Nakumbuka nilikua kidato cha kwanza nikamzimia montress, Mwanaume sijawai kutongoza nikaona njia sahihi niandike barua.Nikajipinda nikaandika barua nikapangilia mistari nikachora na maua ya kutosha.
Nikafunga barua yangu mwanaume nikatia na jero (500) kwenye bahasha ambayo ilikua ni nauli nilopewa home.
Ishu ikaja kumpa ile barua nitaanzaje? Kwa vile alikua anakaa dawati la mbele yangu, nikaamua kesho yake niwahi shule malpema kisha nikaiweke ndani ya dawati lake.
Tulipoingia class ile asubuhi nikaona dada kafungua dawati kachukua barua bila kuisoma akaiweka kwenye begi lake, mwanaume nikajua mambo yanaenda sawa.
Majibu ya barua.
Dada ni mstaarabu akatumia mbinu ile ile akaandika barua kisha kesho yake asubuhi akaiweka ndani ya dawati. Mwanaume kukuta barua asubuhi nikaiweka kwenye begi ili nikaisomee home.
Duuuhhh! nilipoisoma barua nikakuta dada wa watu kanigombeza mbaya anasema wewe bado mtoto mambo ya mapenzi yaache subiri muda wako ufike.
Naomba uniheshimu mimi kama dada yako na ukome kuniandikia vibarua vyako.Duuuhh! niliishiwa nguvu. Ila pamoja na mikwara yote jero langu alichukuwa.
Je wewe unakumbuka ulivomtokea mwanamke/ mwanaume kwa mara ya kwanza ulitumia mbinu gani? Je ulifanikiwa?