LA7
JF-Expert Member
- Aug 26, 2019
- 655
- 2,369
Ndugu zangu huu usafiri ni mzuri Ila usipande ile treni yetu ya wanyonge japo gharama zimepishana kidogo, mfano kutoka Tabora mpaka Kigoma ya wanyonge ni 12500 na ile express ni 16100 kwa wakati huo ila sijajua kwa sasa.
Ilikuwa hivi; wakati nasafari kutoka Kigoma kwenda Singida nilikuta train ndio linakaribia kuondoka sasa nikaingia tu nikiamini nitakatia tu tiketi ndani ya tren.
Jamaa wakaja wakanikatia tiketi ila hawakuniandikia siti, japo siti zilikuwepo. Sasa baadae si nikanyanyuliwa na wenye siti ikabidi nisimame tu tiketi yangu ilikuwa nishukie Manyoni ila ikanibidi tu nishukie Tabora maana sio kwa mateso hayo.
Ushauri wangu kwa TRC; waongeze usalama kwenye treni maana mule kuna askari na bunduki kabisa lakini abiria wanaibiwa tu tena kwa kukwapuliwa na vibaka. Jambo hilo huwezi likuta kwenye express, usafiri huo haueleweki kabisa saa ya kuondoka na saa ya kufika unakokwenda.
Watu kukaa njiani na mizigo ndani ya mabehewa, kila kituo kiwe na wakatisha tiketi kuepuka kuwapiga watu faini wakati wamepandia kituoni ila kituo hakiuzi tiketi.
Nimemaliza ya kwangu, ni hayo tu.