Sisimizi!

Sisimizi!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
SISIMIZI!




  1. Si mkubwa kama temba lakini ana udhia
    Ni mdogo mwenye mambo Kidudu kisosikia
    Ficha hata kwenye tumbo Ujue ataingi
    Sisimizi kanishinda Sijui nifiche wapi.
  2. Atambalia vitamu Vikali avichukia
    Vya nje na ndani hamu Vyote anavifatia
    Huwa tena sina hamu Ni kheri kumuachia
    Sisimizi ana ila Kutambalia vya watu.
  3. Sisimizi hana kimo Angepigwa akalia
    Angelifundishwa somo Milele angetulia
    Bali hesabuni hamo Kupigwa ataonewa
    Sina haja kushindana Kuteta na sisimizi.
  4. Sisimizi hatosheki Kwa vyote vilosalia
    Ameshawekewa keki Yenye pira maziwa
    Bali yeye haridhiki Vyetu kuja tambalia
    Sisimizi wacha inda Vya watu kutambalia.
  5. Sijui nifiche wapi Ashidwe visogelea
    Tena hutambua vipi kama tunamtambua
    Huvizonga haogopi Na wenzake huwambia
    Sisimizi kanishinda Sijui nifiche wapi.
  6. Niseme niweke sumu Hasara nitajitia
    Tajikosesha vitamu Sisimizi kuchelea
    Na yeye akifahamu Chakula hatokijia
    Nipeni tiba ya dawa Nimuweze sisimizi.
  7. Wale wafukuzao dawa Vidudu nawaambia
    Mende,kunguni na chawa Hao hawana udhia
    Kuliko vidudu hawa Vyakula kutufujia
    Sisimizi wacha inda Vyakula kutambulia.
 
Hahahah...

Dakitari pole sana sisimizi kukuliza
mdogo mwembamba sana akutesa pasi kiza
dawaye h'jaonekana kuzurura yampendeza
mpende umchukie, jifunze kuishi naye!!!
 
SISIMIZI!




  1. Si mkubwa kama temba lakini ana udhia
    Ni mdogo mwenye mambo Kidudu kisosikia
    Ficha hata kwenye tumbo Ujue ataingi
    Sisimizi kanishinda Sijui nifiche wapi.
  2. Atambalia vitamu Vikali avichukia
    Vya nje na ndani hamu Vyote anavifatia
    Huwa tena sina hamu Ni kheri kumuachia
    Sisimizi ana ila Kutambalia vya watu.
  3. Sisimizi hana kimo Angepigwa akalia
    Angelifundishwa somo Milele angetulia
    Bali hesabuni hamo Kupigwa ataonewa
    Sina haja kushindana Kuteta na sisimizi.
  4. Sisimizi hatosheki Kwa vyote vilosalia
    Ameshawekewa keki Yenye pira maziwa
    Bali yeye haridhiki Vyetu kuja tambalia
    Sisimizi wacha inda Vya watu kutambalia.
  5. Sijui nifiche wapi Ashidwe visogelea
    Tena hutambua vipi kama tunamtambua
    Huvizonga haogopi Na wenzake huwambia
    Sisimizi kanishinda Sijui nifiche wapi.
  6. Niseme niweke sumu Hasara nitajitia
    Tajikosesha vitamu Sisimizi kuchelea
    Na yeye akifahamu Chakula hatokijia
    Nipeni tiba ya dawa Nimuweze sisimizi.
  7. Wale wafukuzao dawa Vidudu nawaambia
    Mende,kunguni na chawa Hao hawana udhia
    Kuliko vidudu hawa Vyakula kutufujia
    Sisimizi wacha inda Vyakula kutambulia.
Halo MziziMkavu, kumbe wewe mkali kwenye mistar! Naikopi hii nikafundishie somo la ushairi! kwa hisani ya MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom