Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Ningependa kuona wakosaji wote wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria bila kujali itikadi zao siasa.Fine!
Hata kama hayupo, bado sitaki mtu yeyote anaye imply kwamba wewe ukiwa upande wake basi utapata ‘favors’ au ‘courtesies’ flani flani ambazo wengine hawana kutokana na kutokuwa upande mmoja na wewe ki itikadi na kimtazamo.
Au wewe unasemaje?
Kama serikali inaundwa na CCM wewe hupendi kuona watu wakosaji wakishughulikiwa bila kuangalia ni wa chama gani?
Ninaona kwanini hawa '' wa Chadema'' unaosema, wamefikia hatua hiyo.
CCM na serikali yake imejenga ''bad precedent and double standards'' kiasi kwamba hakuna mwenye imani.
Mfano, ukiwa mwizi huna pesa utahukumiwa miaka, ukiwa mwizi wa pesa ndefu utahukumiwa kulipa faini!!!
Ukiwa hohehahe ukakamatwa na kucha za simba, utakula miaka. Ukiwa Mbunge na pembe za ndovu-lipa faini.
Ukienda kwa kundi kurudisha fomu za uchaguzi umevunja sheria. Mkurugenzi aliyekimbia ofisi ana udhuru!
Unapokuwa na mambo kama haya nani atakuamini hata kama unatenda kwa dhamira njema?
Kwahiyo tusiwalaumu hao vijana , tuangalie pia mistrust iliyopo katika justice system na ukweli kuwa lady hayupo