipaji vya wachezaji wetu na mpira wetu.
Walipohukumu kesi ya Morrison mliona TFF wapo sahihi kwavile wafaidikaji ni Simba, ila kwavile kesi ya Feitoto imewapa Yanga ushindi mnaona kuwa TFF imejaa wahuni.
 
Mimi Siwalaumu Simba kwakua wao kwao Feisal ni tishio hasa wakicheza Simba na Yanga, Kwa Bahati mbaya wamejikuta wakitengeneza kitu kibaya sana dhidi Yao.

Kunakitu ule mstari wa mbele wa Yanga unakujanacho kitakuja kuwaumiza Simba na vilabu vingine na wataona Bora ata Feisal angekuwepo.
Ni swala la muda tu.
 
Utopolo Roho mbaya Sana ...!

Dogo Kawatumikia Vizuri tu. Sasa anataka akapate changamoto Kwingineko Mnambania..

Ili Mumkomoe mkachezesha na TieFueFu dirisha dogo likafungwa..... Hawa Wachezaji wanawasoma tu .

Mngongolwa Karidhika sasa.... Maamuzi yangekuwa Kinyume Kila siku ungemuona kwenye Media.
 
Yanga wanamuhitaji Feisal kuliko Feisal anavyowahitaji Yanga. Kama amekosea na amewagomea vipi mbona mnaendelea kumlipa mshahara wake wa aftatu na hamjamuadhibu wakati siku zinakwenda na nyie mnahitaji huduma zake?

Dogo kakaza, wanasiasa na waganga wa Yanga wamenywea.
 
kweli mkuu ndo maana mechi 9 za ligi bila faisal tumepigwa zote

mechi zote tunapigiwa mpira nkubwa
 
Hakika wewe ni mbumbumbu uliye bobea, Yanga kama taasisi Ipo ndani ya Malengo yake mpaka Sasa.
Inacheza Makundi Africa na Inaongoza ligi na upo uwezekano mkubwa ikatetea makombe yake yote.
Feisal kama mchezaji amepoteza vitu vya Msingi katika maisha ya soka. Amepoteza nafasi(platform) ya kuonyesha kipaji chake katika mashindano ya Caf icho ni kitu kikubwa Kwa mchezaji anae jitambua.

Amepoteza furaha na muda wote anakua mpweke na mwenye mawazo mengi yanayo husu maisha yake ya soka.
Kama atakaa muda mrefu nje ya soka, upo uwezekano akirudi kucheza soka asiweze kifikia kiwango alicho fikia Sasa kwakua mazingira hayatakua kama yalivyo Sasa.
Uminifu wake na waajiri wake wapya utakua mashakani Kwa namna alivyo achana na Yanga kunaleta Tafsiri nyingi Kwa mwajiri mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…