Sisikilizwi hapa kazini mimi ni msimamizi kijana.

Sisikilizwi hapa kazini mimi ni msimamizi kijana.

nipo online

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2022
Posts
1,039
Reaction score
2,657
Kiumri wamenizidi ila kielimu nimewazidi karibia wote. nipo katika kiwanda fulani hivi hapa Kanda ya kusini, nimepangiwa kusimamia wafanya usafi lakini kila nikiwakusanya na kuwapa maelekezo wananidharau.

Naomba ushauri je hali kama hii naikabili vip, nimeita adi vikao kadhaa lakini mahudhurio lengo niwape misimimamo yangu kama msimamizi mkuu.

katika jamii tabia ya kuchukuliana poa Sijapenda kabisa. wanasema kua walikuepo kama mimi kwa hiyo nisijifanye mjuaji. dah.
 
Ongea na mkuu wako awaongezee posho na mshahara utaona mabadiliko

Asilimia kubwa ya hapo wafanyakazi ni single maza ambao mashahara hautoshi so ili kuinua hali na mwemko wa Kazi waongezeeni pesa

Hiyo huitwa (Incentives ) marupu rupu
 
Na wale wa kiume? Je?
 
Kiumri wamenizidi ila kielimu nimewazidi karibia wote. nipo katika kiwanda fulani hivi hapa Kanda ya kusini, nimepangiwa kusimamia wafanya usafi lakini kila nikiwakusanya na kuwapa maelekezo wananidharau.

Naomba ushauri je hali kama hii naikabili vip, nimeita adi vikao kadhaa lakini mahudhurio lengo niwape misimimamo yangu kama msimamizi mkuu.

katika jamii tabia ya kuchukuliana poa Sijapenda kabisa. wanasema kua walikuepo kama mimi kwa hiyo nisijifanye mjuaji. dah.
Fanya mmoja wa mfano juu ya vile unavyosema au amua divide and rule tafuta wachache wafanye marafiki kwa vijizawadi halafu support unapata nguvu ya kuwanyoosha wengine huku unauhakika hata wakisiusa hawa wengine watafanya kazi zako
 
Kaza sauti na jiamini wakati unatoa maelekezo.
 
Ndio maana ofisi nyingi wanaajiri makampuni ya Usafi.
 
mbona kama huu uzi nilishawahi kuusoma humuhumu ama naona de javu inanitokea!!!!!!!!!!!!!
 
Dogo kwenye hizi ofisi ogopa sana wafanyakazi wa level ya chini yaani wapishi, walinzi na wafanyausafi tena ambao wana muda mrefu maofisini.

Wengi wao ni Machawa wa maboss pia huwa na uswahili, umbea, fitina na ushirikina.

Wewe simamia kazi yako kwa umakini na punguza kiherehere. Hayo mambo yakutaka kuheshimika na kutaka wazione cheche zako, utauponza.
 
Kuwa kiongozi wao, usiwe Boss wao.
Watakupatia ushirikiano.
 
Waheshimu kwanza,kama uluvyosema wewe ni boss lakini dogo Sasa inakuaje dogo unawaendesha wazee?waheshimu halafu wapangie kazi watafanya.
Weka heshima kwanza
 
Back
Top Bottom