Pre GE2025 Sitamlaumu tu aliyehujumu uchaguzi bali hata aliyehujumiwa kisha akakaa kimya bila kuchukua hatua stahiki

Pre GE2025 Sitamlaumu tu aliyehujumu uchaguzi bali hata aliyehujumiwa kisha akakaa kimya bila kuchukua hatua stahiki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Kuanzia leo, sitamlaumu tu aliyehujumu uchaguzi bali hata aliyehujumiwa kisha akakaa kimya bila kuchukua hatua stahiki.

Kwa miaka mingi, vyama vya upinzani vimekuwa vikilalamika kwamba wameibiwa kura, lakini malalamiko haya yamekuwa bila matokeo yoyote kwa sababu hakuna hatua stahiki zinazochukuliwa. Hali hii imefanya wizi wa kura uendelee na kushamiri mwaka hadi mwaka.

Kukomesha tabia ya wizi wa kura kunahitaji hatua kali mara moja tu, na baada ya hapo hakuna mtu atakayethubutu tena kuiba kura. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Kama utamkuta mwizi akikuibia nyumbani kwako kisha ukamtazama tu na kumwacha bila kumtandika makofi, utakuwa umetenda dhambi kubwa sana."

Kukomesha wizi wa kura kunahitaji kushughulikia kikamilifu yeyote aliyehusika kwa namna yoyote ile kuiba au kuhujumu uchaguzi. Dawa ya moto ni moto. Njia hii ikitumika mara moja tu, hakuna mtu atakayethubutu tena kuiba kura au kuhujumu uchaguzi siku nyingine, kwani watakumbuka athari zilizowapata wale waliowahujumu uchaguzi kabla yao.

Kutokana na wizi wa kura na kutochukua hatua zozote stahiki, wezi wa kura wanajisifia hadharani bila hofu yoyote kwamba wasiposhinda kwa uhalali, wana mbinu nyingi za kuiba kura. Wanasema ushindi wa uchaguzi unatokana na anayehesabu kura na anayetangaza matokeo. Hii inaonyesha jinsi wizi wa kura ulivyoenea.

Vyama vya upinzani, acheni kulalamika tu bila kuchukua hatua kali zaidi mara mnapoibiwa kura.
 
Back
Top Bottom