Uchaguzi 2020 Sitaki kuwa mnafiki. WanaCCM awamu hii tunaburuzwa na Mwenyekiti

Tuwe wakweli jaman 2020 upinzani ni nani wa kupambana na Magufuli?kwa mikakati ipi na kwa sera zipi muhimu wapinzani wajikite kwenye ubunge na udiwani tu

Huyo magufuli wako ana lipi jipya? Dola isingekuwa inawabeba mbona hata hao wapinzani wangemsimamisha Kingwendu kupambana na huyo magufuli, bado Kingwendu angemshinda! tena kwa kura nyingi tu!

Yaani mtu aliyepata 58% ya kura tena baada ya kuchakachua na kuharibu mifumo mingine ya kuhesabu hizo kura, anaweza kushinda kweli uchaguzi Huru na wa Haki!!!!
 
Udiktena hauletwi na raisi bali unaletwa na vyombo vya dola bila vyombo vya dola hakuna dikteta maaana hata akisema fanyeni hivi vyombo vya dola mahakama na bunge vikikataaa huwez endelea kuwa raisi ivo udikteta huletwa na vyombo vyote vya ulinzi bunge na mahakama
Katiba kaka. Kama anateua wakuu wa vyombo hivyo vya dola na vya maamuzi, unategemea nini kama si kusifu na kuabudu ?!. Na hii nguvu anaipata through katiba hii ya Msekwa (1977).
 
Na ile kauli yake ya kuwaambia Wapinzani hawatashinda uchaguzi wa mwaka huu nayo ina ukakasi na inatukatisha tamaa wapenda mabadiliko.

Mzee huwa anaongea tu kila kinachomjia mdomoni mwake. Hana utaratibu wa kuchuja kwanza ili kuondoa mkanganyiko usio na tija.
Ndio uwezo wa CPU yake kuchakata mambo, inakuja kumpa cha kusema wakati asharopoka.
 
Natabiri watakaosimamia uchaguzi kuuliwa hasa pale watakapo tangaza matokeo kwa amri ya jiwe na sio kwa idadi ya kura
 
Anachokitaka ndicho huwa. Na anafanya mambo kwa manufaa yake ya kisiasa. Kwanini nasema haya??

1. Angalia namna mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea urais wa JMT ulivyokuwa na figisu. Eti wanaCCM wengine hawaruhusiwi kuchukua fomu. Ni yeye tu.

2. Angalia chaguzi za marudio ktk majimbo ambayo wabunge wapinzani "waliunga mkono juhudi". WanaCCM tulinyimwa kushindana nao. Na hata ktk uchaguzi huu tumepigwa marufuku kushindana nao.

3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).

4. Kwa kinywa chake mwenyewe amesema kura za maoni za watia nia wa ubunge hazina maaana. Yeye amesema anaweza kumchukuwa hata mtu wa mwisho. Yaani badala ya wagombea kutafuta ridhaa ya wananchi, Sasa wanasubiri maamuzi binafsi ya mwenyekiti.

Demokrasia imezikwa rasmi ndani ya CCM. WanaCCM tunapelekwa pelekwa tu.
Hiyo namba 3 ndiyoimenishangaza,waliweka mtego kutaka kujua mkoa utakao zingua
 
Hutaki mara ngapi? kama umepiga kura ya ndio bila kuridhia basi ndio unafiki huo.
 
Subirini mda wake upite
 
Chama kinajinasibu kuwa na Demokrasia kubwa Sana katika uteuzi na uendeshaji wa chama. Iweje Tena malalamiko hayo kwa Sasa, wakati mgombea wenu ameshinda kwa Asilimia 100??
Hakujawahi kutokea duniani kote watu 1822 wakawa na mawazo sawa kwa mtu fulani. Mazingira yaliwekwa kuipata hiyo asilimia. Karatasi za kura zilikuwa zinakusanywa bila kukunjwa na kila mstari ulikuwa na mkusanyaji wake. Anakagua umeandika nn kqbla ya kuichqnganya karatasi ya kura na nyingine.
 
Anachokitaka ndicho huwa. Na anafanya mambo kwa manufaa yake ya kisiasa. Kwanini nasema haya??

1. Angalia namna mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea urais wa JMT ulivyokuwa na figisu. Eti wanaCCM wengine hawaruhusiwi kuchukua fomu. Ni yeye tu.

Chama hakikuzuia mtu kuchukua fomu, mbona hukuchukua?!

2. Angalia chaguzi za marudio ktk majimbo ambayo wabunge wapinzani "waliunga mkono juhudi". WanaCCM tulinyimwa kushindana nao. Na hata ktk uchaguzi huu tumepigwa marufuku kushindana nao.
Huu ni utamaduni , mpya , hata Makanga aliporudi CCM wakati wa Mkapa aliiachiwa, hata Lowasa aliporudi Chadema aliachiwa, inawezekana hata Membe mtamuachia kama Maalim Seif alivyoachiwa, au mbowe alivyoachiwa u sultan CHADEMA. Kila chama na utamaduni wao.

3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).

Ni utamaduni wa siku zote wa CCM , kuanzia kukaa , kupiga kuara nk acha kupotosha!

4. Kwa kinywa chake mwenyewe amesema kura za maoni za watia nia wa ubunge hazina maaana. Yeye amesema anaweza kumchukuwa hata mtu wa mwisho. Yaani badala ya wagombea kutafuta ridhaa ya wananchi, Sasa wanasubiri maamuzi binafsi ya mwenyekiti.

Naomba uelewe kuwa kura za maoni siyo kigezo pekee, viko vingi kama kura za maoni, mapendekezo ya kamati ya Siasa ya wilaya, Halmashauri ya CCM Mkoa, Kamati Kuu na Mwisho Halmashauri Kuu ya Taifa itatoa uamauzi kwa kuzingatia yote zikiwemo taarifa za upekuzi. Utaratibu huu uko tangu mwalimu mpaka leo, Slaa alikatwa CCM Karatu 1995, Adamjee Kawe, Manji igamboni, hata vyama vyenu vya upinzani rekodi hizo tunazo pia usipotoshe. Huyo pia alikuwa JPM.

Demokrasia imezikwa rasmi ndani ya CCM. WanaCCM tunapelekwa pelekwa tu.
Hamia kwenye Demokrasia za kusubiri CCM ikate/kufukuza watu ndiyo mpate wagombea.
 
Na ile kauli yake ya kuwaambia Wapinzani hawatashinda uchaguzi wa mwaka huu nayo ina ukakasi na inatukatisha tamaa wapenda mabadiliko.

Mzee huwa anaongea tu kila kinachomjia mdomoni mwake. Hana utaratibu wa kuchuja kwanza ili kuondoa mkanganyiko usio na tija.
Yule ni mwwnyekiti wa ccm, sasa unataka aseme chadema mtashinda?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom