Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpwayungu ni muhuni tu kama jamaa yangu mmoja.Ndo nimeanza kuusoma.uzi leo nimefika sehemu najua unaendelea kumbe wajambia uzi washajamba mwenye uzi kakimbia
Mi napenda story hata kama ni uongo why watu wamwingilie hajamaliza?Mpwayungu ni muhuni tu kama jamaa yangu mmoja.
Imeisha hiyo 🤣🤣🤣SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Basi baada ya kina Kidagaa na bosi zake kuondoka, nikaona isiwe tabu kwa vile njia naijua nikaanza kutembea kufuata uelekeo wa lile basi lilipopita huku nikiangalia alama za matariri ya basi la MACHINGA ili nisije kupotea. Niliendelea na safari kwa muda wa masaa matano bila kupumzika na begi langu la nguo likiwa kichwani. NIkapita sehemu nikakuta wanacheza prutable. Kiukweli walinishangaa sana wale wacheza prutable lakini mimi sikuwajali nikaendelea na safari yangu huku begi lipo kichwani.
Kufika mbele kidogo giza lilishaanza kuingia nikaona hapa sina jinsi itabidi tu nitafute mti nilale juu. Na wakati huo njaa inauma kweri kweri. Sasa wakati najadili jinsi gani nitapata chakula na mti wa kulala, nikaona kwa mbali taa za gari. Ikumbukwe giza lilikuwa tayari lishaingia na mimi lengo langu lilikua nifike Lindi Mjini ili kesho niende Mlandizi kwa rafiki ake baba. Nikaona ngoja nilipungie ili gari linaweza kunisaidia kufika Lindi Mjini. Gari ile ikakairbia na kweli ikasimama. Ilikua ni Nissan Hardbody. Aliekua kwenye gari akashusha vioo vya gari nikaweza kumuona vizuri, dah huwezi amini alikua ni Yule mwarabu wa basi la MACHINGA alienirudishia nauli na kunikataza nisipande ile costa yao. Pembeni ya mwarabu alikua Kidagaa. Yule mwarabu akanitukana na kuniambia nitafia porini kwa sabu ya ujuaji wangu kisha akapandisha vioo na nikamsikia Kidagaa anasema IMEISHA HIYO, gari likatimua vumbi.
Kiukweli nilichoka sana na kuanza kujilaumu huu ujuaji unaniponza kwa kweli sasa nitafia kweli kwenye miji ya watu.
Itaendelea ………………………….
Daah..mpwanyungu ni farasi sana yule msengereme..[emoji28][emoji28].Imeisha hiyo [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ulitumwa na nani usome story zake kama huzipendi si ukojoe ukalale ??Mnalibembeleza la kazi gani hili jamaa la STD VII ya 1992?
Hatari sana-------SEHEMU YA SABA - - - - -
Nilipopewa msaada wa kuoga ikabidi nibadilishe nguo za kuvaa japo zimejikunya wale wadada wakacheka kidogo wakakausha, sikuwaomba ila kwa moyo mkunjufu wakasema nizivue wanipigie pasi nilitabasamu Kisha nikaingia maliwato kubadili nguo nikaenda kuwapa wakazinyoosha wakanipa. Niling'aa kwa kweli nilipendeza nikawa mtu. Baada ya hapo akili ikawa inawaza kwenye lengo lililonileta Kilwa japo popote akili ingenituma siku Ile ya safari ningeenda yaani ningeikosa gari ya Kilwa ila ipo ya Masasi ningepanda pia lengo nisiwepo Dar Es Salaam. Nikaona kujiajiri au kuomba kazi na ugeni huu sio jambo jepesi ila inabidi tu nijitoe ufahamu pia nisahau yote yanayonisibu. Nikaulizia wapi Kuna shule ya sekondari ya karibu wakasema labda Kilwa day. Nikabeba begi langu nikaenda kwa kuuliza mpaka nikafika japo Kuna kaumbali kiasi, nilipofika pale nikawakuta non. Staff members waliopo nje maana ilikuwa ni Jumamosi hivyo walimu walikuwa majumbani nilipowakuta wahudumu wa pale nadhani wapishi na walinzi nikasema nimekuja hapa nina shida na mwalimu either mwalimu mkuu, makamu au academic yule mlinzi akasema yupo makamu tu ngoja nikuitie kaa hapo.
