Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
SISIMIZI!
- Si mkubwa kama temba lakini ana udhia
Ni mdogo mwenye mambo Kidudu kisosikia
Ficha hata kwenye tumbo Ujue ataingi
Sisimizi kanishinda Sijui nifiche wapi. - Atambalia vitamu Vikali avichukia
Vya nje na ndani hamu Vyote anavifatia
Huwa tena sina hamu Ni kheri kumuachia
Sisimizi ana ila Kutambalia vya watu. - Sisimizi hana kimo Angepigwa akalia
Angelifundishwa somo Milele angetulia
Bali hesabuni hamo Kupigwa ataonewa
Sina haja kushindana Kuteta na sisimizi. - Sisimizi hatosheki Kwa vyote vilosalia
Ameshawekewa keki Yenye pira maziwa
Bali yeye haridhiki Vyetu kuja tambalia
Sisimizi wacha inda Vya watu kutambalia. - Sijui nifiche wapi Ashidwe visogelea
Tena hutambua vipi kama tunamtambua
Huvizonga haogopi Na wenzake huwambia
Sisimizi kanishinda Sijui nifiche wapi. - Niseme niweke sumu Hasara nitajitia
Tajikosesha vitamu Sisimizi kuchelea
Na yeye akifahamu Chakula hatokijia
Nipeni tiba ya dawa Nimuweze sisimizi. - Wale wafukuzao dawa Vidudu nawaambia
Mende,kunguni na chawa Hao hawana udhia
Kuliko vidudu hawa Vyakula kutufujia
Sisimizi wacha inda Vyakula kutambulia.