Sitasahau nilivyonusurika kuchukuliwa mateka na majambazi mkoani Kagera

Sitasahau nilivyonusurika kuchukuliwa mateka na majambazi mkoani Kagera

Yani 24/7 wageni ukiwasimulia km hivi hawaamini kama mpaka 2005 mitaa hiyo kulikuwa na utekaji
Hawawezi kuamini. Ninamkumbuka RPC Venance Tossi ndio alisafisha issue za utekeaji barabara hiyo na pori la Khimisi. Ilikuwa ikikaribia Krismasi lazima matukio yatokee.
 
Inaendelea............

.....ili nitoe pullover nivae kwa ajili ya kujikinga na kibaridi kilichokuwa kinachoma mwilini mpaka tumboni. Nilikaa pale kwa muda wa saa hivi kisha nikabeba mabegi yangu kuelekea kuitafuta breakfast maana tokea nilipokuwa nimekula jana saa moja usiku nyumbani kabla ya safari sikuwa nimekula tena hivyo nilikuwa nina njaa sana na hivyo nilichukua mabegi yangu nikaanza kupiga hatua za harakaharaka kuitafuta cafeteria moja ambayo haikuwa mara yangu ya kwanza kwenda kupata chochote pale, ilikuwa inaitwa Kishusi sijui Kama bado ipo maana kipindi kile ilikuwa inajitahidi sn kupika na kuuza vyakula vizuri sana vya kishua mjini Bk.
Nilikuwa na wasiwasi maana nilihofia kuwa huwenda wangekuwa hawajafungua lakini nilipofika nilikuta tofauti, nilisukuma mlango wa kioo kisha nikaingia. Niliagiza chai ya maziwa na kababu tano, nikazifuta zote mpk vile visalia vya vipande vidogovidogo vya nyama vilivyokuwa vinabaki kwa sahani nilifuta kabisa. Muhudumu alipokuja kunitajia bill nilijivuta nikasukuma kiti nyuma, ili nipate nafasi ya kumpatia pesa yake. Nikiwa nimekaa niliinama nikaelekeza mikono yangu mguu wa kulia kwenye raba yangu ya Nike nikafungua kamba zake kisha nikashusha soksi chini nikapenyeza mkono kwenye unyayo Kisha nikachomoa pesa noti za rangi ya bluu, miaka hiyo 10k note ndo ilikuwa mekuwa introduced na BOT, nilichomoa moja nikamkabidhi yule dada, muda wote huo alikuwa amepigwaa na butwaa alivyokuwa anashuhudia kile kitendo cha kuchomoa pesa kwenye viatu. Sikumbuki kwakweli nilitumia kiasi gani na chenji ilibaki kiasi gani Ila baada ya kunirejeshea chenji ilibidi nitumie dakika chache sn kutenga nauli na pesa ya kutumia ninapokuwa njiani ili nikishafunga buti (kiatu)nisianze kufungufungua kila mara.Niliwaza kujiondolea usumbufu. Ikumbukwe kuweka hela chini ya nyayo ndani ya soksi nilikuwa na sababu na nilishazoea kufanya hivyo siku zote za safari yangu ya kuelekea shule. Mguu wa kushoto niliweka ada ya shule na sikuwa nimegusa eneo hilo tokea nilipoiweka nikiwa home baada ya kupewa na mzee, na kulia nilihifadhi pesa ya matumizi.

Wakati huo ilishafika saa mbili kasoro, nikapiga hatua chapchap kurudi standi,kipindi kile magari ya abiria yalikuwa ya kuokotaokota Sana kuelekea huko wilayani hivyo Mimi nilishazoea kupanda kwa kuunga unga na siku hiyo nilipofika eneo hilo nilikuta usafiri unaoelekea Mutukula mpakani kabisa mwa Tanzania na Uganda. Nilipanda lile gari na tulipofika Kyaka kabla ya daraja walinishuka pale ili nisubirie usafiri wa kuunga angalau unifikishe Karagwe wilayani, kisha nikifika pale nilale ili nianze tena safari ya kuunga unga mpaka nifike mwisho wa safari yangu.

Nilikaa Kyaka takribani masaa matatu sikuwa nimepata usafiri, yakipita magari matatu ya abilia lakini yalikuwa yamejaa. Nakumbuka gari za abiria mara nyingi zilikuwa ni Land lover. Pia magari binafsi pamoja na ya Mashirika ya Umoja wa mataifa kama UNHCR, Calitas, UNICEF, Help Age niliyashuhudia yakipita nilikuwa nayasimamisha but hayakuwa yakisimama. Sikukata tamaa niliendelea kusubiri, lakini nikiwa pale niliona nijisogeze kwa mmoja wa vijana wengi waliokuwa wanauza ndizi za kuchomo kule zinaitwa gonja tamu sana i see, nilikula kadhaa huku nikisukumia na soda yangu bariiidi kabisa ndizi mbili tu nikatosheka zingine nikahifadhi kula huko mbele ya safari. Nilikaa Kyaka mpaka saa tisa hivi ndipo gari binafsi iliposimama kisha tukapanda na abilia wachache waliokuwepo pale nakumbuka ilikuwa double cabin, wote tulipanda nyuma

Tulianza safari bila ya kuchelewa,
kipindi hicho barabara zilikuwa mbaya, mbaya mbaya kabisa mashimo kwa kwenda mbele na ukichanganya na kipindi hicho mvua zilikuwa zinanyesha mkoani Kagera barabara zilikuwa hovyo kabisa. Kadiri tulivyokuwa tunaiacha misenyi ndivyo jua lilizidi kuelekea usoni kwetu kwa maana ilikuwa linaelekea magharibi.

Baada ya kuwa tumevuka vilima na mabonde na Safari yetu ikingali inaendelea magari yaliyokuwa yanatokea upande tunakwenda sisi yalikuwa hayaji tena, hatukuwa tukiyaona kupishana nayo kama ambavyo ilikuwa hawali ama kipindi kile bado niko Kyaka nasubiri usafiri.Kwa ujumla nilifikiria kuwa ni kwasababu ya muda kuwa umekwenda. Kitu kilichonishangaza ni yale magari ya abiria yaliyokuwa yamenipita pale Kyaka stand na yalishatembea muda mrefu lakini tuliyapia, Ila nilijiambia moyoni kuwa sababu ni mabovumabovu ndio maana tumeyacover na kuyapita.

Tuliendelea na Safari yetu lakini kilomita chache za mwendo tulikuta gari moja limekwama kwenye dimbwi la tope katikakati ya barabara na hivyo likasababisha tushindwe kuendelea na safari kwa kuwa liliziba njia. Tulikaa hapo kwa muda kama wa nusu saa na muda huo yalishafika magari mengi yaliyokuwa yanasubiri njia iwe wazi. Watu tuliokuwa eneo hilo tuliokuwa tumeshuka kabisa kwenye magari yetu tunalandalanda tu huko na huko wakati huo ni saa kumi na mbili jioni. Nikielekea kwenye bag langu nikafungua mfuko wa pembeni nikachukua kidevice changu Cha kuchezea cassette nikatia cassette moja ya 2pac Omary Shakur kisha nikachukua headfone zangu nikaziseti juu ya masikio barabara (Kama DJ vile) nikaanza kula hip hop kali za moto sana kipindi hicho nikikoshwa zaidi na kibao cha 'Dear Mama'

Ile naanza kuenjoy biti nilishtushwa na milio ya risasi .....papapu..papapaa..... zilipigwa mfurulizo Kama dk 5 hivi tena zilipigwa kutokea both sides yaani kule tulikotokea na huko tunakoelekea, sikujua zile headfone ziliacha kichwa muda gani zaidi nilipokuwa nazungusha macho huku na huko niliyaona mabandidu yanameshika siraha yanahamrisha watu tulale kifudifudi muda wa sekunde kadhaa eneo kulikuwa kimyaa.

Mabandidu yakajichukulia utawala wa gafla Katika kale kaeneo tukiwa tumelazwa pale nilishtushwa na mtu akiniinua Kama sisimizi maana alishika ile kofia ya 'pullover' ilivyokuwa imelalia nyuma ya kisogo akanivuta kisha nikamtizama usoni jamaa lilikuwa limevalia siraha Ina mkanda kama wale waasi wa M23, I see jamaa lilinistua na banzi (kibao)moja heavy la usoni, nikaziona nyota na rangi za bluubluu ilochanganyika na rangi ya damu wakati huo akili yangu ikanituma kuwa sikutaka nimtizame usoni though alikuwa amejifunika uso. Kabla sijatafakari nisali Sala gani nikashangaa mtu ameleta gunia akanivika, nilistuka gunia linanivaa, nikajua nimekwenda na maji.

Ubongo wangu ukiwa umefeli kutafakkari niliishangaa wanaletwa watu wengine sikujua ni wangapi Ila nilikuwa nasikia vishindo kuja kwangu Kisha tukaambiwa kwa kiswahili kibovu 'Mutu hakuna kutembeya' Mimi kila kiungo kimoja kilikuwa hakina mawasiliano na kingine maana kwanza nilikuwa mdogo na ndiyo mara ya kwanza nasikia milio ya risasi. Nilikuwa natetemeka Kama generata bovu kuzidi yale majenerata ya mgao wa Umeme ya tanesco.

Kipindi chote hicho nilikuwa nimefunikwa gunia, Kuna Yale magunia ya enzi hizo yalikuwa yanatengenezwa na katani. so hewa ilikuwa inapita na muda wote ule tokea nimepigwa like Kofi nilikuwa nimefumba macho kwa uoga.Lakini nilikaza moyo baada ya kuhisi majamaa yamesogea hatua chache kutoa pale nilipo nikafumbua macho, kupitia kwenye gunia nikaona mabandidu kama wanasearch magari kwa haraka haraka kisha ndio nikaona pembeni yangu tuko kama watano hivi tuliosimama.Hapo hapo bandidu moja likasogea pàle tuliokuwa huku limetulenga na bunduki sikuwa na mawasiliano ya mwili Ila nilihisi mkojo unateremka kutokana na kuhisi maji ya Moto yakiteremka kutoka saizi ya kiuno Hadi chini kwenye viatu. Jamaa alipokaribia na sisi akapiga risasi (nahisi juu) Kisha Mimi miguu ikaishiwa nguvu nikahisi nimepigwa mimi, nikadondoka chini. Chakushangaza jamaa akaja akaniinua tena akanitoa lile gunia kisha akanambia "we mwana we ntakupiga 'rishashi' cha ajabu nikahisi nguvu zimenirejea maana nilidhani ile risasi amenifyatulia mimi na tayari nimeshakufa kumbe nilikuwa hai sina hata jeraha. Basi wale wenzangu nao walikuwa wanapita wameshika magunia yao nyuma yao kuna mabandidu yanasimamia zoezi kama ilivyokuwa kwangu. Mimi nilikuwa mdogo lakini nashangaa hata leo kwanini Yale majamaa yalining'ang'ania kunipa gunia?? Waga najiuliza Sana, kisha wakawa wanatupitisha kwa abiria pâle walipolazwa, ukifikiwa unaamrishwa utoe ulichonacho kila kitu uwe na pesa saa nzuri unatia kwenye gunia hakuna kupoteza muda.Zoezi hilo likiwa linaendelea wakati huo mateka unatekeleza zoezi kichwa ukiwa umeinamisha chini , mijamaa ikawa inasema ukiinua kichwa unakula 'rishashi' Nakumbuka hili jina rishashi mpaka Leo jinsi walivyokuwa wanatamka neno 'risasi'

Ikumbukwe kitendo kile kilichukua dk zisizozidi ishirini hv, na sehemu walipotutekea ilikuwa ni sehemu ya Kona maana waliokuwa wanatokea tunakokwenda walikuwa hawawezi kuona kuna nini kinaendelea na hata waliokuwa wanakuja wasingejua kutokana na ile kona ambayo pale Kati ndio hiyo ambushi ilipofanyika.

Basi, baada ya like tukio kukamilika waliamrisha watu kulala kimya tena uso chini Kisha wakatwambia sisi wenye yale magunia kwa ukali kilammoja abebe furushi alilonalo tuanze kukimbia kufuata njia kuelekea kwenye msitu. Kiukweli hapo ndipo nilianza kuwaza sitawaona tena Baba, Mom, na ndg zangu, tena nilianza kuwaza ninapotea kwenye uso wa dunia bila kutambliwa nimefia wapi. Uso wote ulijaa machozi, tumaini likapotea tukabebeshwa yale maroba ya vitu na wao walikuwa wamebeba mamizigo kibao waliopora kwenye magari, safari ya maisha nisiyoyafahamu ikaanza, nikakata tamaa, nikakosa tumaini, mwili ukazidi kuvibrate, miguu ikawa inagongana gongana kama mtoto aliyeugua utapiamlo,akili yangu itaitengeneza taswira ya mama angu machozi yakajaa machoni hata kushindwa kuona vema, moyoni mwangu nikahisi kutamka jina langu Mara tatu....Derick....Derick......Derick (Code) why was I born??!!

Itaendea...

Muendelezo soma
Sitasahau nilivyonusurika kuchukuliwa mateka na majambazi mkoani Kagera
Nourhan pita hapa kuna kipendacho roho
 
Hilo eneo mlipotekewa nalifahamu kwa uzuri kabisa (kwa sasa kuna mifugo ya JPM) nimeenda karagwe kabla ya lami kwahiyo siko mtoto hivyo ila umezidisha mbwembwe
Ukosahihi kabisa Ila jamaa vitunguu anazidisha kwenye mboga
 
Ilikoishia......
Ko....nko...nko...nko...nilikuwa nagonga mlango wa Ile nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la KKKT. Baba mmoja mwenye Kati ya umri wa miaka 45-50 ndiye aliyenifungulia mlango.

Inaendelea....

Ile anafungua tu, facial expression yake ilionekana kubadilika gafla baada ya kuona ( labda mtu asiyemdhaania amesimama mbele yake). Akiwa amesimama wima kati kati ya mlango wake, aliinua kinywa chake akatamka neno 'Karibu kijana' nikamjibu Asante, Kisha nikamsalimia.

Baada ya kuijibu ile salamu niliyompa akauvuta mguu wa kwanza kutoka mlangoni kuja nje kisha wa pili ukafuata wote tukawa tumesimama kwenye kibalaza. Akanikazia macho ili kutaka kujua shida gani imenifanya niwe hapo. Ikumbukwe kwamba nilikuwa mchafu, sijaoga yapata Siku tatu, mavazi yangu hayakuonesha mvuto kwakuwa yalikuwa machafu pia ukizingatia nilikuwa nanyeshewa nakauka nalala kwenye matope wakati ule nikiwa mwituni.

"Eeeh... unasemaje kijana wangu, nikusaidie nini?"

Nilianza kwa kujitambulisha,

Ninaitwa Derick, Mimi ni mwanafunzi wa shule X, hapa nilipo naelekea shule. Nimetokea Mwanza toka juzi, ila wakati tuko njiani kutoka Bkb kuja Karagwe, tulitekwa na majamba.....
kabla sijamalizia, alinikatisha story akadakia

Ooooh...kwenye utekaji wa juzi?.....na wewe ilikuwepo?! aliniuliza kwa mshangao huku akiwa na hamu ya kusikiliza ni nini kilitokea. Wakati huo huo akanikaribisha ndani sebuleni kwake nikachagua kwenda kukaa kwenye kochi moja lenye siti Kama nne hivi, huku yeye akiketi kwenye kochi lake mwenyewe.

Eeekh... ikawaje.....alitaka nimpe huo mkasa.Nilimwelezea kila kitu kilichohusiana na ule utekaji. Alisikitika sana yule Mchungaji akabaki kunipa pole nyingi. Kisha baada ya hapo alimwita kijana aliyekuwa anakaa naye pale nyumbani Kisha akampa maelekezo ya kunitengea maji ya kuoga kisha anioneshe chumba ambacho nitapumzikia.Wakati huo ilikuwa tayari saa 12:50 za jioni kwa mujibu wa saa iliyokuwa ukutani.

Baada ya kumalizia kuoga, nilifua ile t-shirt, Ila suruali sikuifua maana hali ya hewa haikuwa rafiki na ilishakuwa jioni, hivyo isingekauka mpaka kufikia siku iliyokuwa inafuata. Mchungaji alinipatia shati mbadala nikavaa, kisha nikakaribishwa chai ya mdarasini na vipande kadhaa vya mkate nikala nikashiba, nikajisikia sasa naanza kurudi kwenye maisha ya utu.

Baadaye Mchungaji aliniruhusu kwenda kwenye chumba nilichoandaliawa ili nijipumzishe.

Kitanda Cha wastani chenye godoro lenye ujazo mkubwa na mashuka meupee ndipo nilipojirusha na kujitawanya, mikono kule miguu kule kisha nikavuta pumzi na kuishusha kwa nguvu 'huuuu....ffvuuuuuu...' nikawa najisemea moyoni hatimaye kifo kimeniepuka!

Nikiwa nimejilaza chali kitandani, sikuwa nikiwaza tena masahibu yaliyonikuwa yamenipata kwa Siku mbili mfurulizo kule porini bali mawazo yangu yalianza kutakatishwa na taswira za wale mademu zangu warembo. Mama, Baba na all my siblings sikuwa nikiwakumbuka tena mawazo yote yalikuwa yametuama kwa sura nzuri za wale warembo wangu (wa shule). Nilihisi kuwamiss sana. Nilimkumbuka Jasmine na ahadi yangu kwake ya kumletea albam nzuuri ya kuhifadhia picha ambayo alikuwa amenituma.

Ufafanuzi.
Enzi zile hapakuwa na hii digital technology iliyopo sasa na wanafunzi wengi kipindi hicho kuwa na albam ya kuhifadhia photos ilikuwa lazima yaani laazima.

Aliniagiza nimletee nikitoka Mwanza, na Mimi sikuwa nimefanya hiyana nilikuwa nimemtafutia albam unique kabisa. Kitendo kile kilinifanya niyakumbuke mabegi yangu.

Kwa upande mwingine nilikuwa namfikiria Viviana pamoja na Shansy kila mmoja kwa namna yake. Niliwaza Vivy alivyoniambia wakati tunafunga shule kuwa wakati wa Kufungua nihakikisha sichelewi kureport kwakuwa angekuwa na surprise yangu siku hiyohiyo ya Kufungua shule. Aliniahidi kuwa nikichelewa kuja Kama ambavyo ilikuwa kawaida yangu siku za kufungua, nisingekuta kitu maana alinambia surprise yenyewe Inge expire in a single day. Wakati huo nilipigia mstari kuwa surprise nimeshaikosa kutokana na vizingiti nilivyokutana navyo.

Shansy.... niliwaza juu ya kudekadeka kwake na vidompo vyake mashavuni. Niliwaza umayaimayai wake hususani ninapokuwepo shule yaani alikuwa anajisikia more secured kutokana na kuwa nilikuwa prefect so nilikuwa namdefend Sana. Nilihitaji kuwaona, Pia nilifahamu fika kuwa nao kila mmoja kwa wakati wake walihitaji kuniona.

Kiujumla nilikuwa mwenye furaha sana, mawazo mengine yakanijia nikaanza kuwaza, Sasa.....nafikaje shule na hizi kauka nikuvae? Hata kama nimepoteza mabegi lakini hela si ninayo? Wazo likanijia why nisitumie hela ya ada ninunue nguo chache na mazaga mengine ya kutumia huko shule. Nikajisemea hilo wazo ni zuri maana jambo la kutekwa si dogo, mzee akisikia tu yawezekana hata akaja shule. Si ntamwambia nilipoteza everything?! Nikaona mpango huu ni mzuri nikapigia mstari.

Nikiwa kwenye mawazo yenye kunipa furaha, nilisikia mlango ukigongwa. Niliporuhusu kijana akaingia watati huo akinipa taarifa kuwa chakula kilikuwa tayari, akanikaribisha. Baada ya kufika mezani Mchungaji aliombea chakula Kisha akanikaribisha, akaniambia " Kijana pakua chakula"

Chakula kilikuwa kitamu, zilikuwa zimepikwa ndizi mixed na maharage vikiwa vimekamatana haswaa, Kisha pembeni kuna mchuzi wa samakl Sangara mkavu mixed na karanga. I real enjoyed dinner that day.Wakati tukiendelea kupata msosi Mchungaji aliniuliza...
" Derick we unaabudu dini gani"
nikamjibu RC (Roman Catholic)
"Aaah...vizuri je huwa unasali"
nikamjibu, ndiyo Mchungaji
"Vizuri hakikisha unafanya hivyo kila mara....."

Maongezi yalikuwa marefu hata baada ya kula tuliendelea kuongea. Kisha nikamkumbusha kuwa ningeondoka siku inayofuata kuelekea shule na hivyo nilihitaji kujua wapi nitapata usafiri. Ikumbukwe, lile kanisa haliko karibia na barabara bali liko kwa ndanindani hivyo aliniondoa hofu akaniambia nisiwe na wasiwasi kijana wake ataniescort mpaka ntakapopandia gari. Baada ya maongezi mengi pale sebuleni tuliagana kila mtu akaenda kulala. Muda huo saa ilisomeka saa nne za usiku.

Nilikuwa kitandani nimelala, nikashtuka nikawa nahisi baridi sana huku mwili ukinitetemeka pia. Shuka na blanketi nilivyokuwa nimejifunika vikawa havisaidii,nikawa nahisi homa.
Nilijikunja kwa kujikunyata ili kujiepusha na baridi bado ilikuwa havisaidii. Akili ikanijia kwa nini nisimgongee Mchungaji labda ana dawa zinazoweza kunituliza, nikaamka, nikafungua mlango kisha nikachungulia kwa kolido vyumba ni vinne changu ndo cha tano nikaanza kujiuliza nigonge kipi kati ya vile vinne.

Muda huo llikaja wazo, so vizuri kugongagonga milango ya watu usiku hivi na ukizingatia mimi ni stranger kwenye hii nyumba. nikaamua kuifuata sauti ya pili nikaona niache, nikarudi kitandani kulala. Jinsi wakati ulivyokuwa ukienda ndivyo hali ilizidi kuwa mbaya, nikaona hii Sasa hapana nikatelemka kitandani nikajikongoja mpaka mlangoni, nikafungua kisha nikatoka.

Nilikwenda kugonga mlango wa kwanza bahati nzuri ndicho kilikuwa chumba cha Mchungaji akanihitikia kisha akatoka nikamwelezea tatizo nililokuwa nalo. Alinituliza pale kisha akafungua mlango mmoja wapo wa vile vyumba akaingia, baada ya dk.3 akaja na vidonge mkononi akanikabidhi akanitaka nimeze, vingenipunguzia homa. Nikameza kisha nikarudi kulala.

Asubuhi kulipokucha nilikuwa pia nimeamka nikiwa sina ile hali iliyonipata usiku badale yake kichwa kilikuwa kinauma. Nilianza kujiandaa, nikacheki t-shirt yangu ilikuwa imekauka tayari sikuwa na begi wala nini niko mimi na kauka nikuvae zangu.Mchungaji alipoamka alinijulia khali kisha tukasalimiana na hapohapo nikamjuza kuwa Mimi nimeishakuwa tayari kwa safari.

Mchungaji alinitazama kwa kutabasamu kisha akaniambia mbona bado mapema sana maana magari hayapiti mapema muda huo. Alimwita Sam yule kijana wake akamuuliza Kama ameshaweka chai jikoni kijana akamjibu ndio inakaribia kuchemka. Mchungaji alikuwa anaishi yeye pamoja na huyo kijana Sam. Sikupenda kuuliza Kama alikuwa na familia au la (yalikuwa hayanihusu).

Baada ya kumalizia kunywa chai na kukumilisha kila kitu, ulikuwa ni muda wa kuagana na Mchungaji akanitakia baraka nyingi kisha akanipa kiasi cha pesa ambacho sikikumbuki, kisha akanipa kijana wake Sam anisindikize hadi kituo ambapo ningepandia gari. Katika pesa aliyonipa aliniambia niya matibabu nikafanye (health check-up), Pia na nauli ya kunifikisha shule. Alinielekeza kuwa nikipanda gari nishuke mji wa Murushaka kisha pale maeneo ya karibu Kuna Hospitali ya Wilaya kwa wakati huo sijui sasa, inaitwa Nyakahanga Hospital.

Nilimshukuru sana Mchungaji, kisha tukaanza kuondoka na kijana wake kuelekea stand ilikuwa mida ya saa nne asubuhi.

NIWARUDISHE NYUMA KIDOGO

Niwakumbushe kwamba, Siku ile napanda mti ule mrefu ambao kesho yake nilijikuta nimelala chini baada ya kukumbana na kadhia ya wachawi, nilikuwa sina viatu miguuni.

Kumbukeni nilivivua baada ya miguu kuwaka moto. Sasa tokea siku Ile sikuwa na viatu tena maana wakati nakwea ule mti nilipanda navyo nikiwa nimevining'iniza begani lakini baada ya kujikuta chini siku iliyofuata sikuwa navyo. So binafsi sikuangaika kuvitafuta maana nilishaishiwa nguvu kwa ile njaa. Kwa hiyo tembea zangu zote baada ya hapo nilikuwa na soksi ambazo nazo zilikuwa zimeanza kuchanika kwa kuchakaa.
Nilipofika pale kijijini kwenye kile kicenter nikiwa na yule jamaa mfugaji aliyenileta pale, baada ya kuagana naye niliingia kwenye kiduka nikanunua viatu aina ya CHACHACHA ndivyo nilivyofika navyo pale kwa Mchungaji Kanisani.

SASA TUENDELEE....

Tulipofika pale pa kusubiria, hatukukaa sana nikapata gari ilikuwa ni ya binafsi tena nilipewa lift. Nilianza safari tukapiga mwendo mpaka Kayanga mjini kisha tukaendelea mpaka mji uliokuwa mbele unaoitwa Murushaka na kwa bahati sana walinishusha hospital kabisa kisha wao wakaendelea mbele na safari yao.

Pale Hospitali nilifanyiwa vipimo, kisha nikaenda kwa daktari akaniuliza maswali kadhaa huku akiandika kisha akanipa kadi na kunielekeza sehemu ya dawa. Nurse kwenye dirisha la dawa akaniambia chukua hii kadi nenda kwenye chumba cha sindano kisha ndio urudi.

Nilichomwa sindano kisha nikaambiwa bado mbili ambazo nilitakiwa kuchomwa kila siku saa nane mchana. Cha ajibu sijui nilikuwa na ujinga gani maana hata sikuuliza nilikuwa nasumbuliwa na nini

Baada ya kupata huduma kimatibabu
nirudi pale Center Murushaka kisha nikatafuta lodge kwa ajili ya kukaa pale nimalize zile sindano Kisha ndiyo niende shule.

Nikabahatika kupata nafasi palepale Center kwa lodge za bwana mmoja jina lake silikumbuki alikuwa maarufu sana kipindi hicho, lodge zake zilikuwa kando kabisa na barabara kuu.

Baada ya kujiseti vizuri kwa room, niliamua kutoka ili nipite pite kwenye maduka na sokoni ili niangalie vitu vya kununua. Kitu Cha kwanza nilihitaji nianze na viatu kisha ninunue saa ya mkononi. Nilishakubaliana na mawazo yangu ya kutumia ada kununulia ninachohitaji.

Muda mfupi niliingia sehemu iliyokuwa na soko ambalo kila kitu kilikuwa kinauzwa humo. Nilinunua saa Kisha nikaenda madukani kucheki kiatu. Maduka mengi pale mjini yalikuwa yanauza readymade na Mimi nilikuwa sifagilii sana. Niliuliza wenyeji wakanielekeza bidhaa za mtumba zilipo hapo ndipo nilipata kununua viatu nikavaa kisha chachacha nikaziacha palepale. Nilichukua begi jipya Kisha nikanunua mambo yote muhimu ya kwenda nayo shule. Kibegi kikajaa ndi.

Muda mfupi nilikuwa reception pale lodge nikapewa funguo kisha nikaenda kwenye room nikaweka begi langu mahala pale kisha nikajirusha kitandani kupumzika maana nilikuwa nimechoka.

Jioni ilikuwa imefika, nikaamka kitandani nikaamua kujimwagia maji ili nipate nguvu mpya kisha nikachukua dawa zangu nikazimeza nikatulia kidogo Kama dk.10 nikatoka nje.

Ile natoka nje tu nikawaona wasichana wawili maji ya kunde wanapita wakiwa wamepiga pigo za kupendeza nikawa najisemea duh! kumbe mji huu una vifaa. nikatoka pale ikabidi ninyooshe miguu kidogo niusome mji ulivyo.
Nilitembea mpaka sehemu moja kuna kanisa panaitwa Bugene Parish, nikaona barabara bado inazidi kuendelea ila ikabidi niishie pale. Njiani nilikuwa nakutana na videmu vikalivikali, sikushangaa sana maana mimi mwenyewe nimesoma ukanda huo so nilikuwa nawaona shule lakini nikabaki kujisemea hii Karagwe hii Ina mademu wakali sana.

Ilikuwa ni saa mbili usiku wakati namkabidhi yule receptionist funguo za chumba na nikamuaga naenda kucheck msosi. Nilianza kucheck huku na huko kuangalia wapi ningeona sehemu wanauza chakula, nilipaona kisha nikaingia, sikumbuki niliagiza chakula gani Ila nilikaa sana pale kwasababa sikuona haja ya kurudi kule lodge mapema.

Ilipofika saa nne, wakawa wanahitaji kufunga na Mimi ndipo nilianza kupunguza hatua kudokidogo kurudi lodge kulala. Watu walikuwa wamempungu kabisa kwenye mtaa niliyokuwa nakatiza , ni mtaa uliokuwa nyumanyuma ambapo pia maeneo hayo yalikuwepo makazi ya watu.

Nikiwa sina hili wala lile nikashangaa kuona vijana wanakimbia huku na kule.Nikapigwaa na butwaa, na Mimi nikaamua kula unyoya hata ile direction niliyokuwa naelekea nikawa tayari nimeipoteza kwa hiyo ukawa ni mkurupushano mimi akili yangu nilishajua majambazi, kwasababu tayari ndicho kitu kilikuwa kichwani takribani siku nne zilizopita.

Kiherehere changu nikaanza kupiga kelele ....majambaziiii...majambaziiiiiii huku nikikimbia bila malengo. I see nilikutana na mtama mmoja ambao sitausahau maishani. Sijakaa sawa nikashtukia nimeshanyanyuliwa Tanganyika jeki kuangalia vuma kumbe ni mapolisi. Cha kushangaza nilijikuta na faraja tena niko happy maana nilijua nimsharudi mikononi mwa mabandidu.

Ilibidi niwe mpole na wakati huo walishaturundika rundo la vijana pale. Kumbe ilikuwa operation kamatakamata ya vibaka pale Murushaka town. Tulipakiwa kwenye difenda mpaka kidogo cha polisi karibu na eneo hilo tukaachwa pale na polisi kadhaa kisha wakarudi kubeba wengine.

Baada ya kuwa watuhumiwa wote tuko pale tayari, ilitumwa difenda nyingine ambayo ilitoka kituo kikuu yaani makao makuu kuja kutubeba maana pale tulipokuwa ni kituo kidogo cha polisi wakati huo sijui sasa. Hivyo hakikuwa na lockup.

Zilikuwa ni difenda mbili, zikiingia katika viunga vya polisi pale makao makuu na Mimi nilikuwa kwenye moja ya madifenda hayo Kama mtuhumiwa.
Tulishushwa huku tukipangishwa line Kisha tukaambiwa tuchuchumae palepale tulipokuwa. Baada ya hapo taratibu za kutusweka lockup zilifanyika tukatiwa ndani. Wakati naangalia saa yangu muda ule naivua kuikabidhi ilikuwa inasona saa 00:12 usiku. Na hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuswekwa ndani.

Nikiwa mle lockup nilianza kuwasikia vijana wakilaumiana wenyewe kwa wenyewe kwa kilugha....


" .....cha Lenard nicho chabaletayo......"

anayelahumiwa akaanza anajitetea sasa

".......iweee towakukangaaaa........ "

Sasa nyie wajuvi wa lugha njooni mtafsirie wasomaji!!!

Basi Mimi sikutaka hata kuwajali kuwasikiliza, maana na mimi nilikuwa nawaza yangu. Nilianza kufikiri, ....hivi ni nini hiki mbona naona kama nimekaa kaa kimikosi mikosi......eeeeh nini hiki i see ,nikawa najiuliza bila majibu. Yaani kutoka kuwa msafiri hadi mateka, sasa kutoka mateka hadi mtuhumiwa??! nilijiuliza.

Kupitia vidirisha vya juu pale lockup ndiyo niligundua kumekucha maana mwanga ulikuwa unaonekana. Mazingira ya mle ndani wakati huo hayakuwa rafiki Ila sijui sasa, hivyo nilibaki nimekaa pale pale bila kutoka mpaka ilipofika muda wa kunichukua maelezo ikiwa ni muda wa saa 11:10 asubuhi.

Afande alianza kunichukua maelezo;

"..,...Jina lako ...... Derick (sio halis)
......Kabila.......... Muwemuwe (sio halisi)
......kazi...........Mwanafunzi
........nini??! yaani Mwanafunzi ndiyo umeshaanza kujiingiza kwenye makundi ya kihalifu......pumbavu kabisa"
akaacha kuandika kabisa akaniangalia, Kisha akasema. ..

"Alafu mbona hufananii kabisa" akamwita afande mwenzie....
"Afwande Rafa (code) eti angalia huyu dogo ni Mwanafunzi anafanya uharifu"

"Achana nalo lihifadhiwe na serekare hayo ndiyo baadaye yanateka watu afande"

wakati wote huo Mimi nilikuwa kimya nawasikiliza baada ya kunipiga mabango meeengi afande akashika kalamu tena ili aanze kuandika na kabla hajaanza nikamwambia

"Afande Mimi ni mmoja wa waliotekwa kule uzuri wa kondoo na si kutekwa tu bali kuchukuliwa na manajambazi kabisa. Na hapa ninapokwambia Kati ya watu watano tulioondoka na wale majambazi Mimi peke angu ndio nilisalia wengine walioondika nao"

Pale pale baada ya kutoa ile taarifa hata ma afande wengine waliokuwa karibu wakasogea karibu kusikiliza. Baada ya muda mfupi wakanirudishia vifaa vyangu Kisha nikapelekwa kwenye ofisi ya mmoja wa wakuu wao nikapewa na kikombe cha kahawa kabisa. Kiukweli nilieleza mambo mengi, nilitoa ushirikiano wa kutosha kabisa na mwishowe nikaeleweshwa kwa ufasaha umuhimu wa kureport polisi pale uharifu unapotokea ili haki zangu ziweze kulindwa kisheria.

Baada ya maongezi yetu pamoja na kipongezwa niliulizwa nimefikia wapi nikamwambia afande niko Lodge pale Murusha, nikamfahamisha kuwa nimeandikiwa sindano pale Nyakahanga hospital kwa hiyo muda si mrefu nahitajika nikachome na ntakuwa nimebakiza moja ili nimalize siku iliyokuwa inafuata.

Kwakuwa muda wa sindano ulikuwa unakaribia nilipata lift ya gari yao iliyokuwa inaelekea Murushaka hivyo wakaambiwa mfikisheni huyu kijana pale hospital. Na pia afande aliniambia Kuna Askari anayefanya kazi kituo Cha karibu na nilipokuwa nimefikia aje anichukue nikakae kwake na pale lodge nitoke mpaka nitakapokuwa nimekamilisha utaratibu wa matibabu tayari kwa kurudi shule. Na alinieleza nitaombewa lift na yule Askari atakaye aliombwa kunipa hifadhi.

Ilikuwa ni alfajiri ya tarehe na siku nisiyoikumbuka, ni siku ambayo nilikuwa narudi shule. Ilikuwa ni siku tulivu iliyokuwa na manyunyu kidogokidogo ambayo hata hivyo yalikuwa yanakata kutokana na jinsi kulivyokuwa kunazidi kupambazuka. Tulijiandaa, Kisha baada ya hapo tuliongozana na afande hadi stand ili anisaidie kuniombea lift kwa gari lolote ambalo lingekuwa linaeleke mwelekeo mmoja na ninakoenda.

Hatukukaa muda mrefu likatokeza Land cruiser la UN, afande alilisimamisha na bahati nzuri likasimama tulishangaa kidogo maana mara nyingi madereva wa UN walikuwa hawaruhusiwi kupakia watu hovyo. Baada ya kusimama ndio tukagundua kumbe alikuwemo bosi ndani ya gari. Afande Said aliniombea lift Kisha nikakubaliwa. Tuliagana Kisha safari ikaanza.

Magari ya UN yalikuwa yanatembea balaa, ilitutumia masaa kadhaa nikawa niko kwenye viunga vya shule.
Amini husiamini ile gari ilikwenda kusimama moja kwa moja Admin block na muda huo nilishuka , nikamshukuru sana yule boss kwa ule msaada wa kunifikisha shule.

Nikiwa nimemaliza kutoa maelezo ya kwanini nimechelewa pale ofisi kwa Second Master, akinipa pole na alilidhia na kunipokea hapakuwapo na kizuizi nilianza kuelekea bwenini. Ile tu natoka Ofisini ni dakika chache tu kengele ya wanafunzi kuwa break kwa ajili ya kupata uji ilikuwa imegongwa na timu yangu ilikuwa imeshaniona na kunikimbilia kunipokea. Wakati huo nilikuwa naangalia huku na huko nikijaribu kucheck Kama nitawaspot Jasmine, Vivy na Shansy Ila sikuwaona kabisa madent walikuwa wametawanyika tawanyika, ingawa baadaye kila mmoja kwa wakati wake wakati naongea nao walinidokeza kuniona vizuuuri kabisa bila chenga wakati nikiingia.

Kisa cha hawa wadada ni kirefu sana,Nilipata chungu na tamu ya hawa mabinti ambao leo ni wake za watu na heshima zao. Jasmine anafanya kazi na kuishi Arusha ana watoto watatu, Vivy anafanya kazi na kuishi Z'bar ana watoto wa Tatu pia na Shansy Mnyarwanda huyu anaishi Belgium yuko na watoto wawili ameolewa huko.

TAMATI

STORY YANGU KUBWA ILIHUSU MASAIBU NILIYOYAPITIA BAABA YA KUNUSURIKA KUCHUKULIWA MATEKA IMEISHIA HAPO.

ASANTENI WOTE MLIOIFUATILIA NA NISAMEHENI PALE NILIPOWAUDHI.
Nikupe kongole ndugu yangu kwa kupata wasaa kushare kidogo na sisi maswaibu yaliyokupitia .......ni msoto ulipitia lakini ni funzo kubwa umetuapatia ambao unatujenga na kutuongezea ukakamavu na ujasiri tukimtanguliza Mungu Mbele

Ulipotukwaza hatuna budi kukusamehe maana na sisi hatuna cha kukulipa zaidi ya ASANT kwa kushare
 
Back
Top Bottom