Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😅😅 Pole Sana mkuuBinafsi sijawahi kabisa kucheza mpira ukiacha ile mipira ya makaratasi tuliyocheza utotoni. Sasa kuna wakati nilikua naishi karibu na uwanja mmoja ambapo pembezoni mwa huo uwanja kuna kanjia ka kuelekea home.
Siku hiyo sina hili wala lile najipitia zangu nje kabisa ya uwanja nikiwa nna mawazo lukuki juu ya ugumu wa maisha, na kuna mechi ilikua inaendelea mi wala sikua na time nayo. Sasa ikatokea jamaa kafumua shuti la juu juu huko mpira ukatoka nje ukawa unakuja uelekeo wangu. Mi nikauona ule mpira unakuja kwa juu, nikasema huu niutie kichwa urudi uwanjani.. Hua naona wachezaji wanavyopiga mpira kichwa wanaendelea na shughuli zao..
Bwana bwana..! Hivi kumbe mpira huu uone tu hivihivi aisee ukikupiga kichwani ni kama umepigwa na tofali! Kitendo cha kupiga kichwa ule mpira yaani nilihisi kama ubongo umechanganyika, kwa sekunde chache niliona nyotanyota, nikapepesuka kidogo huku nahisi kuanguka. Ikabidi nisogee pembeni kulikua na mti nikaegemea hapo. Ilichukua karibu dakika 5 akili kukaa sawa maana muda wote nilikua naona maruweruwe tu. Sijawahi kurudia tena na ule mtaa nikaja kuhama.