Uchaguzi 2020 Sitaki kuwa mnafiki. WanaCCM awamu hii tunaburuzwa na Mwenyekiti

Uchaguzi 2020 Sitaki kuwa mnafiki. WanaCCM awamu hii tunaburuzwa na Mwenyekiti

Ni vyema kama ni kushiriki kupiga kura watu wahimizwe kwenda na silaha za jadi. Ila kwenda kupiga kura kama wanaenda kwenye nyumba za ibada ni utani. Uchaguzi wa safari hii kama wapinzani wamekubali kushiriki chini ya tume hii, wajiandae kwa machafuko zaidi kuliko kinyume chake.
Hapana. Sinufaiki na utawala huu zaidi ya kuwa na nafasi ya kufanya biashara zangu bila vita na machafuko. Silaha za jadi za nn kwenye kura sasa? Kukishatokea machafuko tutafanyaje kazi sasa?
 
Kondoo? Au kondoo ni watu kama wewe ambao kazi yenu ni kupinga tu hata jambo ambalo mnanufaika nalo. Wanachama wa Ccm wameona kazi aliyoifanya ndio maana wamempa kura kwa 100%. Subiri JNHPP ikamilike ule matunda ya Ccm.
Awe dictator huko ccm au la hilo ni swala la ccm. Huku nje raia hawaoni huo udictator, raia mwenye duka mbagala udictator wa mwenyemiti wa ccm unamuhusu nn? Kuhimiza watu waende kupiga kura na silaha za jadi ni ubinafsi wa hali ya juu kwa raia wasiojali udictator unaoimbwa. Wapo raia wanataka uhuru wa biashara na kufanya kazi, machafuko si rafiki kwa biashara.
 
3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).
Duh poleni aisee,huyu Mzee ilitakiwa asiachwe kuwa na mamlaka makubwa hivi mwanzoni kabisa wakati wa utawala wake. Nahisi hata kinana aliachia uongozi wa chama baada ya kushindana nae na kuona anaenda kujimilikisha chama.

Mwisho wa siku baada ya kuwaminya wapinzani sasa amewaminya ndani ya chama,hii ni tabia ya madikteta wote,hapa tushapata rais wa maisha hatuna ujanja. Mamlaka yamempa upofu Mzee kwani anaona hakuna mtanzania mwingine anaeweza fanya kama yeye.

Sifa za kinafki anazopewa,anavyo abudiwa,jinsi anaogopwa,ana tetemekewa ana amini watu wanafanya hivyo toka moyoni mwao wakati sio kweli. Anaweza kuja kufia madarakani au kupata anguko la aibu kama wakina Mugabe, Mutharika,compaore, Mubarak, bouteflica na wengineo. Tuendelee kufanya kazi tu muda ndiye mwamuzi bora.
 
Mimi naona mnastahili kuburuzwa, acha awaburure mpaka akili iwakae sawa, kama chama ni chenu na katiba inaeleza wazi (kwa mujibu wa bashiru) kwamba palitakiwa kuwa wagombea watatu ili wapigiwe kura, ilikuwaje mkakubali katiba ikiukwe, anachukua fomu mtu mmoja halafu wakati wa kupiga kura anasimama hapo anawaangalia, nyie kwanini msimtoe awaachie chama ?, Demokrasia ni msamiati mgumu sana kwa sisi waafrika.

Lakini kweli kwa katiba ya ccm Nec wangetakiwa kutoa wagombea watatu kwenda mkutano mkuuu
 
Anachokitaka ndicho huwa. Na anafanya mambo kwa manufaa yake ya kisiasa. Kwanini nasema haya??

1. Angalia namna mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea urais wa JMT ulivyokuwa na figisu. Eti wanaCCM wengine hawaruhusiwi kuchukua fomu. Ni yeye tu.

2. Angalia chaguzi za marudio ktk majimbo ambayo wabunge wapinzani "waliunga mkono juhudi". WanaCCM tulinyimwa kushindana nao. Na hata ktk uchaguzi huu tumepigwa marufuku kushindana nao.

