2008 hiyo Mshua alikuwa anapiga kazi zake za wiki lakini ikifika Ijumaa mida ya saa mbili flani hivi anapiga vyombo vyake kistaarabu kabisa hana kelele wala fujo na ni ndani sio bar.
Nilipewa takribani elf 10 kuchukua lvinywaji alivyoniagiza, enzi hizo ni pesa kubwa hii.
Nilipita sehemu wanachezesha mchezo kuna visahani vitatu, kwenye kimoja kuna picha, jamaa anavizungusha vile visahani, ukichagua chenye picha unashinda pesa ila ukikosea unapunwa.
Aisee kama hujawahi liwa na hawa jamaa usiniambie kitu kuhusu kamari. Ni wakora vibaya mno na hawafai!! Nilipigwa elf 15 paaap!! Yaani ndani ya sekunde kadhaa, nilikuwa na kinokia changu nacho nikaambiwa niweke ili nikomboe pesa, Mjombaa!! nayo wakaisomba, nilihisi kuchanganyikiwa, tumbo lilikuwa linazunguka kwa spidi kali mno.
Kurudi home mida ushayoyoma nje kabisa ya ratiba za mzee, nikajitetea nmeibiwa njiani, mzee hakunielewa kabisaaa hasa ukizingatia kanisubiri sana na alikuwa na kiu ya wiki nzima ya vinywaji vyake, nilisikia tu "mama bright niletee mtwangio" nilitaka nikimbilie chumbani kwenda kujifungia, nilipiga tambo 2 tu nikala ngwala, mshua aliuliza kwa sauti "mliopo jikoni kuna mtwangio huko?", Bahati nzuri waligoma haupo, alinikokota kwenda nje kwenye miti ya matunda, alinikwida kwa mkono moja huku mwengine anakiandaa kiboko cha mpera, stiki zilianza pale kiukweli nilichapika si kitoto.
Kipindi hicho yaani nikipita sehemu walipo hao wakuda nafumba macho dakika 2 naomboleza ile elf 15, simu na kichapo.