Sitashaangaa FIFA au CAS wakaamua kufanya uchunguzi wa kuahirishwa kwa mechi ya Simba na Yanga kabla ya kutoa uamuzi

Sitashaangaa FIFA au CAS wakaamua kufanya uchunguzi wa kuahirishwa kwa mechi ya Simba na Yanga kabla ya kutoa uamuzi

Kuna mambo ya msingi unayasahau.

Katika muktadha wa kisheria, haki si jambo la kutekelezwa kiholela bali linahitaji kufuata taratibu maalumu ili kuhakikisha linatendeka kwa usawa na haki.

Hii ina maana kwamba, hata kama sheria inakupa haki fulani, utekelezaji wake unapaswa kufuata utaratibu wa busara unaoeleweka katika mazingira husika.

Katika mfumo wa haki kuna misingi ya mawasiliano na ushirikiano wa pande zote zinazohusika. Sheria inatambua utaratibu wa mawasiliano na unaheshimiwa.

Kwa mfano, kanuni inamtaka Yanga amwandalie Simba kabla ya mechi ili aiangalie pitch na sababu nyenginezo zinavyoeleza.

Simba kuja bila taarifa hapo uwanjani kisheria hoja yake inabaki kuwa ni dhaifu na ni kwa sababu sheria inatambua utaratibu wa mawasiliano na unaheshimiwa. Yaani, Simba alifanya jitihada yoyote ya mawasiliano ili hilo litimizwe?

Ikiwa kama Simba haikufanya hivyo na ikadai yeye amefuata kanuni kama inavyoelekeza bado sheria itamtupa mkono kwa sababu, haki haiwezi kutekelezwa nje ya utaratibu.

Yaani, sheria imempa Simba haki fulani, lakini sheria inataka utekelezaji wake unapaswa kufuata utaratibu wa busara unaoeleweka katika mazingira husika. Kwa nini? Kwa sababu, katika muktadha wa kisheria, haki si jambo la kutekelezwa kiholela bali linahitaji kufuata taratibu maalumu ili kuhakikisha linatendeka kwa usawa na haki.

Kwa nini kwa usawa na haki? Sheria haitumiki kwa namna ya kulazimisha upande mmoja kushindwa kwa sababu ya makosa ambayo ungeweza kuepuka. Huwezi ukaja ghafla tu ukiwa hujatoa taarifa, kisha ukadai kuwa umenyimwa haki yako. Sheria pia hutegemea na nia njema na busara pia.

Ukija kwenye hoja ya kughairisha mechi, kwa kuwa Simba ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa tamko, Je, kuna kifungu chochote ambacho kinalinda dai lake awali na kufanya kuighairishwa kwa mechi? Jawabu ni hakuna!

Pengine inaweza kutoka hoja nyengine kuwa Simba si aliyeghairisha mechi, bali ni bodi ya ligi.

Ikiwa hali ni ya namna hii na yakifanyika marejeo ya asili ya madai ya Simba na kwa kuwa hakuna madai ya msingi kisheria kwa Simba kususia mechi kuna mambo yataibuka nayo ni bodi ya ligi au mamlaka ya mpira inamlinda badala ya kuchukua hatua stahiki.

Mazingira haya yanaweza kisheria kuitwa willful blindness yaani kufumbia macho ukiukwaji wa kisheria.

Katika muktadha wa mpira wa miguu hali hii inaweza kuangukia kwenye makosa yafuatayo:

1) Upendeleo wa wazi (Bias/Favoritism)
Yaani bodi ya ligi inamlinda mhusika badala ya kuhakikisha sheria na kanuni zinaheshimiwa (zinafuatwa bila upendeleo).

2)Rushwa au mgongano wa maslahi (Corruption/Conflict of interest)
Yaani, bodi ya ligi inamlinda mhusika kwa sababu ya maslahi fulani binafsi au kuwa na ukosefu wa dosari za kimaadili (rushwa)

Na sababu nyenginezo zinaweza kuwekwa na wengineo!

Mimi ni shabiki wa Simba, lakini hili suala ukiliangalia kisheria na hata kimuktadha wa sheria za mpira wa miguu madai ya Simba ni dhaifu. Ikiwa kama Yanga wakilivalia kidete na kulipeleka mamlaka za juu kabisa za mpira Simba lazima rungu lishuke kwake!

Si Simba tu, bali bodi ya ligi nayo pia. Ikiwa TFF ikashindwa kusimamia ipasavyo na kisha Yanga ikaamua kulipeleka ngazi za juu kama Uzi zitende haki hilo rungu litaathiri mpaka ligi yetu, mfano halisi ligi ya Italia rungu walilopigwa, kwa sababu Simba itaashibiwa na TFF itaadhibiwa pia na ligi yetu itakuwa mashakani.

Ni busara za Yanga pekee ndiyo zitakazoinusu ligi yetu.
Ndugu umeandika matakataka mengi yasiyo na msingi!siku ya tarehe 7 mchana wote walikuwa katika kikao cha pamoja na makubaliano nikwenda uwanjani! Kama ni hivyo kwa nini Yanga iliweka mabaunsa wakati katika kikao cha tarehe 7 ilijua dhahiri kuwa Simba jioni yake itakuwa na mazoezi uwanjani Nijibu
 
Uhu ujinga mnautoawapi wakati niwatu tunawaheshimu nyuma ya keybord??Simba aliandika barua kwa umma na akaandika bodi ya ligi akihainisha kinachofanya asiende uwanjani siku inayofuata sasa wewe hao uliowataja wanafuata nini wakati mwenye mamlaka na Mpira kaahirisha mchezo wewe uyanga wako unakuja na hoja chai!
Nyie na Bodi ya Ligi lenu moja.
 
Nyie na Bodi ya Ligi lenu moja.
Sema Simba wamepiga ya kidevu! kuliko ilivyotarajiwa!Bodi ya ligi ingekaa kimya 3point na mabao 3 yalikuwa ya Yanga!...Hila yanga niwaulize ile barua ya Bodi ya Ligi hawakuiona au walijua ni mambo ya mitandao??Maana walienda huko hakuna refa wala kamisaa au afisa ulinzi na sijui ni nani aliwapa kibali cha kuingia ndani ilibidi muishie getini!! 😀
 
Back
Top Bottom