Duh poleni aisee,huyu Mzee ilitakiwa asiachwe kuwa na mamlaka makubwa hivi mwanzoni kabisa wakati wa utawala wake. Nahisi hata kinana aliachia uongozi wa chama baada ya kushindana nae na kuona anaenda kujimilikisha chama.
Mwisho wa siku baada ya kuwaminya wapinzani sasa amewaminya ndani ya chama,hii ni tabia ya madikteta wote,hapa tushapata rais wa maisha hatuna ujanja. Mamlaka yamempa upofu Mzee kwani anaona hakuna mtanzania mwingine anaeweza fanya kama yeye.
Sifa za kinafki anazopewa,anavyo abudiwa,jinsi anaogopwa,ana tetemekewa ana amini watu wanafanya hivyo toka moyoni mwao wakati sio kweli. Anaweza kuja kufia madarakani au kupata anguko la aibu kama wakina Mugabe, Mutharika,compaore, Mubarak, bouteflica na wengineo. Tuendelee kufanya kazi tu muda ndiye mwamuzi bora.