Wakuu, heshima kwenu!
Moja kwa moja kwenye mada.
Mtajwa hapo juu ni mchapakazi, tatizo lake kubwa simuoni kama mzalendo wa kweli.
Tayari alishajihusisha na makundi, makundi ambayo yanalaumiwa kwa kukosa uzalendo.
Karata ya CCM 2015 ilikuwa nzuri, pengine kuliko zote baada ya ya Nyerere. Magufuli did the best, alijitoa kwa mwili na roho. Alichopungukiwa ni kutojua namna ya kuishi na mabepari, akawa mjamaa kupitiliza.
Nchi yetu sasa inahitaji Rais aina ya Magufuli, mzalendo wa kweli na jasiri. Mjamaa lakini mwenye kujua namna ya kuishi na mabepari.
Tunao watu wengi, ambao hata wakiongea unausikia uzalendo ndani ya sauti zao.
Ukiacha ile kufanya kazi kwa maelekezo ambapo hutakiwi kumkatalia wa juu yako zaidi ya kumshauri, nauona uzalendo wa kweli ndani ya Humphrey Polepole, Dk Bashiru, Tundu Lisu lakini pia hata Luhaga Mpina. Hawa ni baadhi ya watu ambao wakiandaliwa vizuri wanaweza kutufikisha.
Natamani baada ya Samia anayefuata atoke team uzalendo na sio zile team.... sijui team Lowasa nk. Mambo ya Mwitongo tuyaweke pembeni kwanza.
Nchi yangu Tanzania, nakupenda kwa moto wote!