Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika Ametawala mpaka kafia madarakani hongera sana "Mnamaara"..Wewe pinga kwa hoja kwa nini asiwe wa milele mpaka tunamsindikiza kaburini ? Sio unaleta ngalambe.
Heshimu watu, Sponsor huvuta!Ugumu upo katika ufahamu wenu,hivi nyie mtaweza kusomeshwa na maprofesa ? mmebumaa vibaya mno ! Nawashangaa ikiwa mna macho lakini hamuoni,eti mna akili lakini hamfahamu,masikio dizaini za ungo lakini hamsikii .
Mnabwabwaja sana lakini bado sijaona wala hamjamuonyesha angalau mkasema huyu na huyu na yule wanaweza kuendeleza mkazo wa JPM,hamna CCM hawana kifaa wala speya inayoweza kukidhi vigezo vya Mheshimiwa Raisi Magufuli.
jamaa zangu wanaovaa makoti kama makobe huko ni utitiri wa mihemko utadhani wanatangaza mnada,hamna kitu wala sifa ndio kabisa hawana,Naachana nao.
Huku aliko JPM hakuna mwengine wa kuweza kuwafunga mapaka makengele,Leo hii mnaona nchi inavyochemka hakuna kuvumiliana tena,hufai unawekwa pembeni,na hadi leo tumepiga hatua ya kupigiwa mfano na sasa kila nchi wananchi wake wanasema wanatamani wawe na kiongozi jasiri kama Mheshimiwa Magufuli.
Mabezo yenu hayana mashiko,mara sijui kuandika,mara hufahamiki,mara huna hoja,ndio nikasema hamna elimu ya uelewa waulizenu wanaofundishwa na maprofesa.
Ila kwa huu ungumbaro mnaouonesha ni wazi mmekamatwa pabaya na ndio nikasema na kudai ni huyu huyu kwa miaka mingi ijayo,hatutaki mbadala.
Magufuli Ameanza kuijenga Tanzania ndio hivyohivyo ilianza kujengwa Roma.
Hivi bado Una mawazo kama hayo kwa sasa au umeuona ukweli?Yaani kila nikiiangalia CCM kusema kweli hawana anaeweza kumrithi Magufuli, hamna nikiwaangalia naona hawaiwezi kazi ambayo Mheshimiwa anaendana nayo, Sasa hata kule kwa wavaa makoti wala bata na pilau nako ndio yaleyale maji ya futi kwa nyayo.
WaTanzania walio wngi sasa wameanza kuona matunda sio ya CCM maana CCM wamepita wengi, matunda ya Magufuli ukianzia kwenye usalama, leo Tanzania unatembea muda wowote ule hakuna mwenye habari na yeye, leo kila mtu alie na simu basi hakosi net live, hayo ni maendeleo na yalikuwa hayapo, wengi sasa wanamiliki vitu ambavyo wakiviona ni ndoto kwenye maisha yao.
Sasa ikiwa mitano iliyopita tumefarijika kiasi hiki, je mitano mingine tuseme mpaka aridhike kuwa amewafikisha waTanzania sehemu ambayo hawatajuta milele.
Na wala sio vibaya kuna nchi nyingi maraisi wao ni wa milele, haitokuwa ajabu kwa Tanzania.