Kama bahati tu, ilipofika saa 3 usiku kuna gari ya mizigo ilipita ,muda huo nikiwa nimekata tamaa ya kupata usafiri wakunifikisha sehemu Salama ukizingatia pale ni sehemu hatari sana, japo muda huo nilishakata kilometa kadhaa uelekeo wa Lindi
Kumbuka mpaka muda huo bado nilikuwa sijala chakula chochote ukiacha kile kipande cha nyama poli ambayo ilikuwa ni ngumu nilichokula usiku na wale majangili .
Konda wa hili gari alivyoshuka ili kuniuliza nahitaji kuenda wapi ghafla nikaona kama amesita wakati alipokuwa amesogea karibu na akawa anataka kurudi kwenye gari ,huenda hii ilitokana na jinsi muonekano wangu ulivyokuwa, labda aliniona kama kichaa au sijui ni mawazo gani yalimjia kichwani kwake juu yangu.....
NB wengine watamilizia