Sitasahau biashara ya uchimbaji ilivyonifilisi

Sitasahau biashara ya uchimbaji ilivyonifilisi

Nipo Geita kiutafutaji kwa miaka 6 sasa. Mwaka 2017 kuliibuka machimbo jirani na ninapoishi.

Kama utakuwa una ABCs za uchimbaji mdogo wa dhahabu, kuna mashimo mafupi (sesa) na marefu (Rongo).

Hayo machimbo yalilenga sesa yaan ni kuchimba ft 15-20 unakuwa ushapata udongo wenye dhahabu.

Nikaona bora nijitose kwenye uchimbaji huu rahisi. Nikasaka mashimo (wenyewe wanaita maduara) ambayo wameshaanza na wanahitaji mfadhili wa chakula.

Nikapata maduara 3 ambayo nilianza siku hiyo hiyo kuhudumia chakula. Nikiwa na matumaini ya kupata mafanikio baada ya siku 3 za kazi.

Duara linatembea mara naambiwa inahitajika kamba. Nikaona sio mbaya nikanunua za kutosha.

Kazi ikapigwa weee, mara duara limekuwa refu sasa wanahitaji rola ya mti ili iwarahisishie kuvuta mchanga chini. Kidume nikaona poa tuu mzigo si unakuja.

Hapo katikati jamaa wakaomba vitu kama tochi, betri, pesa ya kunoa vitendea kazi, nikaona sio mbaya siku zimekaribia.

Kisanga kilipoanza sasa

Lile eneo lina maji mengi sana maji ya pale mzungu aliyapigia saluti lakini tukamuona hana akili.

Tukumbuke nilishika duara 3. Watendakazi wa duara 2 walikuwa wanajua wanachokifanya wakatoka baada ya kuona hawapati mwamba wa karibu. Hivyo nikabaki na duara 1.

Duara inajaa maji nikatafuta pump ndogo ya kukata maji. Hizi ni pump ndogo zina boya dogo kwa juu ni mahususi kwa visima. Lakini tunalazimisha maduarani.
Zinaendeshwa na jenereta.

Jamaa anakata maji unalipa 20,000 halafu anaingia kwenye uanachama. Akishakata vile yale yanayotoka kidogo kidogo mnakuwa mnachota kwa dumu hadi wakipumzika labda usiku hapo ndo anakuja tena.

Ikafika stage maji hayafai kuchota kwa dumu. Nikatafuta pump ya kukodi halikupatikana basi kidume nikamwambia bibiye tutafute hela tununue pump full set.
Na yeye akishasikia pesa nyingi huwa anachanganyikiwa kabisa.

Hapo nishachoma hela sina hata 100 kibanda nilichokuwa nacho nikafilisi, huduma hakuna, pesa haiingii, ujenzi nikasimamisha nyumba ilikuwa kwenye lenta sikufunga na tofali ni za choma fikiria mvua zikinyesha.

Basi turudi kwa bibiye. Akasema tutafute mahali tukope. Tukazunguka mjini kutafuta wale jamaa wa kukopesha kwa riba.

Jamaa yangu, ngoja nikuache kwanza hapa weka kumbukumbu. Huku nyuma pale duarani kuna mzee yeye ni kamati ya ufundi.

Kila siku ni kwenda kwa waganga kupiga Ramli na kumpa dawa. Kila mganga anapoenda anaambiwa mambo safi utajiri upo dhahabu itapimwa kwa kilo sio gm tena, ikianza kutoa mtakodisha polisi maana kuna viongozi wakubwa wataitafuta hiyo duara na makorokoro mengine mengi.

Nikaona ni vyema japo sijaenda kusikiliza mwenyewe. Vijana wanahamu ya kazi balaa walikuwa 6 wanapungua wakabaki 3 ikabidi tutafute mmoja wawe wanne.

Hapo katikati kila mmoja anatafuta mganga wake na anawaambia mtapata kwenye duara hiyo.

Hata tuendelee kule mjini. Tulipata jamaa mmoja ni mwal akatukopesha mil 1 kwa riba ya %15 kwa mwezi ah nikaona ndani ya wiki tuu hela isharudi mke wangu akasaini ile hela akaacha kadi.

Tukaingia dukani nikaongezea kama laki 5, ikawa mil 1.5 nikanunua
- Pump ndogo.
- Generator ya kingmax 8800
- Cable
- Pipe
- Na vitu vidogo vidogo.

Kule kambini nikabadili utaratibu wa kula nikanunua unga, dagaa wajipikie.

Nikafikisha mzigo duarani kila mmoja ni shangwe nikajiona mwamba. Kumbe viazi tu.

Jenereta inakula mafuta balaa lita 1 inasaga kwa dk 30 imekausha na inatakiwa kurun muda wote mtu akiwa chini.

Kwa bahati nzuri nikapata wengi wa kuwakatia maji kwenye duara zao hivyo muda wa kupumzika kwangu napeleka generator kwa wengine nachukua hizo 20 20 zao sio haba nikitoa mafuta kwa siku nalala na 50 -70.

Hii ikawa inaendesha shughuli za duarani kwangu. Gharama zikawa kubwa lakini zinapozwa na kufanya kazi pengine.

Duara likatembea likahitaji kufungwa matimba, hii ni miti inayofungwa pembeni nayo hii ni gharama kubwa.

Itaendelea.

Mwendelezo

mara nikaanza kutafuta mdhamini wa matimba......huku na huku hola.....
ikabidi nikomae wapige kazi kibishi japo ni riski.

hapo pump ikaanza msala.
mara kuungua.....mara hitilafu ndogo ndogo tuu....mara jenereta izingue.....maana ngoma ilipiga kazi zaidi ya uwezo wake.

Pump ndogo ikiungua au iki heat.....unatoa nyaya zote na unasuka upya.
kusuka ni 150
kama ina shida ndogo labda kebo imekatika ndani lzma fundi ale 20-30
jenereta ndo nafuu kidogo.

na kipindi kile ilishaungua mara 2.

nikaona hawa jamaa wanapanda na chabo (sampuli ya mwamba ) inaonekana vumbi ya dhahabu na shaba kwa wingi.

hapa watendakazi wanakuambia yaan nina v8 yangu hapo chini.....hii duara sibanduki.....

nikaona niwe nashuka chini.
sio siri nilianza kutumia ponch bila kupenda.
aisee kazi ya chini ni balaa.
unatoka hoi hoi.

balaa lingine tena linaanza.


Tumekuta mwamba mgumu hatari hakuna ponchi ya kutoboa. Ikabidi tuanze mlipuko.
Hapo kidogo akili zikaanza kujikaza sawa.

Huyu jamaa wa kamati ya ufundi ni kuomba tuu nauli aende kwa waganga mara akaja na jibu kwamba kuna mtu wa hivi na hivi ana mkosi inatakiwa aje aoshwe maana huyo ndo ameshika utajiri wenu .
Yeye ndo atapata mwamba wa mali katika shift yake na blaa blaa nyingi.
Kidume nikaona kumbe issue ndogo tuu nikamwambia aende na gharama zote kwangu..

Kumbuka duara inahitaji miti(matimba)
Nikapeleka kibabe sasa tumekuta jabali gumu (westi) linahitaji mlipuko na haiwezi kurongwa kabla ya kufungwa miti (matimba)

Nikaanza gharama za miti na fundi ikala 300's kwa kuibania maana.
Nikaleta compressor ikadrill tundu 3 kwa gharama ya 100's
Tukalipua lkn haikuweza kuvunja mwamba sehemu kubwa.

Hapo na mimi nishaanza kuzunguka kwa waganga.... wanasema ukitoa hilo jiwe gumu tu....utaaga umasikini.
Ilikuwa changamoto sana kwenda kwa waganga ukizingatia jinsi jamii inavyonichukulia huku....mtu wa kanisani nn...... Dha nakumbuka siku niliwahi kubadili njia na kuzuga kutafuta punda nikiwa natafuta mganga nioijicheka sana.

