Sisi wafuasi wa Hayati Magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Rais Samia

Sisi wafuasi wa Hayati Magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Rais Samia

Mabalozi kurudishwa nyumbani kama wasipofuata protocol za kibalozi ni sawa..ila ubalozi wa EU haukufungwa
Wewe ni mbumbumbu wa diplomasia, hakuna kitu utaelewa. Shule Haina Headmaster bado ni shule?
 
Nawashauri makada wote wa CCM msiokubaliana na siasa za Samia jiungeni sasa katika harakati za kudai katiba mpya. Hiyo ndio sahihi ya kuhakikisha nchi hii inasonga mbele na sote tunafurahia uhuru, haki na maendeleo.
 
Ulimchagua kwa ajili hiyo wakati wananchi hawana hela,,,tajiri/mwekezaji akiumia masikini haponi na hata serikali inakoswa kodi, Tangu migodi aifunge wananchi wangapi wamerudi manyumbani!!! Maelfu ya wananchi hawana makazi.

Mama samia tunakuombea afya njema na umri mrefu wewe na familia yako,,umekuja kulikomboa taifa. Hakika wewe ndiye rais wa wanyonge.
Sikumchagua mimi peke yangu, ni 84% ya wapiga kura, hadi wapinzani wengi walikubali mziki wa JPM na kujiunga CCM
Ni wananchi gani hao unaowasema walipitia maisha magumu? Hawa waliomchagua kwa 84% au hizo asilimia zilizobaki?
 
SSH ni mkweli embe analiita embe haliiti tunda la mwishoni mwa mwaka. Ni mkweli kwa maana hawapi watu anaowaongoza matumaini ya utajiri wa bandia.

Anaitazama sasa yenye uhalisia sio ile baadae ya matumaini ambayo kuifikia ni mpaka tutoke jasho jingi na tuumize sana vichwa vyetu.

Sisi ni tajiri wa rasilimali lakini hatuna bado ujanja wa kuzigeuka rasilimali hizo leo hii zikawa fedha, ni mpaka watu wetu wasomeshwe na wawe na mitazamo ya wanaotafuta kweli utajiri.

Ni kumvimbia mzungu ni kupoteza muda tu, lazima mmoja ajishushe kwa kutumia hekima ili watu wake wafaidike na kinachoweza kupatikana.
Wakati wa JPM tulikwama wapi pamoja na kunyimwa hiyo misaada ya masimango?
Si ndio kipindi tulifanya miradi mingi mikubwa ktk history ya Tanzania?
 
Mtu alishakufa mnajifanya wafuasi wake kwa hiyo mnaongozwa na mzimu? Nyerere mwenyewe alipokufa aliibuka Kikwete akajiita JK watu wakaaminishwa eti alikuwa mwanafunzi wa Nyerere na mfuasi wa Nyerere Ila alichokuja kufanya anajua mwenyewe.

Same as nyie mnaojifanya wafuasi wa mfu, Magufuli is dead so as his doings, beliefs and legacies.

It's high time for you to come back to your senses and get used to the new system coz things will never be the same again.
Tupo wengi sana mkuu mm bado naishi kwenye ulimwengu wa JPM na nitaishi hivo maisha yangu yote
 
Sijasikia kwa masikio yangu huyo Samia kasema nini lakini kama amezungumzia masuala ya PPP... yaani Public Private Partnership basi ni kiongozi wa ajabu tu ndie anaweza kukataa PPP katika dunia ya leo!!

The problem watu mlimwamini sana JPM na matokeo yake mkaaminishwa kila anachokisema yeye ni sahihi! Lakini kubwa zaidi, aliyokuwa anawaambia wananchi ni tofauti na ukweli uliokuwa unaendelea serikalini!!

Kwa mfano, chukua mabadiliko haya ya kisheria:-

View attachment 2125825

Ilikuwa ni serikali ya nani hiyo iliyopeleka muswada bungeni kuhusu PPP?!

Na hapo unaambiwa, an Act TO AMEND...

Baada ya hiyo amendment, mwaka 2020 ikatengenezwa regulation:-
View attachment 2125870

Kwenye hizo kanuni husika sio tu zimeelezea Solicited Proposals bali hadi UNSOLICITED PROPOSALS! And what's Unsolicited Proposal?

