Sisu ni moja Movie Bora 2023

The equalizer jamaa anajua sana.
 
Kabla sijaangalia extraction 2020, nilikuwa nikisikia ikisifiwa sana.
Binafsi huwa sipendi just kuona watu wanapigana tu halafu huelewi wanapigania nini au story yake haieleweki.
Niliipuuzia ile filam kutokana na trailer pia cover photo yake jamaa anaonekana kimapambano nikajua ni mambo yaleyale tu. Ila 2022 baada ya kelele kuwa nyingi nikaona ngoja niitafute.
For me it was among the best i have ever seen na sichoki kuitazama. Ngoja niitafute na hii naona inapigiwa kelele sana.
 
Hata hizo ulizozipa 9/10 karibu zote zimejaa uongo. Equalizer ni uongo mtupu kwenye scenes za mapigano.
 
SISU ni movie iliyotakiwa itolewe na director wa Bollywood. Movie zilizotoka siku za karibuni ni nzuri ila hazijafika viwango vizuri kwa upande wangu. Covenant, Kandahar, Sisu & Extraction 2 ziko njema ila wapambane zaidi.
 
Kiukweli mbaya bora jamaa alivyokufa.
 
Hii kama mtu anakupa kwenye flash ni sawa, ila kama ni unataka kununua kwenye movie library aiseee achana nayo kabisa.
 
Hata hizo ulizozipa 9/10 karibu zote zimejaa uongo. Equalizer ni uongo mtupu kwenye scenes za mapigano.
Kuna movie unayoijua ambayo watu wanakufa kweli wakipigwa risasi au kulipukiwa na mabomu, au kuna movie unayoijua ambayo mtu m'moja kiuhalisia anaweza wachakaza watu 30 pekee yake?

Swala hapa tunaongelea namna uongo unavyogeuzwa kuwa ukweli. Kunatofauti ya kuigiza mtu anapigana na watu 5 kwa wakati m'moja akiwa pekee yake na kuna ili ufundi unatumika kuonyesha hilo tukio yaani technicalities zinazojumuisha mapigo, upigaji wake, speed ya attack, timing, namna edits zinafanywa, etc.

Tunaongelea ni namna gani producer na director wamefanya uongo kuwa mtamu ili story isikose uhalisia.

Hizo movie nilizolist hapo si mimi tu ambaye nimezikubali hizo ni movie ambazo zimeuza na zimefanya vizuri sana Hollywood na kuwafanya actors wake wapande chati na kuwa na shavu kubwa sana la kulipwa sababu ya kucheza vizuri movie hizi.

Kuna namna movie inatengenezwa hadi inakushawishi na kutrick akili yako kuwa ni kweli.

Tarehe 2 mwezi December mnamo mwaka 1983, Michael Jackson, alipoachia video kali ya "Thriller" ambayo ni Music Video yenye maudhui ya movie, yenye urefu wa dakika zaidi ya 14,iliyofanyiwa udirector na John Landis, iliwafanya watu watembee usiku huku wameshika mawe, wengine walishindwa kulala vizuri kwa wiki kadhaa baada ya kuitazama ile video, wadhani ni kwasababu "werewolves " walikuwapo kweli? Ila huyu director pamoja na Michael Jackson wakahakikisha watu hawatalala kwa kile watakachowaonyesha katika ile video.

Na ikawa hivyo.

Uongo ambao unafanana na ukweli.
 
Mzee SISU ameanguka na ndege toka juu mpak chini alafu ametoka hana hata michubuko
 
Hebu jiulize kile kibati kimetengenezwa kwa madini gani hayo hadi hakipitishi marisasi zaidi ya elfu tano jamaa alichapwa nayo. Inamaana jamaa walikuwa wanalenga lile bati tu miguu hawaoni? [emoji23][emoji23][emoji23]
Nafkiri aliyefeli ktk hiyo movie ni mtu cinema ila story iko sawa kabisaa...
 
Binafsi John wick4 ndo haifai hata kidogo[emoji706]
Kuna wakati ktk movie waandishi wa story wanaishiwa...hivyo wanauzia jina la franchise na siyo content...hii imeikumba Fast and furious, expandables, prison break, escape plan, terminators, Avator na Sasa tumeona John Wick. Afadhari avators wao wametoa movie wakiitafutia njia nyingine yaani kisa kilifika mwisho hivyo inabidi watafute visa vingine na movie ikavutia ktk mambo ya nature na viumbe bahati Sasa wick ni marisasi mengi yasioendana na kisa yaani ile scene ya ktk ngazi ni ndeefu na haina reality yoyyte...kumuweka mtu kipofu Yen halafu hana uhalisia wa kipofu yaani wametupoga kama DP world tuuu
 
🤣🤣🤣 umesahau kaanguka na ndege kwenye matope, af mwanaume ametoka hana ata mkwaruzo.
 
Boss mbona Keanu ame-play part vizur tu, Hata hii chapter 4 imekaa vizur na most ov the scenes zimepangika vizur na zina uhalisia ... Au nitajie scene ambayo wew unaona director amekata viuno
 
Extraction II Ni safi sana ila Fast X [emoji41] aaah pale wamekata viuno yaani unaangalia mpaka unasema eeh hapa wameniongopea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…