Msio na akili mnapongezana kwa kuambiana mna akili. Kweli Rage hakukosea kuwaita mbumbumbu.
Kati ya Simba na Yanga yupi unayedhani anaenda kuibadili hii ligi kutokana na tukio hili? Hili vumbi likishaisha mambo manne yatatokea:
- Haitawezekana tena timu kutumia milango isiyo rasmi. Adhabu yake hamtaweza tena kuihimili.
- Mabausa wasiotambulika hawataruhusiwa kulinda viwanja kabla ya mechi.
- Timu zitaruhusiwa kufanya mazoezi viwanjani kwa jinsi kanuni inavyoruhusu. Adhabu ya kuizuia timu kufanya mazoezi itakuwa kali sana.
- Viashiria vyote vya ushirikina vinaenda kuwa na adhabu kali ambayo sidhani kama mtaweza kuzihimili.
Sasa hapo niambie, kati ya Simba na Yanga, nani ambaye atakuwa amesaidia kuibadili na kuiboresha ligi ya Tanzania?