Sitasahau biashara ya uchimbaji ilivyonifilisi

Wanapolo ni watu wenye historia nzito sana na zenye mapito magumu na fundishi. Ni kheri umetumegea kiasi ya yale wanayoyasikia wengi mijini kwani ni hali ya shurba sana katika sekta ya madini, nimepata hadithi nyingi ya ndugu zangu waliokuwa mbuguni Arusha mpaka wengine kuokoka hali ni tete sana na mafanikio yake yakikubali ni murua mara 1000.
 
Natamani ningekugongea likes 1,000. Ahsante sana kwa kutushirikisha changamoto na uzoefu wa migodini.
 
Hivi hizo Gest,zinakua na vitanda,mashuka au inakuaje?
Kitanda ni miti inachimbiwa....dogoro lipo la ft 2-3. Shuka zipo ila ni nyepesi.
Zinajengwa kwa miti na kufunikwa kwa capet au karatasi za nailoni. Juu hadi pembeni.......joto lake mchana sasa....hakuna wa kulala mchana.
Au zipo advanced za full bati juu hadi ukuta hii ni ghali zaidi. Chumba elf 5 Hadi 10 kutegemea na Chimbo.
Wanaolala hizi mawa nyingi ni kota(broka) wanunuzi wakubwa wa mawe.... ila mchimbaji halali gest
 
Hivi hizo Gest,zinakua na vitanda,mashuka au inakuaje?
Kitanda ni miti inachimbiwa....dogoro lipo la ft 2-3. Shuka zipo ila ni nyepesi.
Zinajengwa kwa miti na kufunikwa kwa capet au karatasi za nailoni. Juu hadi pembeni.......joto lake mchana sasa....hakuna wa kulala mchana.
Au zipo advanced za full bati juu hadi ukuta hii ni ghali zaidi. Chumba elf 5 Hadi 10 kutegemea na Chimbo.
Wanaolala hizi mawa nyingi ni kota(broka) wanunuzi wakubwa wa mawe.... ila mchimbaji halali gest
 
Ila maisha bwanaaa, unaweza kwama sehemu ktk halakati zako za kuwekeza ukajiona ni ww tu ndyo umefeli, kumbe kuna wengine wamefeli mpk na magonjwa ya pressure wamepata na wengine kufa kabisaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa kuna jamaa kachimbisha duara hadi Kauza nyumba...gari....hadi kaachanana mke
 
mkuu kuna mambo yangu hayaendi naomba namba ya huyo mtaalamu anayeweza kutabiri hata akiwa mbali naomba kuna kitu anisaidie kuna mabwege wananichezea msaada wako tafadhari
Hahahaha...
 
Huyo aliyekwambia uende strong room ya GGM ni tapeli wa kuogopwa, mle kuna Camera kibao na funguo zipo 3, hivi wanazani Mzungu siyo mchawi kuibiwa hawezi aisee.
Anasema huhitaji funguo kwenda.
Unapita kama upepo tu.

Kuna jamaa aliwawezesha wakaenda....wamefika kule wakamkuta mzungu anakata mzigo ....wakaanza kumchezea kwanza.....hakushtuka wakachukua mali wakasepa..ile wanatoka getini muda wao ulikuwa umeisha wamepoteza muda kule ndani..,.wakaonekana

...unaweza kusikia sauti inakuita....uligeuka tu imekula kwako

Ila kwa mimi simwamini
 
Ni kweli ila wachimbaji wadogo hawa afford cost.
Mtaalamu wake ni mganga.
Mbaya unakuta mali ipo mt 100+ kuipata ni ngumu sana.
Kwenye kukata maji walikuwa wanatumia dieseli lita 40 perday....fikiria hapo ufanye mwezi ndo uanze uzalishaji.
Inafika mahali duara inahitaji watu 12 per 1 shift.....fikiria gharama za kuwamudu hapo uwe na shif 2 zote inahudumia ww......
Gharama ni kubwa.
Kama kuna umeme na una mtaji inapunguza gharama za mafuta na watendakazi maana utatumia cren sio kamba ya mkono tena
 
Tulichimba kwa style hiyo lkn tukala za uso
 
Aisee mkuu umenikumbusha 2017, milipoona kilimo hakiendi sawa wafanyakaz wangu walikuja kunishawishi tukachimbe Ruby, nikasema Aluta Continua mtafutaji hachoki tukaenda mpaka kwenye hilo pori mzigo ulipo. Aisee vile vimawe vya damu ya mzee sijui pinki vimetamalaki balaaa.

Mzee nikasema sasa utajiri umefika tukapanga mikakati nikanunua mashoka na makorokoro kibao na msosi mahindi kama debe 6 hivi na maharage.

Kesho yake kazi ikaanza cha ajabu jioni ndo kwanza shughuli imeanza leo dogo mmojawapo kanifuata eti kuna mzee kamwambia aende akachukue mali ya mjerumani. Alarm ikakiliki nikasema mimi hiyo hela sina

Tulikua na mwanangu mmoja na yeye aka join team akasema kabla hatujaendelea mbali tutume sampla tulizonazo Mererani ili watwambie kuna tumaini kiasi gan?

Ebwana kutuma wakasema hiyo siyo ruby ni Rodlite. Nikamwambia mshkaj wangu pesa tulizomwaga shambani zinatosha mimi narudi zangu town yeye akasema haitatokea mimi kuonywa kwa E-mail mimi chalinze nikanyoosha kuja town yeye akakata kushoto mpaka leo yuko Merelani huwa namuungia 20k akikaukiwa mimi ngoja nipambane kwa mkaburu kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…