Sitosahau nilipotongoza kwa mara ya kwanza

Sitosahau nilipotongoza kwa mara ya kwanza

Big Lion

Member
Joined
Jan 5, 2015
Posts
46
Reaction score
15
Nakumbuka nilikua kidato cha kwanza nikamzimia montress, Mwanaume sijawai kutongoza nikaona njia sahihi niandike barua.Nikajipinda nikaandika barua nikapangilia mistari nikachora na maua ya kutosha.

Nikafunga barua yangu mwanaume nikatia na jero (500) kwenye bahasha ambayo ilikua ni nauli nilopewa home.
Ishu ikaja kumpa ile barua nitaanzaje? Kwa vile alikua anakaa dawati la mbele yangu, nikaamua kesho yake niwahi shule malpema kisha nikaiweke ndani ya dawati lake.

Tulipoingia class ile asubuhi nikaona dada kafungua dawati kachukua barua bila kuisoma akaiweka kwenye begi lake, mwanaume nikajua mambo yanaenda sawa.

Majibu ya barua.
Dada ni mstaarabu akatumia mbinu ile ile akaandika barua kisha kesho yake asubuhi akaiweka ndani ya dawati. Mwanaume kukuta barua asubuhi nikaiweka kwenye begi ili nikaisomee home.

Duuuhhh! nilipoisoma barua nikakuta dada wa watu kanigombeza mbaya anasema wewe bado mtoto mambo ya mapenzi yaache subiri muda wako ufike.

Naomba uniheshimu mimi kama dada yako na ukome kuniandikia vibarua vyako.Duuuhh! niliishiwa nguvu. Ila pamoja na mikwara yote jero langu alichukuwa.

Je wewe unakumbuka ulivomtokea mwanamke/ mwanaume kwa mara ya kwanza ulitumia mbinu gani? Je ulifanikiwa?
 
mie sikuizi utuuzima unanijia kwa speed hata sikumbuki,au sababu sijanywa chai!! ntarudi mkuu nioe vijidakika vichache..
 
Daah braza umeanza kuhonga zamani kweli.
Hapa apaone miss chaga
 
Last edited by a moderator:
Mi nilimpenda sana ila kumwambia sikuweza basi ikawa hivyo hadi leo sijui
 
Big Lion ka ni mimi ningemdai hela yangu hadi school nzima wajue.
sisi wengine mitandao ya simu imekuwa ndio njia rahiiiiiiisi,yani ni kutumiana sms tu mwisho mnaelewana fasta

Samboko angalia hiyo tabia yako ka nakuona vile ulivyokuwa ukipata kipigo cha father,vipi ushaacha au ulikuwa utoto ?
Msalimie sana Tamalisa
 
Last edited by a moderator:
Big Lion ka ni mimi ningemdai hela yangu hadi school nzima wajue.
sisi wengine mitandao ya simu imekuwa ndio njia rahiiiiiiisi,yani ni kutumiana sms tu mwisho mnaelewana fasta

Samboko angalia hiyo tabia yako ka nakuona vile ulivyokuwa ukipata kipigo cha father,vipi ushaacha au ulikuwa utoto ?
Msalimie sana Tamalisa

Da Idd kumbe hapa ulinichokoza e
 
Wenyewe wanasema mwanzo mgumu imebaki historia sasa, bila shaka kibuti kikakupa ujasiri zaidi kwa aliefuata e...
 
Nakumbuka nilimwandikia barua nikamwabia wewe ni dokta wa ugonjwa wangu, lazizi cjiwez kwako sasa barua ikaokotwa na wambea wa shule hata hawakuamini kama ni mimi na ukauzu kama Hitler.
Mpaka Leo demu ni mke wa mtu na watoto wawili
 
Hata Kama nikiwatongoza bado wanaona kama nawatania tu!
Huwa naishia kuchambwa kwa kipindi kile ila sasa hivi ha ha!
Wanajigonga wenyewe najiuliza mbona sasa hivi hawachambi...😅

Ila tatizo lipo hapa "anaekupenda humpendi!, unae mpenda nae hakupendi!!"
Ndio maana wengine husema maisha ni milima na mabonde😜
 
Back
Top Bottom