Mkuu kwanza nikupe Hongera kwa kuthubutu....
Coz siku zote wanaojaribu na kufanya ndo Wanaofanikiwa.... Kama huwezi kujaribu na kupoteza huwezi kufanikiwa....
Hata hao unaowasema kuwa Wananunua Magari kama Ndala, wamepitia changamoto nyingi na kupoteza sana....
Kama kuna Watu waongo basi ni Wachimbaji wa Madini..... Wanaweza kukutia Moyo kwa kitu ambacho hakipo.... Wakikupigia hesabu wanakwambia hapa Mizamo 3 tumeufikia Mwamba tunaanza kuzarisha.... Wanapokupigia hesabu za kudhamini duara hawakupi hesabu kamili, wanakukadiria hesabu Ndogo tu ya Chakula na Vitendea kazi vichache wastani wa 200,000 ambapo utaona ni ndogo na unaweza kumudu..... Baadaye mkishaanza ndo wanaleta hesabu za vitu vingine.....
Ushauri wangu kwako usiache, Ungewaacha wenyewe waende kwa Waganga n.k ila Wewe ungefanya kazi kitaalam.... Mfano mlipoufikia Mwamba ungepeleka Sample Maabara, ingesoma Kiwango cha Dhahabu kilichomo, then baada ya kuchimba Mita kadhaa ungechukua tena sample Maabara ingekupa majibu kuwa kadri unavyokwenda kiwango cha Dhahabu kinaongezeka ama vipi!?
Kuna sehemu unasema jamaa walipiga chabo ikasoma Dhahabu kidogo na Copper nyingi means ukienda chini zaidi Copper itaanza kupungua na Dhahabu kuongezeka!
Omba Ushauri kwa Wazoefu pia unaweza kuleta Geologist kwenye Duara lako akakushauri.
All in all Hongera na usiache, kusanya nguvu rudi tena, ila fanya kazi kisasa..