Sisi Wanaume wa Dar leo hii tumesimama hapa Kuwapa ukweli Halisi. Dar Vs Mikoani Battle is around

Wanaume wa Dar si ndio nyie mnaokimbia vitoto vyenye mapanga au c nyie??, mnatuaibisha sana wanaume wa Tz.

Mwanaume gani anasikia eti panya road wapo mbagala, yeye yupo Sinza anaanza kufunga duka na kukimbia

Mnatuzidi kwenye kula mahindi ya kuchoma na pili pili limao.
 
Dar es salaam [emoji123] [emoji123] [emoji123] [emoji123] nguvu moja
 
Mda wa makonda ukiisha kunywa bia hapo ntapitia kulipa
 
Si kwa sababu nyie vijana wa mikiani skiuz hamlimi tena mmekimbilia pulutebo kazi kushinda barabarani na kuuza viyai mmewaachia babu zenu ndo walime matokeo yake tumejiongeza
 
Asubuhi : maziwa na mihogo/viazi vitamu vya kuchemsha. kama ni mkate basi ule brown.
Mchana: ugali mkubwa wa dona na samaki/nyama+mboga za majani+ mapera/maembe/matunda mengine yaliyopo, Kisha maji mengi ya kunywa.

Usiku: Ugali + mboga za mchana kama zilibaki. kama hazikubaki basi mtindi uliogandishwa kiasili haukosekani.

Hapo achilia mbali matunda na vingine vibichibichi vya kutafuna huko shambani.

Huku mikoani tunakula vitu 'Organic'. yani virutubisho vyote tunavifyonza.

Mikoani ni marufuku kula/kutumia
- mafuta yenye cholesterol...huku tunakomaa na ya alizeti,mawese etc.
-Ugali wa sembe. Hili ni kosa kubwa sana huku kwetu. ukionekana unakula sembe unaonekana umepotoka na kuacha desturi ya kwetu.
-Ngano nyeupe. Huku kwetu ngano hatukoboi... yani tunasaga kama ilivyo (Brown). hatutaki poteza kitu.
- Kula viazi mbatata vilivyokaangwa (huko Dar mnaita chipsi)
-Kuimaliza siku bila kumaliza lita zisizopungua mbili za maji kwa siku.
-Kula mayai ya kisasa. huku kwetu tunatumia yale tu ya kienyeji maana tunafuga kuku wa aina hiyo tu.

Mwanaume wa Dar asubuhi anaanza na chipsi kavu ......yule niliyemwona siku ile nilipokuja huko Dar nilimshangaa sana. Yani mimi naagiza supu na chapati 3 na kikombe cha maziwa, yeye anamwambia kijana yule muuza viazi 'niwekee chipsi kavu na mishikaki 2 na tomato nyingi sana' nikawaza moyoni 'laiti angelijua kuwa anajimaliza mwenyewe, asingeliagiza hivyo vitakataka asubuhi hii'

KWANZA KABISA: Kama kuna mwanaume wa Dar anataka kubishana kuhusu chakula ajibu hii kwanza ili tuone chakula cha huku mikoani na cha huko Dar kipi kinafaa kuliwa na mwanaume.

Baada ya kujibiwa.....NITARUDI KUENDELEA....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…