Sendoro Mbazi
JF-Expert Member
- Jan 18, 2013
- 3,329
- 2,169
Duj
Duh pole
Nilipoingia kwenye vichaka sikupata usingizi zaidi ya kuwa na mawazo yasiokwisha, ukiwa mpweke tena porini usiku masaa hayaendi kabisa kwahiyo ikabidi nikaze roho na kumwomba mungu maana hiki ndokipindi ambacho mungu anatamkwa mara nyingi zaidi yaalivyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu. Sikupata majanga yoyote nilipokuwa ndani ya vile vichaka mpaka palipopambazuka, saa kumi na mbili kasoro ilinibidi nijongee taratibu kuelekea barabarani huku nikijifanya kama nimetoka tu kuchimba dawa. Hapakuwa na watu wanaopita maana ni asubuhi sana ni wachache tu niliowaona hata watatu hawafiki ila nikaona baada ya mda flani hiace, pikipiki na kila Aina ya magari yapita huku na kule nikasema kumbe kumekucha. Mda si mwingi ikapita hiace inaenda mjini konda akasema panda haraka nikamwambia nitajie nauli nitapanda akasema nauli ni jero, nikapanda kwenda mjini baada ya mda mchache tukawa tumefika ikawa ni saa moja na nusu hivi asubuhi. Ikumbukwe kuwa sikuwa na simu ila nina namba za huyo mkuu wa shule ya kineng'ene ninakoenda kwahiyo ikabidi kwanza nijiweke Sawa kimwili na kiakili nisije tena kutia aibu. Kama ilivyo ada ikabidi nizunguke kutafuta kigest uchwara nipate msaada wa kujimwagia mwili wangu maana nilikuwa nimeanza kupauka niliipata gest moja hivi nyuma kidogo ya stend ya mkoa inaitwa SOUTH HONOUR imetazamana na ukumbi flani hivi wanaonyeshaga mpira. Nikaingia mle ndani nikamkuta muhudumu ni mdada nikasema hapo Sawa hawa wanawake sio wachoyo, nikamwambia hali halisi akasema kuoga 500. Nilitaka kusita kidogo lakini nikasema Sawa nielekeze nioge nikaelekezwa nikaenda kuoga.
Nikamaliza kuoga nikavaa nguo zile zile maana hakuna zenye uafadhali zaidi ya hizi zilizopigwa pasi japo nazo zilianza kuonekana zimepitia misukosuko kiasi. Nikaingia mfukoni nikampa 500 yake huyo mdada anaitwa Zena kutokana na watu walipokuwa wanamwita maeneo hayo ni mmwera pia kutokana na tabia aliyoionesha nisingekuwa na pesa basi nisingeoga. Baada ya hapo nikabakiwa na 15000 tu mfukoni nikasema ngoja nitoe jero nipate tangawizi na kalimati ndonisepe, kutoka tu nje Kuna mdada alikuwa amebeba beseni akasema kaka karibu MING'OKO, hili jina ni geni Kwangu nikaona sio mbaya ashushe beseni nione aliponionesha nikaona ni mizizi tu kama hii inayotambaa kwenye miarobaini ila kutokana na njaa nikasema haya madude inaonesha yanashibisha mihogo cha mtoto kwahiyo nikamwambia anichotee ya 500 nikasisitiza ya kushiba. Alinijazia bakuli nikaanza kula japo hayakuwa na radha lakini sikujali maana lengo ni kushiba na sivinginevyo baada ya hapo nikampa 500 yake mm nikabeba begi langu nikapotea.
