Sitaki kutukanwa, nataka nishauriwe

Sitaki kutukanwa, nataka nishauriwe

Je mkeo akikuomba kupata mme wa pili utakubali? maana mapenzi yanauma sana hasa unapofahamu kwamba muda huu yupo kwa naniii.
Iwapo sheria inamruhusu basi niamfanyia na sherehe!
 
kwani akioa kuna shida gani jamani?
Mbona mwajijaza taabu za bure?

Aoe tu mtu mwenye quality za kuosha, sio alete Asha Ngedere nyumbani.
Nashangaa! Eti wanadai haki kwa kunivunjia haki yangu iliyopo!
 
Ushauri wangu wa bure, ndoa ya pili au ya tatu ni ndoa ya utapeli au uwizi, keep in mind love is not enough to convince someone lazima kutakuwa kuna maslahi fulani yanatarajiwa from both side.

Hakuna mwanamke anayekubali kushare mume if there is nothing in return apart from love thats the fact.

Nakubaliana nawe mia kwa mia kuwa ndowa yoyote inaangalia maslaha kwani kusingekuwa na kuchagua. Kuchagua ni kuangalia maslaha na iwe ya mwanzo au ya nne maslaha lazima yawepo!
 
Mkuu sawa lakini kumbuka ni ruhusa na si wajibu....na itakuwa vema ukaoa mjane nadhani hii ruhusa ilitolewa kutakuwa na resson behind na sio kimatamanio zaidi tafuta mjane mstiri ana mkeo atafurahi.... wenye dini watanisahihisha hapa...!

good luck
 
Nataka kuongeza Mke wa Pili!
Awali ya yote Mabrouk! Ila nakusia nafsi yako na yangu pia katika kuwa muadilifu kaka! Allah akutangulie katika hilo, akupe mke mwenye imaan, awaja'alie wote afya njema, rizk ya halal na watoto wema InshaALLAH!
 
Hiyo hela kwa nini usiwasaidie watoto yatima.Manake ndo nyie mkifa mnaacha watoto wengi mtaani wakipata shida.
 
Nauheshimu msimamo wako lakini nini tusi katika ulimwengu wetu wa sasa? Samahani, lakini kama kivazi chenyewe ni kuvionyesha hivyo vinavyoitwa matusi unafikiri dunia yetu ni ya kujali nani kasema nini? Angalia maslaha dada angu after all hakuna uhakika wa mtu chake peke yake dunia yetu ya leo. Tukiowana angalau tutakuwa tumehalalisha huo usasa wa leo.

Nadhani hujanipata vizuri, mapenzi kwangu ni nafsi wala si maslahi!! So siwezi kuteketeza wala kunung'unisha nafsi yangu kisa maslahi hasa kwa kugawana penzi la mume!! Vile vile mapenzi/ndoa sio kazi hata niletewe assistant, kumbuka mimi kuolewa haimaanishi kwamba ni koloni la mtu na wala similikiwi to the extent niendelee kuchekelea tu bwana akiteka na kuendelea kuongeza makoloni mengine na mie nibaki kurundikwa tu...........so kunijia na kuniambia habari za kuongeza mke ni sawa na kunitusi!!! Hivi ni nini hasa kinachokufanya uongeze mke wa pili, tatu......kama sio tamaa zako tu na kiburi cha uzima??
 
Kwa huo umri wa zaidi ya miaka 40 unatakiwa ufanye vizuri tathimini ya kipato chako kama kinaweza kuwahudumia wake wawili na kusomesha watoto watakaozaliwa na mke mdogo kwa zaidi ya miaka 20 ijayo ambapo wewe utakuwa una umri zaidi ya miaka 60 na uwezo wako wa kufanya kazi utakuwa umepungua wakati wanao bado wanakutegemea. Kama uwezo wako kifedha ni mzuri na unaona bado unaweza kumudu majukumu ya ndoa kwa wake wawili na mkeo mkubwa ameridhia unaweza kuoa.
 
Usiwe na wasiwasi nakuahidi mambo yatakuwa mazuri. Hutokosa kitu hebu nipe wasiwasi wako , nikutowe!

Tafadhali baba, mimi sio waya hata unitafutie pacha wangu na kutuconnect kwenye receiver moja kwa manufaa yako binafsi!!! Na kama wasiwasi unatolewa kwa namna hiyo, basi ni heri nijikung'unte mwenyewe udondoke!
 
Awali ya yote Mabrouk! Ila nakusia nafsi yako na yangu pia katika kuwa muadilifu kaka! Allah akutangulie katika hilo, akupe mke mwenye imaan, awaja'alie wote afya njema, rizk ya halal na watoto wema InshaALLAH!

hee! Kumbe una imani hivyo! Nimependa.
 
sababu za kutaka mke wa pili ni kwa sababu za tamaa za mwili au mengineyo,,kama mmoja hajaweza kukutosheleza wa pili unadhani anaweza?
 
Sijasema kuwa nilieowa wa mwanzo hana sifa bali namaanisha dunia ni kubwa na wazuri kila siku wanazaliwa, sasa nina haja gani ya kuowa nijifunge huku naweza kila siku kubadilisha kwa mujibu wa nitakaeona ni mzuri zaidi?
Nakuhakikishia kuwa zipo ndowa ambazo zinakwenda vizuri tu na hilo la mkubwa kunyongeka zipo ndowa ambazo mkubwa hubaki na mdogo akashindwa.

Ama hili la kuletewa mtu mwengine mwenzangu nikuulize wanaokwenda nje ya ndowa au kuharibu ndowa za wenzao huwa wanaumme kwa wanaume? Iweje mwanamke kutokana na kuwa na roho nzuri (Wachilia mbali mwamme mwenye roho mbaya) akafanya jitihada za kuharibu ndowa ya mwanamke mwenzake na iweje wewe mwanamme ukijiwa kuwa kinu fulani kinatwangwa na fulani tena wa ndowa ukafanya jitihada ili nawe utwange kinu kilekile?
Mimi sioni kuwa tutaweza kuepuka Biblia au Qurqni katika ndowa, after all si nilishakwambia ndowa toka hapo ni kujinyima uhuru?

Swahiba wangu,kinachofanya niseme unataka kuoa kwa kuongozwa na tamaa zako za kimwili na sio kwa kufuata lengo halisi lililoelekezwa na mwenyezi Mungu ni maneno yako mwenyewe hayo ya rangi ya blue.Wewe unatumia vibaya hii ruhusa kugeuza ufuska na kuuita ndoa.Au maneno yako hapo ndivyo Quran takatifu inavyoagiza hivyo kuwa muoe wake wengi sbb dunia ni kubwa na wazuri ni wengi?

Ofa yako ya kutaka kunifanya mke wa pili iwapo bado sijaolewa naikataa kwa jina la Yesu.Kamwe siwezi kuwa mke wa pili,sbb naamini mim ni malkia mwenye hadhi ya kuwa na himaya yangu peke yangu.Bora niwe bachelor maisha yangu yote kuliko kushiriki mume na mwanamke mwenzangu.

mkuu wangu hata hivyo naona kama nimekutupia shutma nyingi nikasahau kuwa wewe sio mwenye makosa,wenye makosa ni hao wanawake wanaokubali kuolewa uke wenza.Wangekua wanakataa sidhani kama mngepata nafasi ya kuona kuwa wanawake ni kama mashati,ukiona ya kwanza yamepauka hayana mvuto tena unakwenda dukani kutafuta zuri linalovutia.
Nakutakia kila la kheri mkuu wangu ktk ndoa yako ya pili,usinisahau ktk pilau.
 
Back
Top Bottom