zawadi kutoka wapi mkuu.....Huwa nawaambiaga watu kuwa Nyerere alikuwa zawadi kwa watanzania.
Huwa nawaambiaga watu kuwa Nyerere alikuwa zawadi kwa watanzania.
Huu umasikini na maisha mabovu mnaomlaumu JK yote yamesababishwa na CCM iliyowalea watanzania kuwa waoga, wasiojiamini, wenye hofu ya mabadiliko, waliolishwa itikadi ya kuamini wananchosema viongozi ni sawa (slogan ya zidumu fikra za mwenyekiti)...n.k yote haya kasababisha Nyerere...kama asingefuta vyama vingi baada ya uhuru (mfano South Africa) basi leo watanganyika mungekwisha isahau CCM...am I lying...?
Nyerere alikuwa mtu wa aina yake. Yeye alikuwa thinker and philosopher. Unaweza ukamlinganisha na thinkers kama akina Plato; Karl Max, na wengineo. Bahati mbaya kwake ni kuwa alizaliwa katika nchi maskini kama Tanzania. Kama angekuwa Mmarekani, saa hizi angekuwa anaenziwa na dunia nzima.
BWANA YESU alishasema NABII akubaliki nyumbani kwao.Hivyo watu kutomkubali MWL si ajabu maana hata maandiko matakatifu yalishatufunda kuhusu kukataliwa kwa Wakombozi wa jamii zao.
Kuhusu kuwepo uovu na ufisadi katika uongozi wa mwalimu hilo hata yeye alikiri, alishawahi kusema kuwa kutokana na ukubwa wa CCM anaifananisha na kokoro, kokoro likitupwa baharini au ziwani wakati wa uvuvi uibuka na samaki na wadudu mbalimbali na mauchafu kibao hivyo hata CCM uvuvi wake wa wanachama umepelekea kubeba wasafi, wachafu, manyang'au, mafisadi papa na nyangumi n.k
Pia MWL alishawahi kukiri kuwa yeye si malaika hivyo katika uongozi wake kuna makosa ambayo aliyatenda na kuwaomba msamaha watanzania kwa makosa hayo. Nyerere katika kukiri makosa yake hakuacha kutuhasa na kutufunza, pale aliposema, "uongozi wake umefanya mema na mabaya lakini anachowashangaa viongozi wa sasa badala ya kuiga yale mema wao wanaiga na kudumisha yale mabaya" Hapo Nyerere alishangaa na kuhoji uwezo wa viongozi wetu katika kutuongoza
Kwangu Mwalimu ni kiongozi mfano na wa kuenziwa, ni mfano wa uadilifu, na Nyerere na kwa TZ ni "ishara ya mchungaji na kondoo wake"
nyerere, alikuwa na akili sana tena sana.
Tunataka baada ya miaka 10 au 20 tuwe na mtanzania wa pili baada ya nyerere awe role model wetu. Huyu si mwingine bali ni dk. Slaa
Jifunze kiswahili kaka, amesema sana (very intelligent)Na wewe ndiyo huna au ndiyo inakuaje? :becky:
Thinkers Marekani!!! Wewe ambaye ni exposed unalisaidiaje taifa lako na Afrika kwa ujumla? Mchango wa Great Thinker Mwalimu Tanzania na Africa kwa ujumla unaendelea na utaendelea ku-enziwa daima. Hao thinkers wa Marekani wanatusaidia nini?Kuna hundreds and thousands of the so called "thinkers" huko Marekani. Haya ni matatizo ya kutokuwa exposed enough kujua kuna nini kikubwa zaidi ya hivyo vitabu vya Nyerere. Thinkings na philosophy ambazo haziko practical zinaitwa intellectual masturbation.
Na huyo Mkapa, chaguo la Nyerere, ndiyo mnaona alikuwa kiongozi wa maana? :confused2:
kuna tetesi kwamba kitabu cha mwalimu kiitwacho 'uongozi wetu na hatima ya tanzania' kimepigwa stop kimya kimya. kuna ukweli gani kuhusu hili??
ama kweli sitomsahau mwl nyerere kwa hili.
Mkapa was much much better kuliko huyu jamaa! Mkapa ndiye aliyejitahidi kuiletea kaheshima kidogo hii nchi yetu tukufu. Mkapa alikuwa anajitahidi kuifanya nchi ijitegemee yenyewe. Kuna miradi mingi ya kipindi cha mkapa imefanyika kwa kutumia pesa yetu yenyewe na si kupigapiga magoti kwa wahisani amao wanakupa misaada ya masharti. Sasa huyu jamaa yetu anadiliki kusimama jukwaani na kuona fahari kusema Obama kaniahidi hiki na kile!!! Stupid fool!! mifweza ya hepa yote ilitengenezwa kipindi cha Mkapa. Jamaa walikula lakini kilichofanyika atleast kilionekana.