Mlipuko wa kwanza haukauweza kumaliza lile jabali....ikabidi nirudie tena
Hapa nikatumia drilla wa mkono cha ajabu fataki hazikulipuka.....akatega tena mambo yakawa yale yale.
Nikarudisha compressor....tunapiga tena 3 lkn jabali bado ipo.

Hapo msosi unatembea kinyama ...msosi mkuu ni ugali dagaa.
Washenzi wakaota vitambi huku mimi nakonda mbaya sana


Jamaa wa pembeni wananipamba....jamaa komaa hapa umepita mkanda kabisa
Tangu nichukue ile mil miezi inasonga inalipiwa riba....na nikikwama naenda kuongeza...mara 300 mara 200 deni linakuwa tuu.


Nakiri wazi hadi mama mkwe nilimkopa.

enzi hizo nilikuwa na Samsung Galaxy Grand....ikaibwa nimelala juubya duara....
Vita ikaanza home.
Nakumbuka siku mama aliniomba ela ya kuvuna kama laki nikamwambia wiki ijayo nitakuwa na ela nyingi we kopa mahali.....ikawa kimya ....
Akanirudia tena naomba 21000 nijaze gesi ndogo nimpikie mzee....nikamzungusha hadi akachukua.

Baba hataki niendelee na uchimbaji.
Mke wangu ana mimba miezi 8 na ndani hakuna ela zaidi ya madeni.

Duara zimerefuka hadi ile pump ndogo inashindwa kuvuta maji sawa sawa inahitaji niletee pump nyingine.

Tena ninza kukodi unalipa 600 kwa mwezi....mafuta na ukarabati ni ww

Huku mganga anasema usiache pesa ipo.

Huku wachimbaji wanasema michirizi inaenda kuungana hivyo tuendelee.

Nikampigia mzee m1 ni mganga mzuri ananifahamu vyema ila yupo mbali na anaweza kutabiri kwa simu tuu.

Mzee akasema " duara ina mali nyingi ila sioni zikielekea chini. Inaonekana zipo juu sio kwa urefu huo mliopo.
Ushauri wangu isitumie gharama nyingine ya kuchimba....tafuta mtaalamu wa karibu akusaidie.

Hapo kazi nimeanza mwezi wa nane....hapo ni dec mwanzoni mama nawesabia bado wiki 3.

Muda mwingine mke wangu anafanya biashara ndogo ndogo ananipa 20....napeleka duarani.

Muda mwingine nakosa hata nauli ya boda inabidi nitembee kwa saa 1 ....hatari sana.

Nikarudi nyumbani nikamwambia bibiye tupumzike kwanza hii kazi.
Nakumbuka alilia sana.

Maana tegemeo lote ni duara na unavyojua akili za wanawake kwenye pesa nyingi......
Nikarudisha vyombo nyumbani kwa roho ngumu nikarudi kijiweni nikajipanga tena

Mtaji mpesa ulikata...hata vocha haikupatikana tena kijiweni nilibaki nachaji tuu simu.

Nikaanza mdogo mdogo tena nikarudisha hadhi ya kijiwe changu.


Naomba niwaambie kitu kimoja

Hii ni biashara yenye pesa nyingi kama utapatia. Kuna jamaa wananunua magari kama ndala ..... Anajenga kama anajenga banda la mbwa.

Kwa wenye mtaji mdogo ni bora ukaenda kufanya biashara
Peleka chochote utauza kasoro pingu.

Chajisha simu ni 500
Tengeneza guest ni 5,000 kwa siku kulingana na wakati.
Hizi zinatengenezwa na turubai au mabati au zile nailoni nyeusi.
Mwizi akija anakuja na kiwembe anaingia ndani....

Biashara ya baa na malaya inalipa sana pia chakula.

Nakiri wazi sijawahi kuchukua malaya wa mgodini maana ni hatari sana.

