Dah! Ukiona mtu anaomba lift Kwa Bodaboda ujue kweli Yuko serious, nimejikuta nacheka na kuhuzunika Kwa pamoja.
Kwamba ukiwa hauna pesa unajulikana tu.
Hii stori inanikumbusha siku naenda kuanza kidato Cha sita Moshi nikitokea Kanda ya kati kupitia Arusha, sitasahau maishani mwangu. Nimefika Arusha nikalala kesho yake nikutane na ndugu yangu anaetokea Dar kuniletea pesa za ada na matumizi, kumpigia Kwa zile box za ttcl, ananiambia nishushe Dar, hatoweza kuja Arusha...hapo nna pesa ambayo nililala guest tu, nakosa nauli ya kwenda Dar
Niliadhimia kulala nje ili nibanie pesa ya kulala guest inisaidie nauli kesho yake. Nikadhania stand ya Arusha watu wanakesha ili nijumuike nao Hadi asubuhi, kumbe pale watu hawakeshi. Nikajitutumua nikapiga kahawa kutoa usingizi na kupunguza machungu ya baridi.
Watu walianza kupungua nikabaki peke yangu, nikawa nakatiza mitaa kama ntabahatisha sehem kijiwe nikeshe, wapi. Ikafika mahala nakutana na polisi wa doria na mbwa, nikaona hapa ntaishia lockup.
Ilipofikia saa nane kasoro usiku, nimepigwa na baridi, nilivaa t-shirt tu, nikafanya maamuzi ya kutafuta guest house nilale, sikuwaza Tena mambo ya nauli. Nilihangaika sana guest zilikua zimejaa. Nikaja kupata njia ya kuelekea Ilboru. Ilibaki chumba kina vitanda vitatu, Kwa hasira nililala Cha kwanza, nikaenda Cha pili, nikamalizie Cha tatu, wakati naingia yule Mama mhudumu ananiambia Kuna maji ya kuoga ya moto, sikumbuki nilimjibu kitu Gani lakini sikuoga Wala kutoka Tena Hadi asubuhi.
Kesho yake Nimeenda stand, nauli Sina, nawaza niongee na makondakta nikifika Dar niwasiliane na ndugu niletewe nauli niwaachie bag. Kila nikiwaza Hilo Wazo ujasiri unaniishia, sikuweza kuondoka. Nikaamua kuwa mtalii natembea bila kujua naelekea wapi, nilijikuta Kijenge huko ndio muujiza wangu ulipokua. kilichotokea Mungu alikua na makusudi yake.
Ni kitu kimenifanya Hadi Leo mtu akiniambia ana shida/ tatizo nimsikilize Kwa kutulia.
Sikwenda Dar nilipotakiwa kufuata pesa za ada na matumizi, nilijikuta nimefika sehem sahihi hapo hapo Arusha, nikaambiwa nisubirie ntaletwa Kila kitu kabla ya kuelekea shule Moshi. Nilikua naambiwa ingia ndani, naogopa nataka nikae chini. Yaani matatizo yaliyonipata na zile shida naona kama Kila mtu anajua yaliyonipata na hadhi yangu sistahili hata kuingia kwenye nyumba ya watu.
Jioni najifanya kuaga utafikiri nna pakwenda, ndio nikaambiwa tumeambiwa usiondoke Hadi utakapoletewa vitu vyako.
Mwisho, ukipata nafasi ya kumsaidia mtu Kwa namna yeyote Ile, na ukaona kabisa unapata msukumo moyoni mwako, Fanya hivyo. Usijiulize maswali mengi sana ( sikiliza moyo unasemaje) akikutapeli mwachie Mungu tu, itakua umefanya Kwa nafasi Yako.