Nilikaa sana kama masaa matatu hivi makamu wa shule ya Kilwa day akaja, tukaingia ofisini kuzungumza nikamwambia mimi nimekuja hapa kuomba kufundisha japo nimeishia form six, alitabasamu Kisha akasema aone vyeti alipoangalia akasema wana uhitaji wa mwalimu wa physics ila hana ruhusa ya kuniweka ili nifundishe bila ridhaa ya mkuu wa shule na mkuu wa shule anaumwa ana zaidi ya mwezi hayupo kwahiyo akirudi tutaongea.
Nilichoka sana mwishowe nikasema mimi nikipata pa kula na kulala tu nafundisha bure, akasema hawezi kuniweka bila uwepo wa mkuu wa shule kwa hiyo ngoma ikawa imebuma mwili wote upo hoi. Ikabidi nibebe begi niondoke Ile nabeba tu Kuna mwalimu mmoja kutoka shule ya Mtange sekondari jinsi alivyojitambulisha Kwangu akawa amefika Kilwa day secondary yule makamu akasema vipi huko kama mna shida ya mwalimu wa physics huyu hapa hataki hata Mia yako yeye apate pakula na kulala tu. Mkuu wa shule Mtange sekondari akasema ninao wakutosha walimu wakuajiriwa wamekuja wapya na watatu wanafundisha physics.
Nikasema basi tena lakini yule makamu akasema ngoja ampigie simu mwalimu wa Kivinje sekondari, hii shule ipo Kilwa kivinje. Yule mwalimu mkuu akasema yupo njiani ametokea Shinyanga kwenye msiba ila baada ya masaa matatu atakuwa yupo Kilwa Kivinje. Sijui alitumia usafiri upi kufika Kivinje maana Kuna watu humu mtasema Shinyanga mpaka Kilwa huwezi kufika mchana.
Yule makamu akasema nijiandae niende tukakutane lakini pia nimwachie namba yangu ya simu kwahiyo nikampa namba ila nikamwambia simu sina niliuza ili nipate nauli, akanipa pole akafunga ofisi tukaagana nikamuuliza huyo mkuu nyumbani kwake ni wapi akasema yupo pale pale Kivinje sekondari. Nikaenda stend ya kilwa masoko mida ya saa nane hivi kufika pale baadhi ya watu walioniona asubuhi nikiwa rafu wakaanza kunishangaa tena juu ya usafi wangu [uchafu walishangaa usafi wanashangaa pia.. Hii ndo kilwa]..
Mimi nikawa nipo straight forward na mambo yangu Sasa pale Kuna hiace na tax tu zinaenda Kilwa Kivinje gharama ni buku mbili, pesa ikaanza kupungua nikapanda nikasubiri ijaze siti zote tukaamsha. Kufika Kivinje bodaboda haoo unaenda wapi nikasema siendi.
Nikamuuliza jamaa mmoja anauza samaki akasema Kivinje sekondari ni mbali sana kufika kule kwa mguu na Hilo begi sidhani kwahiyo nichukue tu bodaboda hamna namna, nikachukua bodaboda nikasema nina buku hataki natembea kwa mguu, yule bodaboda akasema panda tukafika Kivinje sekondari ikawa ni saa kumi na robo hivi kufika pale yule mkuu wa shule akawa bado yupo njiani ila nikamkuta mkewe akapiga simu akamwambia nisiondoke muda si mrefu atafika.
Walikuwa ni wasukuma sio wamwera kwahiyo nilikaribishwa ugali na maziwa ya mgando na nyama ya utumbo la taulo nikala nikashiba, nilipumzisha shida zangu kwa mda huo. Saa kumi na mbili jioni akawa amefika mkuu wa shule ya Kivinje alipofika tukasalimiana na maongezi kiasi baada ya hapo nikamwambia kiwango cha elimu yangu, akasema ooh sihitaji wa form six mimi nikajua umehitimu chuo either diploma au degree maana afisa elimu kata hataki kabisa mtu afundishe bila kuwa qualified. Ikawa imebuma na siwezi kufosi.
Akaniambia amechoka sana anahitaji apumzike nikamwambia saizi ni saa kumi na mbili na nusu giza limeingia mimi huku ni mgeni naomba nilale hapa, akasema pole ila hata mm hii nyumba Ina Vyumba viwili tu na jiko na hapa sebleni, vile Vyumba wanalala watoto wangu na hapa sebleni haturuhusu maana sio sehemu ya usingizi ni sehemu ya kupumzika na kupata dinner and lunch.