Ukilala gest chumba kimetenganishwa na capet kama kuna malaya humo unasikia kila kitu. Huwezi lala .

Ugomvi ndo kwao kule ila wenye roho nzuri ni wengi sana.

Mwanangu alizaliwa salama sasa anatimiza miaka 2.
Madeni tulimaliza na ile nyumba ilibidi ninunue tofali 8,000 kama za mwanzo ndo nikaweza kumaliza maana tofali nyingi ziliharibika na sehemu ya ukuta kuanguka.
Sasa nimefunika nategemea kufikia June 2020 niwe kwangu.

Naomba niishie hapa kama kuna maswali nitayajibu .

Samahani kwa uandishi mbovu nimewachosha wengine.

Likowapi hiro duara tuliendeleze?

Nina uzoefu sana na haya mambo.
 
Na Mimi nimeingia mgodini rasmi nitaleta mrejesho. Huwa sikatishwi tamaa na story Kama hizi, huwa nazichukua kujifunza namna ya kupambana na changamoto lakini sio kuzikimbia changamoto

Nimevuta crusher kabisa Bei unajua na kujenga mwalo.. sitalia nitapambana mpaka pumzi ya mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndio kidume inatakiwa hivyo, mkuu na mimi nakusanya pia vifaa nipe mrejesho ntakua jirani yako, wapi ulipo?
 
Nakumbuka siku moja nilitoka na kutafuta mganga mmoja hivi.....
Nilikuwa naenda kwa mganga mwingine...nikapotea njia nikafika kwake
jamaa akaniuliza kama nimekuja kwake kwa hiari au nimekosea....nikamwambia we fanya kazi.
nikaweka jiwe chini jamaa akasema " hapo hakuna kitu...hata kama utapata utapata kidogo sana hakita rudisha cost.

nikasema basi......nikakung'uta miguu nyuma kama nzi.


kuna mganga mwingine huyu aliniambia ana dawa ya kusogeza mwamba....analeta juu

mwingine akasema ana uwezo kwa kunipa dawa niende GGM kwenye stoo ya dhahabu nichukue pure gold. Yaan vile vitofali kisha nirudi.
kasharti yake nisigeuke tuu nyuma.

Anasema ashasaidia wengi na hapo ana miradi mingi ....nikamwangalia.....hafanani na asemayo nikaona hapa chawa.

Simu kafunga na rababendi...
anaomba salio
Suruali hazieleweki...
mkanda ni uzi......
begi la kazi ni shida.....

nyumbani kwake ni shida tuu.....

hawa jamaa ni shida sana

Inakuaje mnawaamini waganga wanaoongea uongo mkavu kiasi hiki?
 
Pole chief.
Hii biashara kwa hapa nilipo 99% inafanyika kwa ushirikina.
Ili upate ni lzm uwatumikie wakuu wa giza
Hata wachungaji wa makanisa ni washiriki wazuri tuu.
Matajiri wenye migodi yao mikubwa wanafanya kwa siri sana japo kuwa wana vifaa vya kisasa.

Hawa wenzetu weupe (wachina wazungu) sijui wanafanyaje ila kafara kwao ni kugusa tuu
 
Huo ukware ndio kitu gani? Unapigwaje? Ni kutafutia mahawara watu au? Hebu elezea vizuri kidogo Mkuu.
Ni eneo mawe yanaporundikwa kutoka chini...mawe yanatoka huko chini yakifika juu yanamwaga...mawe yakishauzwa pale chini kunakua na vumbi la dhahabu..so wamama wanakuwa wanatembea na vidude Kama spatula ..wanakwagua had udongo...wakienda kuosha wanapata dhahabu..ukijidamka mapema au ukiwa sharp na eneo ulipo kukawa na mzigo .mzuri wanaodoka had na gram moja!
Lakini ni kazi ngumu Sana...kisukuma kwingi...maana inakupasa kuwa mtata pia upate eneo ukwangue...wenye maduara wanaweza kuniambia uwape buku 2 au 5 ukwangue. So ukilipia atleast inakuwa Bora unakwangua kwa Uhuru..
Ukware mwingine ni eneo la mwaloni kwako....Kwasababu unasaga hapo na kuosha lazima Kuna vidhahabu vitakuwa vinadondoka...so ukishamaliza kazi kbs hapo mwaloni kwako namansha unataka kuuza kifusi unauza hiyo place yako wanakuba wajuzi wanakwanguaaaaaa....yaan ukiangalia ni mchanga tu lakini una dhahabu..km ulikua unanunua mawe mazuri hukosi 300k!
 