3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).

4. Kwa kinywa chake mwenyewe amesema kura za maoni za watia nia wa ubunge hazina maaana. Yeye amesema anaweza kumchukuwa hata mtu wa mwisho. Yaani badala ya wagombea kutafuta ridhaa ya wananchi, Sasa wanasubiri maamuzi binafsi ya mwenyekiti.

Demokrasia imezikwa rasmi ndani ya CCM. WanaCCM tunapelekwa pelekwa tu.
Demokrasia bila miongozo ni vurugu. Kwa maono yangu demokrasia ilikuwepo na watu tuliiona kwa maono yetu. Bila kufanya vile mkutano ungetumia siku 20
 
Anachokitaka ndicho huwa. Na anafanya mambo kwa manufaa yake ya kisiasa. Kwanini nasema haya??

1. Angalia namna mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea urais wa JMT ulivyokuwa na figisu. Eti wanaCCM wengine hawaruhusiwi kuchukua fomu. Ni yeye tu.

2. Angalia chaguzi za marudio ktk majimbo ambayo wabunge wapinzani "waliunga mkono juhudi". WanaCCM tulinyimwa kushindana nao. Na hata ktk uchaguzi huu tumepigwa marufuku kushindana nao.

3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).

4. Kwa kinywa chake mwenyewe amesema kura za maoni za watia nia wa ubunge hazina maaana. Yeye amesema anaweza kumchukuwa hata mtu wa mwisho. Yaani badala ya wagombea kutafuta ridhaa ya wananchi, Sasa wanasubiri maamuzi binafsi ya mwenyekiti.

Demokrasia imezikwa rasmi ndani ya CCM. WanaCCM tunapelekwa pelekwa tu.
Pole kama ndio umegundua Juzi baada ya kuanza Mkutano Dodoma.
 
Na ile kauli yake ya kuwaambia Wapinzani hawatashinda uchaguzi wa mwaka huu nayo ina ukakasi na inatukatisha tamaa wapenda mabadiliko.

Mzee huwa anaongea tu kila kinachomjia mdomoni mwake. Hana utaratibu wa kuchuja kwanza ili kuondoa mkanganyiko usio na tija.
Litakuwa ni kosa kubwa kuua upinzani uliojengwa kwa jasho. Ccm hakutakuwa salama upinzani ukifa
 
Kwa nini bado uko kwenye chama?
Mkuu kuondoka ktk chama awamu hii Kuna kaugumu. Si unaona walio ondoka wanarudi? Jaribu kufunua chini ya kapeti kujua kwann wanarudi
 
Magufuli ni symptom tu ya uozo tunaolea wa kukubali kuwa na Rais mwenye absolute powers. Akina BWM na JK nao wamelea mfumo huo kwa jeuri na kiburi ingawa, Leo hii, nao wameishia kuhukumiwa na kudharauliwa kwa kuharibu nchi kiasi cha mrithi wao kudai eti anahangaika “kuinyoosha na kurudisha heshima iliyopotea” huku akifanya vituko vya kila aina vingine vikiwa aibu tupu!
Inasikitisha na kuumiza.
 
Mzee kwani anaona hakuna mtanzania mwingine anaeweza fanya kama yeye.
Anajiona yeye tu ndani na nje ya chama kuwa ndiye mjuaji. Hii hatari sana. Mm kanikera hatari.
 
Hama chama unaleta utopolo wako humu ndani tukusaidie nini...
 
Tatizo mnawaza Chuchu sana...na kupiga push ups.
 
Hama chama unaleta utopolo wako humu ndani tukusaidie nini...
Nihame niende wapi wakati huko upinzani ndiko mbinyo na vilio vilikoanzia? Yaani niondoke kwenye majivu nikimbilie kwenye moto? Hivi unadhani akina Kinana, Nape na Makambas wanaomba radhi hivi hivi tu. Au kina Sumaye na Lowasa wanarudi ccm kwa kupenda? Kuna makubwa yaliwapata.
 
Back
Top Bottom