Ugumu upo katika ufahamu wenu,hivi nyie mtaweza kusomeshwa na maprofesa ? mmebumaa vibaya mno ! Nawashangaa ikiwa mna macho lakini hamuoni,eti mna akili lakini hamfahamu,masikio dizaini za ungo lakini hamsikii .
Mnabwabwaja sana lakini bado sijaona wala hamjamuonyesha angalau mkasema huyu na huyu na yule wanaweza kuendeleza mkazo wa JPM,hamna CCM hawana kifaa wala speya inayoweza kukidhi vigezo vya Mheshimiwa Raisi Magufuli.
jamaa zangu wanaovaa makoti kama makobe huko ni utitiri wa mihemko utadhani wanatangaza mnada,hamna kitu wala sifa ndio kabisa hawana,Naachana nao.
Huku aliko JPM hakuna mwengine wa kuweza kuwafunga mapaka makengele,Leo hii mnaona nchi inavyochemka hakuna kuvumiliana tena,hufai unawekwa pembeni,na hadi leo tumepiga hatua ya kupigiwa mfano na sasa kila nchi wananchi wake wanasema wanatamani wawe na kiongozi jasiri kama Mheshimiwa Magufuli.
Mabezo yenu hayana mashiko,mara sijui kuandika,mara hufahamiki,mara huna hoja,ndio nikasema hamna elimu ya uelewa waulizenu wanaofundishwa na maprofesa.
Ila kwa huu ungumbaro mnaouonesha ni wazi mmekamatwa pabaya na ndio nikasema na kudai ni huyu huyu kwa miaka mingi ijayo,hatutaki mbadala.
Magufuli Ameanza kuijenga Tanzania ndio hivyohivyo ilianza kujengwa Roma.