Mkuu unapokuwa na shida hata ukiambiwa m***i Ni dawa sharti utumie
Ajabu mnaendaga kwa waganga na hakuna mafanikio..dah..mie sitaki a chanjwa Michale kisa mganga kasema nikichwanjwa nitazifumnia dhahabu...arghh...99%watu wa migodini Wana chale balaa🙌🙌😀😀🤸!Imani hizi
 
Ni eneo mawe yanaporundikwa kutoka chini...mawe yanatoka huko chini yakifika juu yanamwaga...mawe yakishauzwa pale chini kunakua na vumbi la dhahabu..so wamama wanakuwa wanatembea na vidude Kama spatula ..wanakwagua had udongo...wakienda kuosha wanapata dhahabu..ukijidamka mapema au ukiwa sharp na eneo ulipo kukawa na mzigo .mzuri wanaodoka had na gram moja!
Lakini ni kazi ngumu Sana...kisukuma kwingi...maana inakupasa kuwa mtata pia upate eneo ukwangue...wenye maduara wanaweza kuniambia uwape buku 2 au 5 ukwangue. So ukilipia atleast inakuwa Bora unakwangua kwa Uhuru..
Ukware mwingine ni eneo la mwaloni kwako....Kwasababu unasaga hapo na kuosha lazima Kuna vidhahabu vitakuwa vinadondoka...so ukishamaliza kazi kbs hapo mwaloni kwako namansha unataka kuuza kifusi unauza hiyo place yako wanakuba wajuzi wanakwanguaaaaaa....yaan ukiangalia ni mchanga tu lakini una dhahabu..km ulikua unanunua mawe mazuri hukosi 300k!
Wangari Nina laki 5 hapa nipe dili ndogo nijilipue pande hizo kwa kadri ya huo mtaji.
 
Ajabu mnaendaga kwa waganga na hakuna mafanikio..dah..mie sitaki a chanjwa Michale kisa mganga kasema nikichwanjwa nitazifumnia dhahabu...arghh...99%watu wa migodini Wana chale balaa🙌🙌😀😀🤸!Imani hizi
Kwenye uchimbaji sio lazima chale.
Chale Ni kwa ajili ya kuingiziwa dawa mwilini dawa za kujiponya, kujilinda, bahati,nk.
Ila migodini ni kusafisha duara na kuvuta bahati na kafara za vikuku. Hizi mnzfanyia duarani sio mwilini
 
Wangari Nina laki 5 hapa nipe dili ndogo nijilipue pande hizo kwa kadri ya huo mtaji.
Kafanye m-pesa wakati unajimix na watu kujua abc!
Wewe nakuonaga uko vzr kichwani...nenda kajichanganye na matajiri wanaonunua vifusi ..ujue wanafanyeje...ukirud mjini tafuta 10m uanze nunua vifusi vile vidogo dogo walau ujaze Tanki 5!ulinunua kifusi tuseme vifusi vi4 kwa watu tofauti unatumia 10m hukosi 5m as faida...!yaan Juana na wenye plant na mafekechee Kama hayo usiwe unakaa folen...!
 
Kwenye uchimbaji sio lazima chale.
Chale Ni kwa ajili ya kuingiziwa dawa mwilini dawa za kujiponya, kujilinda, bahati,nk.
Ila migodini ni kusafisha duara na kuvuta bahati na kafara za vikuku. Hizi mnzfanyia duarani sio mwilini
😀😀Na maudi yenu😀🤸
 
Back
Top Bottom