Nashukuru kwa views zako lakini bado hata wewe ni kama mimi ni vile hujataka kujua kuwa hata ww haujui, kwanini? kwa sababu
1. Mansa mussa aliexist karne ya kumi 14 kwenye utawala wa Mali, nachotaka kujua miaka 300BC hapo mali palikuwaje? Hamna unachokijua kubali.
Mansa mussa anatajwa kuwa moja ya matajiri wakubwa kuwahi kuwepo duniani, umaarufu huu anaupata kwakuwa tu alienda kuvisit Msikiti wa Mecca hichi ndicho kinampa umaarufu. Je umewahi kujiuliza kuwa hakukuwa na matajiri na watawala wengine kama yeye? Kwanini kwenye historia hawapo?
2. Timbuktu University ni chuo kilicho kuwepo kuanzia karne ya 12 na kimepata umaarufu wake katika karne ya 15-16. Chuo hiki kilikuwa kinaunganisha misikiti mitatu katika Mji wa Timbuktu nchini mali, kilikuwa ni sehemu muhimu katika Enzi hizo. Chuo hiki kilikuwa kituo cha elimu ya utamaduni wa kiislamu na kilivutia wananzuoni wengi kutoka sehemu mbalimbali za dunia ya kiislamu.
Uislamu uliingia nchini Mali karibu na mwisho wa karne ya 9 na mwanzo wa karne ya 10. Ueneaji wa Uislamu katika eneo hilo ulikuwa ni matokeo ya biashara za trans-Sahara na mwingiliano wa kitamaduni kati ya watu wa Afrika Magharibi na wafanyabiashara Waislamu kutoka Afrika Kaskazini.
"nikurudishe nyuma karne ya 8 uislamu uliingiaje afrika kaskazini"
Uislamu uliingia Afrika Magharibi kuanzia karne ya 8. Wafanyabiashara Waislamu kutoka Bara Arab, India, na Asia walifika katika pwani ya Afrika Magharibi na kuanza kufundisha Uislamu kwa wenyeji. Kufikia karne ya 9, Uislamu ulikuwa umeenea zaidi katika eneo hilo, hasa kupitia biashara na uanzishwaji wa himaya kama vile Dola la Ghana. Uislamu ulileta pamoja na imani, muundo wa kisiasa na kisheria katika maeneo yaliyokuwa chini ya udhibiti wa Waislamu.
Swali linakuja pale kabla ya karne ya 5 au 400BC waafrika tulikuwa na maisha gani? Historia yetu iko wapi?
3. Ukisema Mwanafalsafa mkubwa duniani Mwanafunzi wa
Socrates, Plato kuwa amesoma
Alexandria University nakataa kwa sababu hicho chuo kimeanza miaka ya 1938 karne ya 20 na Plato alikuwepo miaka ya 300KK Huko.
PLATO alitembelea
misri kati ya 380kk Hii ilikuwa ni baada ya kufiwa na mwalimu wake Socrates. Plato alipenda kuzunguka sehemu mbali mbali duniani kujifunza falsafa na tamaduni za watu wengine ikiwemo Misri na
Inasemekana kwamba alijifunza kutoka kwa makuhani wa Misri na alivutiwa na hekima yao na maarifa ya kijiometri na kiastronomia.
4. Ukisema wayahudi walikuwa wanaasili ya Afrika nakataa kwa sababu Wayahudi wanahistoria yao na walikuwa na Dini yao ambayo iliitwa
Yahwism.
Yahwism ilikuwa ni dini ya waislaeli wa zamani hasa katika maeneo ya Seir, Edom, Paran, na Teman, na baadaye na Kanaani ambapo kwa sasa ni eneo la Islael na Palestine.
Yahwism ilikuwa dini ya Waisraeli wa zamani na ilikuwa hasa
polytheistic kwa asili, ikiwa na
pantheon ya miungu mbalimbali.
Yahweh alikuwa
mungu mkuu katika
pantheon hii na aliheshimiwa kama mungu wa kitaifa wa ufalme wa
Israeli na Yuda 1-3 BC.
Kwa mujibu wa wataalamu, Yahwism ilipitia mabadiliko kadhaa na kujikita zaidi katika monolatry ya Yahweh, ambapo Yahweh alitambuliwa kama mungu mkuu na mwingine yeyote alipunguzwa hadhi. Mabadiliko haya ya kidini yalianza kujitokeza kwa kiasi kikubwa wakati wa Ufalme wa Muungano wa Israeli na Yuda na yaliendelea kusambaa kwa watu wengi wakati wa machafuko ya kisiasa ya karne ya 7 na 6 BC.
Kufikia mwisho wa kufungwa kwa Babeli, Yahwism ilianza kugeuka kutoka kwenye polytheism na kuelekea monotheism, ambapo Yahweh alitangazwa kama mungu muumbaji na pekee anayestahili kuabudiwa.
Baada ya mwisho wa kufungwa kwa Babeli na kuanzishwa kwa Yehud Medinata katika karne ya 4 BC, Yahwism ilijikusanya na kuwa Uyahudi wa Hekalu la Pili, ambao kutoka hapo dini za kisasa za Kiyahudi na Usamaria, pamoja na dini za Abrahamu za Ukristo na Uislamu, zilijitokeza.
Utafiti wa DNA ya kale umebaini kwamba kulikuwa na mchanganyiko wa watu katika eneo la Levanti, ambapo watu wenye asili kutoka maeneo kama Anatolia na Iran walichangia kwa kiasi kikubwa katika muundo wa kijenetiki wa watu wa eneo hilo.
Kwa maana hii inaonesha Wahweh ( Mungu mmoja) alikuwa mungu wa Wayahudi, tangu kipindi cha Zama za kati na before christ.
Mungu wa waafrika yuko wapi?, aliitwaje?
JE UNATHUBUTUJE KUSEMA WAYAHUDI WALIKUWA WEUSI na wanahistoria yao? Nipe ushahidi unaoonesha Myahudi alikuwa Mweusi?
5. Kama yesu na wahusika wengine kwenye Bible walikuwa weusi je kwanini Dini ya kikristo ilianza kusambazwa na wazungu?
Kwanini waafrika wao wenyewe wasingepambana kusambaza ukristo wao?
Binadamu wa kwanza alitoka afrika ndio je Mzungu alitokea wapi? Vipi kuhusu wahindi wajapani, Korea China?
Kama adamu na Hawa walikuwa waafrika je spishi ya hizo race nyingine walitokea wapi?
Inawezekana Mwafrika kumzaa Mchina?
Mimi na elimu yangu ndogo hujanishawishi, njoo tena