Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,828
- 165,667
Kwa mtazamo wangu,katika taasisi ambazo zimeundwa kwa sheria nzuri na bora, basi ni EWURA, na si ajabu hakuna taasisi nyingine yenye sheria nzuri kama EWURA kwa maana ya kuwa taasisi ya Serikali lakini ni vigumu kuiingilia na zaidi ni vigumu kwa watawala kuweka mtu wao kama Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo na hiki ndio kinaweza kuwa kikwazo kikubwa.
Wakubwa wakiiona ni vigumu kuweka mtu wao- kama wana nia hiyo-wanachoweza kufanya ni kubadili sheria au hata kuivunja kabisa hiyo taasisi na hiki ndio natabiri kinaweza kuja kutokea katika siku za usoni.
Nasema hivi kwasababu, baadhi ya maamuzi ya EWURA ambayo ni ya kitaalamu, huonekana kugusa wananchi kwa maana ya kuwaumiza jambo ambalo wanasiasa hawalipendi hata kama kuna sababu au mazingira yaliyopelekea maamuzi hayo mfano kupandisha bei ya umeme au bei ya maji kwani EWURA hulazimika pia kumlinda Mora huduma na si kufurahisha wananchi (kumlinda mtumiaji pekee).
Tuliwahi kuona mwaka 2017 kama sio 2018, aliekuwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA aliondolewa ila hatukuona mtu kutoka nje ya EWURA (UDSM, n.k) kateuliwa kukaimu bali aliekaimu alitoka humo humo ndani ya EWURA fofauti kabisa kama ilivyokuwa kwa TANESCO na taaaisi zingine ambazo walioteuliwa kushifa nafasi za mashirika au taasisi hizo walitoka nje kabisa ya taasisi zenyewe.
Kwahiyo, kulingana na mtazamo wangu, wakubwa wakiona sheria ni kikwazo, basi watakuwa na option mbili: (1)kubadili sheria (2) kuivunja taasisi husika.
Kwa maneno mengine, naitazama EWURA kama CAG aliepita.
Time will tell.