Sista, "Kazi ni Kazi" tu sio shida. Mama ataka Polisi waje, kisa mwanae Jobless kununua Benz lake $50,000

dalalitz

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
3,423
Reaction score
1,987
Kwa wengine hii ingekuwa furaha, shangwe, nderemo na vifijo.
Kwa mama huyu wa KiNaigeria yeye anaona 'mapichapicha' tu.
.
Huku akibubujikwa na machozi mithili ya mtu aliefikwa na msiba na akihanikiza na kushinikiza Polisi wahusike kuchunguza imekuwaje mwanae ambae ndio kwanza kamaliza masomo ya Sekondari,
Leo hii eti mtoto anatimba nyumbani huku akiendesha Gari mpya bora ingekuwa ya kuazima,
dogo anajimwayamwaya huku akidai kuwa hiyo ni Mali yake yeye na ambayo ameinunua kwa Pesa zake mwenyewe. Gari husika si si Gari tu bora Gari, unaambiwa ni Ni MERCEDES BENZ.
Dingi yeye nae amestaajabu na kukosa cha kuongea.

Niitieni Polisi jamani,
Hapana hapana hapana haiwezekani"
Anaongea kwa hisia za kumaanishaanachokisema na huku akigaragara.

Kumbuka sio Sinema hii.

Unadhani mama yupo sahihi?
 

Attachments

  • -210710507.mp4
    14.4 MB
Uchawi wa Mwafrika ni wa kutiana adabu na kuoneshana umwamba
 
Ingekuwa Tanzania mama angetamba kwa majirani zake, hata hivyo nyumba ya wazazi wake na gari havifanani sijui atakuwa analilaza msikitini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…