Sitaki kuandika sana lakini ninyi wadau mtasema

Kwani wewe huijui sheria nyingi ni kwa ajili ya kuendelea kuwafanya maskini kuwa maskini zaidi?

Nilicho Fanya Mimi kuwasaidia NI kuwapa kazi na wakimaliza nawalipa pesa wananunulie madaftari na kalamu za shule huo ndio msaada wangu mkubwa ,

hizo drama za sheria zenu mnazo iga iga kwa mataifa yalivyo endelea wewe endelea nazo, Mimi Nina uishi uhalisia kabisa wA maisha ya watoto WA kiafrica
 
Majitu mengine yamekaa kwenye viti vya kuzunguka hayajawahi hata kuona maisha halisi ya watanzania huko vijijini, yamepigiwa pande yamepata kazi na mibaba Yao mifisadi sasa yanazurura Tu na vitambi kwenye V8 za Serikali halafu yanajifanya yanawatetea watanzani unafiki mtupu, wakati yanakula na kuiba hata pesa za miradi kwa ajili ya hao hao watoto wanao jifanya Leo eti kuna sheria inawalinda.
 
Songea manicipal na watoto baadhi nawajuwa.
Kumbe Ruvuma! Tena bora Songea,nenda Mbinga hata hiyo pesa haipo na wanatolewa madarasani na kwenda kupiga kazi.
Kiujumla mkoa ule ni wa kipekee kabisa hapa nchini. Mttoto wa umri wa miaka 13 kuwa na mtoto ni kawaida na ni haki yake.

Walimu kuchukua wanafunzi hasa wanaokaa wanachoita kambi shuleni na kusafirishwa 10+ km kwenda shambani na hata kukaa huko siku kadhaa ni jambo la kawaida sana wala hakuna anaye uliza.
 
Hata mimi nilivua samaki sana ili nipate fedha ya kununulia sare za shule mkuu kipindi hicho nikiwa darasa la 5 tu. Kosa ni kumtoa mtoto masomoni ili akakufanyie kazi ijapo siyo kisheria.
 
Kila la kheri mkuu omba usikutane na kono la bwana msumeno. Litakata huku na kule na hutakua na mtu wa kumlilia. Narudia kama umefanya ivyo na ikapita shukuru Mungu nakusihi usirudie naamini unayo familia bado inakutegemea
 
Watoto wa shule wenye umri wa miaka13-17wanapakiwa kwenye gari na kupelekwa shamba kwa nakubaliana ya malipo ya7000 kutwa baada ya kazi ya kupanda.Je hii ni dawa?
Wewe hamnazo!
Alfu7 mtoto akifanya siku 6 ana Alfu42.... Hivi wewe unajua watoto wawakulima wanavyoishi? Ujue shule zipo karibu kufungua!
 
Hili swala watu mmechukulia very personal na wakati mimi nimezungumza sheria. Haimaanishi mimi sijui mimi nimesema nini sheria inasema. Sasa mnavyonijia juu utafikiri mimi ndio mshika msumeno.
Wewe kima Acha ujuaji kujifanya unataka sheria zifuatwe, sheria pia inakataza kutumia utambulisho bandia kwa mujibu WA sheria ya makosa ya mtandaoni , sasa nikuulize wewe kwenye cheti chako cha kuzaliwa unaitwa ''southern Highland "? Ili tujue kweli mwenzetu unafuata sheria
 
Kila la kheri mkuu omba usikutane na kono la bwana msumeno. Litakata huku na kule na hutakua na mtu wa kumlilia. Narudia kama umefanya ivyo na ikapita shukuru Mungu nakusihi usirudie naamini unayo familia bado inakutegemea
Tusitishane wewe sio wakwanza kuijua hiyo sheria, na watoto wanapiga kazi kama kawaida ILI waendeshe maisha Yao , kipi Bora kwako umpe kazi apate Kula au umyime kazi afe njaa
 
Mkuu mimi kutumia huu utambulisho sijafanya makosa yoyote. Halafu pia nadhani tunaposhindwa kuelewana ni padogo sana naona una hemkwa tu. Mkuu nilikua nakutahadharisha sikua na maana mimi ni mkamilifu sifanyi makosa kama unavyo ninukuu hapo. Tofauti yangu na yako wewe unaenda kinyume na sheria na kujitangaza ndio mimi nimetoa tahadhari.

Sisi wote ni aidha wafungwa, marehemu au walemavu watarajiwa. Kwa hiyo mkuu usikasirike ovyo ovyo
 
Siyo malumbano bali hoja
 
Nyie ndio mnaodekeza watoto yakikuwa yanakuwa mashoga toto hata kazi haliwezi. Kwani shida ipo wapi?
Hivi Ushoga unatokana na kutojua kazi? Huwa mnawaza nn ktk akili zenu?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ruvuma iko mwishoni sana kwa TZ.
Tunaishi kivyetu vyetu. Bombii nyumbiiii
 
umekazania sheria sheria kama ndio unazijua sana ama huyu anakupa tafakuri utafakari hio sheria ipo sawa anachofanyishwa kazi ni ukatili ?....ilitungwa ili mtoto asiweze kufanyishwa kazi zilizo nnje ya uwezo wake au kazi hatarishi...binafsi nawaajiri kila mara hasa mwezi wa 12 wanakuja wenyewe kuomba kazi za kupalilia na huwa wanapenda kuja kwangu sababu ya matunda....nawalipa vyema na kuna wakati wazazi wao huambatana nao kuja kupiga vibarua...kama huwadhulumu huwahatarishii maisha yao kazi hizi ni stadi nzuri za maisha....tumechuma sana kahawa za watu weekiend na lakizo nyakati hizo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…