Regulation husika inafafanua kwamba:-

Kumbe basi, wala sio hadi mradi uwe initiated na serikali! Hata wewe ukiona fursa mahali, unaweza kuandika proposal na kuipeleka serikalini ili hatimae mtekeleze project husika under PPP.

Sasa how come tena unadai JPM alikataa PPP wakati huo huo serikali ilikua inaanda kanuni kuhusu PPP?

BONUS TRACK
View attachment 2125839
Asante kwa kutufafanulia,sisi tusio na elimu ya sheria huwa tunayumbishwa sana.Watu kama nyinyi muwe mwatufafanulia.
 
Mwendazake alituambia hii nchi ni Tajiri sana inaweza kuwa donor country.

Sasa imekuaje tena mama anagombea fedha za mabeberu?!
Hata yeye alikuwa anasema tunajenga kwa pesa zetu kumbe anakopa sana kimya kimya. Hivyo kuna mmoja anaweka wazi wakati mwingine alificha
 
Sisi wafuasi wa Magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Samia baada ya kutoka Ulaya, tunauliuza watu hawa walikuwa chama kimoja kweli? Achilia mbali kuwa kwenye ticket moja ya kupigiwa kura.

Tunauliza where is our pride? Maneno haya ni kinyume kabisa na kujiamini alipotupa Magufuli na Kabudi...na wana CCM wengi walivyo wanafiki wanampigia makofi kama walivyopiga kwa Magufuli, ndiyo maana kuna wakati najiuliza CCM ni chama cha siasa au ni genge tu la watu wanaolindwa na mabunduki kujipa madaraka na kula kodi zetu?

Ni chama gani cha siasa kisichokuwa na itikadi? Ukiwaambia hii haifai wataitikia na kushangilia, kesho mwingine anakuambia inafaa wanashangilia tena, hiki ni chama kweli? Tunapata wapi confidence ya kuwakejeli vyama vingine kama chama chetu kipo hivi?

Rais Samia amesema haya, nanukuu

Lakini pia tumeweza kukwamua miradi iliyokuwa imekwama, kama mnavyojua katikati hapa tulichokozana kidogo na umoja wa Ulaya uhusiano ukatetereka miradi ikakwama, Lakini tumeshakwamua fedha mradi mmoja umeshatiliwa na mwingine utatiwa hivi punde, kazi zitaendelea.

Kuna fedha nyingi zimetengwa kwa ajili ya Afrika kama Euro Bilioni 150 ambazo hizo sasa ni kinyanganyiro kwa Afrika. Atakayewahi mwanzo kupeleka miradi ya maana ndiye atakayepata fungu kubwa, kwa hiyo nasi tunajitayarisha tumeanza kupeleka...

Watoto wa Marehemu hata Kwa Mama Samia kwenda Belgium Kwa Lissu mmeumia sana
 
Well, siku ile tulivyompoteza Magufuli mi binafsi niliumia sana. Nilijua kama nchi tumepata hasara kubwa sana kumpoteza kiongozi wa aina ile. At the same time mi ni mtu wa imani: kufa kwa Musa hakukuwa mwisho wa safari ya kuelekea Kanaani, na kazi aliyoifanya Magufuli ya kujenga imani ya taifa haiwezi kufutwa na mtu mmoja tu pale Magogoni. The man can rest in peace, maana somo lake lilieleweka, hata kama si kwa wale waliokuwa wasaidizi wake wa karibu.
Nimekuelewa sana mkuu
 
Sisi wafuasi wa Magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Samia baada ya kutoka Ulaya, tunauliuza watu hawa walikuwa chama kimoja kweli? Achilia mbali kuwa kwenye ticket moja ya kupigiwa kura.

Tunauliza where is our pride? Maneno haya ni kinyume kabisa na kujiamini alipotupa Magufuli na Kabudi...na wana CCM wengi walivyo wanafiki wanampigia makofi kama walivyopiga kwa Magufuli, ndiyo maana kuna wakati najiuliza CCM ni chama cha siasa au ni genge tu la watu wanaolindwa na mabunduki kujipa madaraka na kula kodi zetu?

