Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni nyinyi kada ya ualimu tu ndio mnaolalamika mishaara na upuuzi mwingine mara sijui hatujapewa t shirt,tumepewa ubwabwa kidogo bila majiKutokutosha kwa mshahara ndio kigezo cha kuwanyima haki zao?
Sawa lakini hao ndio wanaoongoza kulalamikaMimi sio mwalimu mkuu
Soma vizuri dogo!! ukinifuatlia kwa kurupuka hivi huta nielewa kamwe nakwambia!! mie sikutokana na mungu wako unasikia?? ila nakushauri unisome kwa utulivu sana na kwa uelewa!We ni nani ?hahhaha ila we unachekesha kwaiyo kinda umeumbwa kwa mfanonwa mungu basi we mungu?
Unapinga kwa hoja dhaifu sanaUna uwezo mdogo wa kufikiri. Hebu rudi kwenye aya ya kwanza uangalie ulichoandika.
Alafu umepitiaje tanuru la moto wakati Mchele uliunzwa 1, 400
Unga 1, 000/=
Mafuta lita 5,000/=
Sabuni mche 2,000/=
Nk
Watumishi wengi wa umma hasa walimu wana uwezo mdogo wa kuchambua na kupambanua mambo
Mwenye magufuli alikuwa mwizi kama wezi wengine wa kodi yetu. Hakuwa na tofauti na wezi wengine tofauti ilikuwa ni mwizi aliyejipa kinga!Kiufupi kama ulikuwa kwenye Kazi ambazo hazina marupurupu na posho lazima uwe uliuona moto maana Mwendazake hapana aisee..
Mwendazake alikuwa anajua kutumia pesa ila kutafuta au kuweka mazingira ya kuzalisha pesa ndio mtihani.
Naona unachukulia maendeleo ya nchi yanatokana na mishahara minono ya watumishi! UJINGA NI MZIGO, fikra mgando ni janga !Watumishi wa serikali ni DARAJA la kupitisha maendeleo kutoka kwa serikali kwenda kwa wananchi wakiwa na hali mbaya kiuchumi, kiafya na kijamii basi hata maendeleo tarajiwa yatawafikia wananchi kwa namna hali yao ilivyo na wakiheshimiwa, kupewa stahiki zao kwa wakati basi hata utoaji wa huduma na maendeleo kwa jamii huongezeka maradufu.
Alitumbuliwa na nani?
Sekta binafsi hii nchi imesahaulika sana tena watumishi wa umma mna wigo mpana sana wa kutoboa sijui mnafeli wapiHabari,
Niende kwenye mada, kama kichwa cha habari hapo juu, Ninaweza kusema kwamba waliotunga sheria mbalimbali za utumishi wa umma watakuwa wajinga na walikuwa na njia njema kabisa.
Miongoni mwa Vitu muhimu kabisa ni nyongeza ya mishahara, increments na kupanda madaraja kila baada ya miaka kadhaa ili kuendana na kupanda kwa gharama za maisha kila mwaka. HIVYO mtumishi aliweza kuyamudu maisha yake japo kwa kudanadana.
Utawala wa JPM yeye hakuona umuhimu wa jambo hili na kuwasugua watumishi kwa miaka sita bila kuwapatia hiyo haki yao ya msingi, aliwafanya watumishi wengi kushindwa kuendana na gharama za maisha na kuwa na hali mbaya sana kiuchumi.
Hivyo kitendo hiki kilififisha ufikiwaji na upelekaji wa maendeleo kiurahisi kwa wananchi japo wananchi wajinga walikuwa wa kwanza kupiga makofi wakifurahia hayo Mateso ya watumishi wa serikali yao.
Watumishi walifanya kazi quantity na si quality kama maroboti, ufanisi ulishuka sana na nidhamu ya uoga kuwa asilimia 100, nia na hamu ya kufanya kazi za serikali ilipungua kabisa na hata maendeleo yaliyoyowafikia wananchi yalikuwa hafifu japo yalikuwa jina kubwa sana na wale waimba mapambio kama mtakumbuka.
Watumishi wa serikali ni DARAJA la kupitisha maendeleo kutoka kwa serikali kwenda kwa wananchi wakiwa na hali mbaya kiuchumi, kiafya na kijamii basi hata maendeleo tarajiwa yatawafikia wananchi kwa namna hali yao ilivyo na wakiheshimiwa, kupewa stahiki zao kwa wakati basi hata utoaji wa huduma na maendeleo kwa jamii huongezeka maradufu.
Binafsi ninamuona MAMA samia kufanikisha zaidi katika mambo yake hata kwa kulijali hili kundi muhimu katika jamii, na 23% imewaongezea watumishi nguvu sana kabla hata ya kuipata, tunakuomba MAMA samia watumishi utushike mkono na sisi hatutakuangusha kuyatafsiri mawazo yako ya kimaendeleo kuwa uhalisia kwa wananchi wetu tunaowahudumia.
Mungu ibaraki Tanzania, Mungu ibaraki ccm na raisi wetu MAMA SAMIA