Sitakaa nilisahau tangazo la CocaCola la mwaka 1995

Sitakaa nilisahau tangazo la CocaCola la mwaka 1995

Hakuna Kama revola.
Ebu tueleze Siri ya mafanikio yako.
Sio Siri ni revola.
Revola peke yake.
Ndio kwani marashi yake ni tulivu na uniweka fresh mchana kutwaaa
 
Ndo nimekuja kumjua miaka hii kwamba ni yeye nilikuwa simjui ila Hilo tangazo maneno yake yote yapo kichwani.na uwa siyasahau
She was our favourite in that add...halafu huyu dada alikuwa mzuri...ukitaka kumjua kumfananisha vizuri meangalie Flaviana alivyo ndivyo alivyokuwa Miriam
 
Umenipa holiday vibes na kumbukumbu nzuri sana
Heri ya msimu wa siku kuu 🥳
🥳
 
Cocacola walitoa tangazo lao mwezi wa December 1995, likiitwa CocaCola Caravan, nilikuwa nimemaliza darasa la saba. Aisee nilivyoliona nilichanganyikiwa, lina uubunifu wa kuanzisha hisia zako hata kama huipendi Christmass.

Tokea mwaka huo CocaCola walilirusha tena mwaka 1998 na nafkiri 1999 ila version wakiupdate wakaacha kulirusha ila mwaka 2007 walilazimika kulirusha baada ya demand kubwa ya watu.

Huwezi kuhisi Christmass imekamilika kama hujaangalia hili tangazo. Cha kufurahisha na watoto wangu wanalipenda sana baada ya kuliangalia hasa ikifika december, maana niliwahadithia.

Naomba Mungu anijalie maisha marefu nije nione na wajukuu zangu wakiliangali, ni tangazo la tofauti kwa kweli.

Nakwenda Moshi tarehe 20 kwa ajili ya sikukuu, Mungu akinijalia, Mungu ambariki sana Mzee Mengi kwa kutuletea Tv ya bure miaka ile ukafanikiwa kuliona lile tangazo huku tukinywa CocaCola bora kuliko zote kwa miaka 20 sasa Afrika nzima kutoka kiwanda chake cha Bonite Bottlers Ltd.

Wadau wa It mnisaidie kuliweka tangazo hapa kwa faida ya wengine, ila lipo YouTube, andika tu "Holiday is coming" au "CocaCola Caravan" la mwaka 1995, ndiyo bora.

Santeni.
MP
Update nimeweka hapo liangalieni...ila nadhani hili ni la 1999 la 1995 was the best halisemi santa is coming linasema holiday is coming

Nashukurubsana nimelikumbuka
 
Mleta mada umeshare nasi a very emotional memory. Kimsingi hili tangazo linagusa watu wengi maana lilitukuta kipindi kizuri sana cha mwaka.

Mimi hili tangazo nakumbuka miaka hiyo nikiwa bwana mdogo, ilikuwa ni alhamisi kama sio ijumaa but ilikuwa weekend fulani.

Mzee alileta mbuzi wa kutengenezwa sikukuu hiyo. Mbuzi aka kata kamba akatoka nduki. Tulimkimbiza kutafuta tokea saa 4 jioni hadi saa kumi na mbili hatukumpata. Tukawa tunarudi home tukakuta na dingi ndio anarudi toka town kabeba mti wa Christmas (ile mibichi) na mapambo ya sikukuu maana ilikuwa lazima mti uletwe siku moja au mbili kabla ya sikukuu yaani tarehe 23 au tarehe 24 kabla ya tarehe 25 December.

Tukaushusha tukauweka ndani nakuanza kuuandaa na kufunga mataa na mapambo yake. Akarudi tena mjini kutafuta mbuzi mwingine akatuacha tunapamba. Tukapamba sana hadi mida ya saa mbili mbili usiku hamu ya kula haipo hapo tunasubiria tutolewe nguo mpya na viatu tukazijaribu.

Mida ya saa tatu nikatoka na masista na majirani tukaenda zetu church mkesha maana misa ya Asubuhi kwenda mtihani hapo natarget niwahi kurudi nitazame movies zilikuwa zinawekwa usiku ITV.

Tumerudi mkesha kama saa sita usiku nimekaa zangu sebuleni nakula movie yale mataa taa ya Christmas, mti unawaka na mataaa sebule inawaka kwa mapambo hilo tangazo linaonyeshwa ITV mida hizo. Sasa ile feeling yake hadi leo haijanitoka inakufanya uhisi kama upo peponi.
Je mlikuja kupata mbuzi ama vip
 
Umenikumbusha mbali sana
Swala la kwenda kanisani usku nilikuwa nalipenda snaa nalio kilio kikuuu saanaa nikiachwa na masister kwenda church usku nilikuwa napata mzukaa mkali mno kipindi cha chrismass lzm nitupie kiyltu kipyaa cha viatu na pamba kali

Siyo sas hv hkn mzuka wa chrismass eti watu wanjiondokeea kazini siku ya chrismass
 
Yeah speaking of the best Cocacola Adverts kuna hilo

Kuna lile la I love you Africa wimbo wa Steve Kekana

Na kuna lile la Hey Brother wimbo wa Avicii, la wale Brothers ambao mkubwa alikuwa anapenda sana kumchokoza mdogo wake ila mwishoni alimuokoa na wale bullies, kwangu those are the best
 
Back
Top Bottom