Kule Kivinje sekondari hakuna bodaboda unless umchukue mjini na simjui bodaboda yoyote kwahiyo nikawaaga nikaondoka, ilinibidi nitembee kwa mguu nikiwa nimechoka sana kutoka Kivinje sekondari mpaka Kilwa Kivinje ni umbali wa kilometer 7 kama sio saba basi 8.saa mbili usiku nikawa nipo Kilwa kivinje.
Mfukoni nikawa nina 27000 ni nyingi sana kwa kipindi kigumu nilichokuwa napitia. Kufika pale stend nikaona yule bodaboda alienipakia mwanzo akapita kuniuliza vipi unahitaji usafiri? Nikamwambia hapana ila nimeteseka sana kupata bodaboda Kivinje sekondari ikabidi niukanyage, akasema pole ila mbona mkuu wa shule ana namba yangu kwanini hakunipigia nije nikuchukue, Sasa mm ilinibidi tu nikae kimya maana nilipandwa sana na hasira sijui aliona akimwita bodaboda atadaiwa yeye ndo alipe nauli?
Kilwa ni sehemu ngumu sana ukiweza kuishi Kilwa basi hata jangwani panakufaa. Kiustarabu kabisa nikasema ampigie ili nimwambie nimefika Kilwa kivinje salama alipopiga nikaongea nae akasema ngoja ajaribu shule moja ipo Lindi mjini yule mwalimu wanajuana sana nae ana upungufu wa walimu wa physics, nadhani huwa wanakutana kwenye vikao vya wakuu wa shule au wanajuana. Nikamwambia Sawa japo nikataka kuanza kukata tamaa ila nikasema ngoja nijipe uvumilivu kama mwanajeshi aliepo vitani.
Yule bodaboda akapigiwa tena na bahati ni kuwa tulikuwa bado tunapiga nae stori za hapa na pale, akapokea yule mkuu wa shule akasema mbona huyo kijana hajanitumia namba nikachukua simu sikioni mwa yule bodaboda nikasema mkuu mimi sina simu ila nitachukua namba yako nitakuwa naazima ukipata connection utaniambia.
Akasema yule mwalimu mkuu kakubali ngoja nikutumie namba yake muongee nae nikasema Sawa. Dakika tatu hivi akawa ametuma namba tukampigia akasema kesho niende nikamwambia mm ni form six sio chuo akasema hatuwezi ongea kwenye simu serious matter kama hii inabidi kesho niwe Lindi mjini niende shuleni kwake, akasema yeye ni mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Kineng'ene ipo manispaa ya Lindi.
Dakika kadhaa baadae yule dogo wa bodaboda akapata kichwa akaniaga akasepa ikawa mida ya saa tatu hivi nikaona bus la MASHALAH limefika Kilwa kivinje kutoka Dar Es Salaam sijui kwann Lilichelewa siku hiyo nikasema nikipanda hili Gari kwenda Kilwa masoko ni kupoteza tu muda na pesa zangu naenda kufanyaje. Nikapotezea ila akili ikanijia kwani Gari za kwenda lindi mjini zipo wapi?
Wenyeji wakasema nikitaka hata mida hii napata inabidi nipande bodaboda maana mida hii hakuna hiace wala tex lakini pia hiace na tex kituo huwa kipo kule hospital ya wilaya na muda huu kupata ngumu kwa hiyo njia pekee ni bodaboda ili inipeleke sehemu moja inaitwa NANGURUKURU pale ndokuna mabus ya kutoka mikoa ya mbali naweza Pata au malori ya kwenda lindi mjini.
Yule dogo wa bodaboda nilitaka nimuungishe lakini akawa ameondoka nikachukua bodaboda nyingine ila nauli iliniuma sana maana kila mtu alisema mwisho 4000 ikabidi tuondoke mpaka NANGURUKURU ikawa ni saa nne usiku nipo NANGURUKURU kuona kama nitapata usafiri wa kwenda Lindi mjini mda huo.
-------inaendelea usichoke.........
Ilikuwa Ni story nzuru Seema sas msimuliaji Ni nyoko sanaHatari sana
Kwanini na yeye asimalizue? Ingekuwa BAO angesusa?Mi napenda story hata kama ni uongo why watu wamwingilie hajamaliza?
Ni series kabisa,amekukwaza wapi au wee mmwela nini???😂😂😂Ilikuwa Ni story nzuru Seema sas msimuliaji Ni nyoko sana
Mara 5 shekhe,sio 4Msikitini huswali mara 4 kwa siku,asubuhi mchana jioni na usiku,hata ungeenda na jina lako la kikristo kuwaomba msaada hawatakufukuza maana ni dhawabu kumsaidia mgeni.Watu wengi sana tunawasaidia