Ilinibidi nirudi tena stend nikachukue sasa dalalada za kwenda huko kineng'ene secondary ila kabla sijapanda nikauliza wenyeji wakasema nitashukia kituo kinaitwa MTANGE halafu baada ya hapo Kuna barabarani ya vumbi inaenda mpaka huko. Nikasema Sawa nikapanda hiace nakumuuliza konda bei akasema 500 nikamwambia hapo powa, hiace akaondoka mida ya saa nne hivi tukafika MTANGE mda si mwingi ila kumbe MTANGE ni mbele kidogo tu yapale nilipolala kwenye lile pori lenye mabwawa ya chumvi nilijiraumu kupoteza nauli Bure ila ikawa hamna namna. Nilipo shuka MTANGE bodaboda hawakosi kila penye kituo hawa watu, wakaja kunivamba kama sita hivi kwa mkupuo nikasema siendi popote, ilibidi nitumie hii akili maana bodaboda ukimuuliza njia atasema ni mbali ili apige mkwanja Sasa mimi sikutaka stori yoyote na wao japo wanasaidia pia. Nikaenda kumuuliza dogo mmoja hivi hana kazi yoyote akasema huko ni mbali sana tena shuleni ni mbali zaidi nikamwambia kutembea kwa mguu kwani watu hawaendagi? Akasema wanaenda baadhi ila ni mbali. Nikaondoka kuuliza bodaboda wakasema nauli 2000 nikasema Sina nina buku wakakataa wote japo Kuna jamaa akasema nisubiri apate kichwa kinachoenda kineng'ene ili tupande mshikaki nilipe buku, nikaona huu utoto nikasema njia iko wapi akasema nyoosha hii ya vumbi mpaka mwisho.
Safari ya mguu kwenda kineng'ene sekondari ikawaka moto nikasema saizi sitoi pesa hata itokee shida gani labda nivunjike mguu hata hivyo Nitatambaa tu, nilipiga mguu mpaka nikawa nahisi kizunguzungu viatu nilivyovaa vilikuwa vyeusi vikawa vyekundu huku natimuliwa na mavumbi ya gari na pikipiki. Safari nilipoona haifiki mwisho ikabidi nisite kidogo niulize wenyeji kama nimekaribia kufika huko niendako, nilisimama sehemu nikamuona mama mmoja kakaa chini ya mkorosho nikamfata kuomba maji ya kunywa, nilipokunywa maji nikauliza kama sijapotea njia ya kwenda kineng'ene akasema nifate hiyo hiyo barabara ila bado mbali sana. Nikampa Asante za kutosha nikasepa nilitembea sana jamani yani ilifika kipindi nikaona umasikini unatufanya binadamu tuonekane kama manyani hivi maana binadamu halisi ni ngumu kupitia hizi fedheha. Kama baada ya masaa mawili kwakuhisi nikasema niulize tena wenyeji Majamaa flani yakasema ni hapo tu mbele kidogo kunja kona kwenye hiyo mikorosho Fata barabara utakutana na shule. Baada ya mda nilifanikiwa kufika na kupokelewa na stuff members nilipowaambia wakasema mkuu wa shule yupo darasani ila nenda kwenye lile jengo ndoofisi yake ilipo kamsubiri.
Kweli baada ya nusu saa akaja ofisini akanikuta nje nikamwambia mm ndoyule tuliyeongea Kuja kufundisha, akasema Sawa ingia Tuongee. Tulitambuzana kwa mda na kucheka japo mm nilikuwa na cheka kumridhisha tu maana nimepondeka na matatizo sana. Baada ya maongezi akasema je nina ndugu huku nikasema hapana akasema Sasa kijana Shida ya hapa ni pakulala maana Kuna kijana hapa huwa nakaa pekee ake nikajua mtakaa wote ila bahati mbaya ndugu zake wamefika Jana usiku Kuja kumsalimia nahaijulikani wataondoka lini.
Baada ya hapo akasema nirudi ataniita. Namm nikamjibu kwa ghadhabu kwann hukunipa taarifa mapema akasema alimtaarifu yule mkuu wa shule ya kivinje sekondari ila akamwambia Sina mawasiliano na alijaribu kumpigia yule kijana bodaboda niliekuwa nae pale stend ya kilwa kivinje yule kijana akamjibu Ana abiria anampeleka sehemu kwa hiyo ameniacha stend. Hivyo taarifa ilitolewa mapema ila kutokuwa na mawasiliano ya simu ndotatizo. Yule mkuu wa shule akaniambia nirudi Hao wageni wakiondoka ataniita, kwahiyo safari ya kutoka kineng'ene kwenda sehemu nyingine ikaanza kuleta dalili.
........ Inaendelea usichoke.
Duh pole