Sitakuja kumsahau huyu daktari kwa alichonifanyia

Sitakuja kumsahau huyu daktari kwa alichonifanyia

Wakati najifungua mtoto wangu wa kwanza kuna daktari nafikiri alikua bado ni mwanafunzi Muhimbili alinishika mkono kwa zaidi ya lisaa limoja wodini akinituliza, na kunitia moyo.

Yule daktari alikaa pembeni ya kitanda changu akawa ananiambia itakua fine, itakua fine, kwa sababu niliingiwa hofu (anxiety) nikawa nalia nasema “naogopa”.

Hakunifokea wala kuniongelesha kwa ukali na alielewa situation yangu (nilienda hospitali kliniki yangu ya mwisho kumbe tayari nimeshaingia kwenye labour bila kujijua, nikabaki hospitali kujifungua bila kutarajia)! Sitasahau alivyonicomfort na kubaki na mimi wodini mpaka mume na mama yangu walivyofika. Na aliendelea kubaki wodini mpaka nilivyojifungua masaa mawili baadaye.

View attachment 3276598

Ule moyo wake ulinigusa sana, huwa namkumbuka mara kwa mara na kumuombea mema. Sikuwahi kukutana naye tena baada ya kujifungua na sijui yuko wapi. Natumai popote alipo anazidi kubarikiwa sana.

Nani alikutendea wema kwenye kipindi chako cha uhitaji hautakuja kumsahau?
Ni mimi hapa pole sana kwa hali ulopitia
 
Hiv ni kwann wamama wengi wakitoka kupima njia huwa wanalia sana na wengine hadi damu kwani huwa mnawafanya nin au mnawafinya🤣🤣🤣
Kwa mama zetu wa kimatumbi sijajua hilo wala sijaona toka nipo makole pale dodoma.
 
Back
Top Bottom