Ni chama gani cha siasa kisichokuwa na itikadi? Ukiwaambia hii haifai wataitikia na kushangilia, kesho mwingine anakuambia inafaa wanashangilia tena, hiki ni chama kweli? Tunapata wapi confidence ya kuwakejeli vyama vingine kama chama chetu kipo hivi?

Rais Samia amesema haya, nanukuu

Lakini pia tumeweza kukwamua miradi iliyokuwa imekwama, kama mnavyojua katikati hapa tulichokozana kidogo na umoja wa Ulaya uhusiano ukatetereka miradi ikakwama, Lakini tumeshakwamua fedha mradi mmoja umeshatiliwa na mwingine utatiwa hivi punde, kazi zitaendelea.

Kuna fedha nyingi zimetengwa kwa ajili ya Afrika kama Euro Bilioni 150 ambazo hizo sasa ni kinyanganyiro kwa Afrika. Atakayewahi mwanzo kupeleka miradi ya maana ndiye atakayepata fungu kubwa, kwa hiyo nasi tunajitayarisha tumeanza kupeleka...

Kwendraaaaaaaa SUKUMA GANG ninyi
 
CCM kama chama ni kuanzia kipindi cha Nyerere mpaka wakati wa Mkapa tu! Baada ya hapo, iligeuka kutoka chama na kuwa kikundi cha watu wachache wanaofaidi mema ya nchi, huku wananchi walio wengi wakiishi maisha ya kupigika..
Punguzeni upumbavu sasa samia anafanya vizuri wezi wakubwa na wanaotuongoza na kutengeneza sheria mbovu kuingia mikataba mibovu ni zao la nyerere msisahau hilo nyerere alikosea sana kutoa elimu kwa wachache iliaweze kuwazibiti kwa umri wangu Mimi nimefatilia ya kwenye vitabu nje yavitabu niyasikiayo na kauchunguzi kangu nimegundua hilo mfano hivi mwalimu akugundua kuwa katiba hii inampa rais mambo makubwa hivi kwanini aliikubali na alipotaka kuondoka aliiguna hatuoni hapo badotukaa kumsifu mtuambae ametuachia matatizo makubwa lakini kama kumsifu mtu au kiongozi yoyote ambae ameleta sintofaham ndio kunatuletea amani basi nashauri tuwe hivyo amani samani yake inazidi chochote tunachokitaka ila tusipende kuangalia tulipo anguka ilatuangalie tulopo jikwaaa
 
Mkuu unachekesha, yaani Magufuli kaacha miradi inaendelea vizuri, SGR ilikuwa izinduliwe tangia mwaka jana, Bwawa la Nyerere lilikuwa lianze kujazwa maji tangia mwaka jana,

kaingia Samia kavuruga serikali, kavuruga makatibu wakuu, kavuruga mawaziri kaweka watu wake miradi imekwama lawama anatupiwa Magufuli??
Wakati wa JPM ulisikia mgao wa umeme? Ulisikia mgao wa maji? Uliona vitu vikipabda bei namna hii?

Mbona watu mnakuwa vipofu hata kwenye mambo ya wazi kabisa?
Wakati Rais Samia akivuruga nchi wewe jukumu lako ni lipi huko ndani ya chama chenu chakavu?Suluhisho ni kuutetea aliyoyafanya huyo marehemu wenu?Je,kuna namna ya kurejesha nyakati nyuma?
Tunaposema ccm ni janga la Taifa mnalia lia kama vifaranga wasio na mama.
Tunataka kuandika Katiba mpya kwa ajili ya mustakabali mwema wa Mama Tanzania,upo upande wa wanaopinga hilo hitaji?
 
mimi sio mwana CCM, mimi ni mwananchi nisiye na chama ila nilifurahishwa na nuongozi wa JPM
 
Ndiyo shida ya mwafrica jamaa yangu!! omba omba hata ukimpa mipesa mingi bado atarudi mitaani kuomba omba.!! Misaada kama haina masharti ya kipumbafu kama kuwatambua mashoga etc ,acha iletwe maana walituibia dhahabu kwa miaka mingi sana.Hela zao zikija tuzipige tu hamna namna[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Eti hela zao tuzipige tu. Huujui uchumi wa dunia unavofanya kazi. Wale watu hawana shida na hela kwa sababu wanachapisha karatasi. Labda useme waishiwe karatasi.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom