Sitasahau tanuru la moto nililopitishwa na Hayati Magufuli mimi kama mtumishi wa Serikali

Fukua

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2022
Posts
546
Reaction score
479
Habari,

Niende kwenye mada, kama kichwa cha habari hapo juu, Ninaweza kusema kwamba waliotunga sheria mbalimbali za utumishi wa umma watakuwa wajinga na walikuwa na njia njema kabisa.

Miongoni mwa Vitu muhimu kabisa ni nyongeza ya mishahara, increments na kupanda madaraja kila baada ya miaka kadhaa ili kuendana na kupanda kwa gharama za maisha kila mwaka. HIVYO mtumishi aliweza kuyamudu maisha yake japo kwa kudanadana.

Utawala wa JPM yeye hakuona umuhimu wa jambo hili na kuwasugua watumishi kwa miaka sita bila kuwapatia hiyo haki yao ya msingi, aliwafanya watumishi wengi kushindwa kuendana na gharama za maisha na kuwa na hali mbaya sana kiuchumi.

Hivyo kitendo hiki kilififisha ufikiwaji na upelekaji wa maendeleo kiurahisi kwa wananchi japo wananchi wajinga walikuwa wa kwanza kupiga makofi wakifurahia hayo Mateso ya watumishi wa serikali yao.

Watumishi walifanya kazi quantity na si quality kama maroboti, ufanisi ulishuka sana na nidhamu ya uoga kuwa asilimia 100, nia na hamu ya kufanya kazi za serikali ilipungua kabisa na hata maendeleo yaliyoyowafikia wananchi yalikuwa hafifu japo yalikuwa jina kubwa sana na wale waimba mapambio kama mtakumbuka.

Watumishi wa serikali ni DARAJA la kupitisha maendeleo kutoka kwa serikali kwenda kwa wananchi wakiwa na hali mbaya kiuchumi, kiafya na kijamii basi hata maendeleo tarajiwa yatawafikia wananchi kwa namna hali yao ilivyo na wakiheshimiwa, kupewa stahiki zao kwa wakati basi hata utoaji wa huduma na maendeleo kwa jamii huongezeka maradufu.

Binafsi ninamuona MAMA samia kufanikisha zaidi katika mambo yake hata kwa kulijali hili kundi muhimu katika jamii, na 23% imewaongezea watumishi nguvu sana kabla hata ya kuipata, tunakuomba MAMA samia watumishi utushike mkono na sisi hatutakuangusha kuyatafsiri mawazo yako ya kimaendeleo kuwa uhalisia kwa wananchi wetu tunaowahudumia.

Mungu ibaraki Tanzania, Mungu ibaraki ccm na raisi wetu MAMA SAMIA
 
Sasa hivi umeongezewa kamshahara kwa 23% alafu gharam za maisha zimepanda kwa 60% na umewekewa na matozo juu kisha unashangilia! Huo ni utahira.
Lakini angalau haki yangu nimeiona nitaendelea na mengine sio kunipa haki yangu ili kitu likajenge uwanja wa ndege usio na manufaa
 
Habari,

Niende kwenye mada, kama kichwa cha habari hapo juu, Ninaweza kusema kwamba waliotunga sheria mbalimbali za utumishi wa umma watakuwa wajinga na walikuwa na njia njema kabisa.

Miongoni mwa Vitu muhimu kabisa ni nyongeza ya mishahara, increments na kupanda madaraja kila baada ya miaka kadhaa ili kuendana na kupenda kwa gharama za maisha kila mwaka.HIVYO mtumishi aliweza kuyamudu maisha yake japo kwa kudanadana.

Utawala wa JPM yeye hakuona umuhimu wa jambo hili na kuwasugua watumishi kwa miaka sita bila kuwapatia hiyo haki yao ya msingi, aliwafanya watumishi wengi kushindwa kuendana na gharama za maisha na kuwa na hali mbaya sana kiuchumi.

Hivyo kitendo hichi kilififisha ufikiwaji na upelekaji wa maendeleo kiurahisi kwa wananchi japo wananchi wajinga walikuwa wa kwanza kupiga makofi wakifurahia hayo Mateso ya watumishi wa serikali yao.

Watumishi walifanya kazi quantity na si quality kama maroboti, ufanisi ulishuka sana na nidhamu ya uoga kuwa asilimia 100, nia na hamu ya kufanya kazi za serikali ilipungua kabisa na hata maendeleo yaliyoyowafikia wananchi yalikuwa hafifu japo yalikuwa jina kubwa sana na wale waimba mapambio kama mtakumbuka.

Watumishi wa serikali ni DARAJA la kupitisha maendeleo kutoka kwa serikali kwenda kwa wananchi wakiwa na hali mbaya kiuchumi, kiafya na kijamii basi hata maendeleo tarajiwa yatawafikia wananchi kwa namna hali yao ilivyo na wakiheshimiwa, kupewa stahiki zao kwa wakati basi hata utoaji wa huduma na maendeleo kwa jamii huongezeka maradufu.

Binafsi ninamuona MAMA samia kufanikisha zaidi katika mambo yake hata kwa kulijali hili kundi muhimu katika jamii, na 23% imewaongezea watumishi nguvu sana kabla hata ya kuipata, tunakuomba MAMA samia watumishi utushike mkono na sisi hatutakuangusha kuyatafsiri mawazo yako ya kimaendeleo kuwa uhalisia kwa wananchi wetu tunaowahudumia.

Mungu ibaraki Tanzania, Mungu ibaraki ccm na raisi wetu MAMA SAMIA
Kiufupi kama ulikuwa kwenye Kazi ambazo hazina marupurupu na posho lazima uwe uliuona moto maana Mwendazake hapana aisee..

Mwendazake alikuwa anajua kutumia pesa ila kutafuta au kuweka mazingira ya kuzalisha pesa ndio mtihani.
 
Sasa hivi umeongezewa kamshahara kwa 23% alafu gharam za maisha zimepanda kwa 60% na umewekewa na matozo juu kisha unashangilia! Huo ni utahira.
Huoni kwamba wewe ndio taahira maana unaongea upumbavu ambao ubongo wako unakutuma..

Unaweza kuthibitisha jinsi gharama za maisha zimeongezeka kwa 60%?

Mbona Bei za umeme ziko pale pale, kodi za nyumba ziko pale pale na vyakula Bei zake zina ongezeko dogo..
 
Lakini angalau haki yangu nimeiona nitaendelea na mengine sio kunipa haki yangu ili kitu likajenge uwanja wa ndege usio na manufaa
Ungesema tu ule uwanja ulikuuma haya mengine yote ni ngojera.
ww unalalamika kutokupandishwa mshahara, kuna watu private sector walipunguziwa mishahara 25-40% for 1yr during covid na wengine walipoteza kazi kabisa ww unalia lia kutoongezewa salary while uliendelea kupata mshahara na you kept your job during covid.
Kweli shukrani ya punda ni mateke.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, mama anastahili pongezi kubwa kwa hili la kujali maslahi ya watumishi, tangu mwaka jana watu wanapata madaraja na mwaka huu nyongeza ya 23%, kama ikija kampeni ya mitano tena kwa mama naamini watumishi watakuwa wa kwanza kuunga mkono.
 
Sasa hivi umeongezewa kamshahara kwa 23% alafu gharam za maisha zimepanda kwa 60% na umewekewa na matozo juu kisha unashangilia! Huo ni utahira.
Maendeleo hayaji kwa njia rahisi rahisi tu fikiria kama wewe utaamua kujenga nyumba au kununua gari nzuri ujue lazima famili yako bajeti itaenda kwenye matumizi ya msingi tu, pombe utapunguza kunywa. Nyama za kuku na bata zitapungua. Mavazi utapunguza kununua nk nk
 
Back
Top Bottom