Uchaguzi 2020 Sitaki kuwa mnafiki. WanaCCM awamu hii tunaburuzwa na Mwenyekiti

Hapana. Sinufaiki na utawala huu zaidi ya kuwa na nafasi ya kufanya biashara zangu bila vita na machafuko. Silaha za jadi za nn kwenye kura sasa? Kukishatokea machafuko tutafanyaje kazi sasa?
 
Kwa nini bado uko kwenye chama?
 
Kondoo? Au kondoo ni watu kama wewe ambao kazi yenu ni kupinga tu hata jambo ambalo mnanufaika nalo. Wanachama wa Ccm wameona kazi aliyoifanya ndio maana wamempa kura kwa 100%. Subiri JNHPP ikamilike ule matunda ya Ccm.
Awe dictator huko ccm au la hilo ni swala la ccm. Huku nje raia hawaoni huo udictator, raia mwenye duka mbagala udictator wa mwenyemiti wa ccm unamuhusu nn? Kuhimiza watu waende kupiga kura na silaha za jadi ni ubinafsi wa hali ya juu kwa raia wasiojali udictator unaoimbwa. Wapo raia wanataka uhuru wa biashara na kufanya kazi, machafuko si rafiki kwa biashara.
 
3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).
Duh poleni aisee,huyu Mzee ilitakiwa asiachwe kuwa na mamlaka makubwa hivi mwanzoni kabisa wakati wa utawala wake. Nahisi hata kinana aliachia uongozi wa chama baada ya kushindana nae na kuona anaenda kujimilikisha chama.

Mwisho wa siku baada ya kuwaminya wapinzani sasa amewaminya ndani ya chama,hii ni tabia ya madikteta wote,hapa tushapata rais wa maisha hatuna ujanja. Mamlaka yamempa upofu Mzee kwani anaona hakuna mtanzania mwingine anaeweza fanya kama yeye.

Sifa za kinafki anazopewa,anavyo abudiwa,jinsi anaogopwa,ana tetemekewa ana amini watu wanafanya hivyo toka moyoni mwao wakati sio kweli. Anaweza kuja kufia madarakani au kupata anguko la aibu kama wakina Mugabe, Mutharika,compaore, Mubarak, bouteflica na wengineo. Tuendelee kufanya kazi tu muda ndiye mwamuzi bora.
 

Lakini kweli kwa katiba ya ccm Nec wangetakiwa kutoa wagombea watatu kwenda mkutano mkuuu
 
Demokrasia bila miongozo ni vurugu. Kwa maono yangu demokrasia ilikuwepo na watu tuliiona kwa maono yetu. Bila kufanya vile mkutano ungetumia siku 20
 
Pole kama ndio umegundua Juzi baada ya kuanza Mkutano Dodoma.
 
Litakuwa ni kosa kubwa kuua upinzani uliojengwa kwa jasho. Ccm hakutakuwa salama upinzani ukifa
 
Kwa nini bado uko kwenye chama?
Mkuu kuondoka ktk chama awamu hii Kuna kaugumu. Si unaona walio ondoka wanarudi? Jaribu kufunua chini ya kapeti kujua kwann wanarudi
 
Inasikitisha na kuumiza.
 
Mzee kwani anaona hakuna mtanzania mwingine anaeweza fanya kama yeye.
Anajiona yeye tu ndani na nje ya chama kuwa ndiye mjuaji. Hii hatari sana. Mm kanikera hatari.
 
Hama chama unaleta utopolo wako humu ndani tukusaidie nini...
 
Tatizo mnawaza Chuchu sana...na kupiga push ups.
 
Hama chama unaleta utopolo wako humu ndani tukusaidie nini...
Nihame niende wapi wakati huko upinzani ndiko mbinyo na vilio vilikoanzia? Yaani niondoke kwenye majivu nikimbilie kwenye moto? Hivi unadhani akina Kinana, Nape na Makambas wanaomba radhi hivi hivi tu. Au kina Sumaye na Lowasa wanarudi ccm kwa kupenda? Kuna makubwa yaliwapata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…