Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Kuhusu hawa wanaosema ni chai we achana nao hawa ni binadam walivyo hata ukiwaambia unaumwa hawatakupa mchango wowote ila ukifa watatoa rambi rambi huku wakisema kumbe alikuwa anaumwa kweli?
 
Daaaah mkuu umenikumbusha mbali sana,niliwahi kulala nje hapo kilwa kivinje ,karibu na bandari,bahati nzuri nikipata sapoti ya Mzee flan mvuvi alikuwa anasubiri mashua ya kwenda mafia,kipindi hicho nilikuwa natoka kuchimba dhahabu na safaya mbwenkulu,Lindi ndani ndani ,napakumbuka Mangaka,masasi,Lindi ,kilwa,kwa bahati nzuri kesho yake nilipata lift ya roli la sementi nikafanikiwa kurudi daa,mazingira ya huko ni magumu sana ikiwa mgeni
Lindi kuna dhahabu.?? Nieleweshe vizuri mana ndio nasikia leo hii taarifa.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
------SEHEMU YA NANE - - - -

Ilinibidi nipande bodaboda pale Kilwa kivinje kuelekea Nangurukuru kama nilivyoelekezwa na wenyeji huko nitapata usafiri wa kwenda Lindi mjini hata kama ni usiku kiasi gani. Tukafika Nangurukuru saa nne hivi nikampa 4000 yake bodaboda nikawa nimebaki na 23000 nikasema sio mbaya pesa ya emergency ipo.

Pale Nangurukuru uhuni uliopo nilioukuta ni kuwa hupati gari bila dalali na mimi nikawa nimechacha hata nauli ya kutoka Nangurukuru mpaka Lindi mjini siijui na wale madalali wakiona mteja wa usiku wanajua nina shida ya lazima either msiba au kikazi.

Niliona Kuna wamama pembeni wananitamanisha samaki zao huku magari private yakiwa yanasimama wanunua samaki na kufungiwa kwenye bahasha wanaendelea na safari ila mimi nikasema napenda sana samaki ila sitanunua inabidi nijizuie tu hata nikiambiwa changu mwenye kilo 5 kwa buku sichukui maana hii pesa na huko niendako haitoshi.

Majamaa wa pale ambao huenda hawalali wakawa wanasema usafiri wa lindi mda huu ni mgumu ila sio sana kwahiyo niwe mvumilivu na nauli ni 10000 na yeye nimpoze hata buku 3,nikasema Sina pesa nisaidieni tu hapa nina 7000 tu Majamaa yakacheka ya kasema hiyo pesa hata kwa Lori hawakubali. Pale Nangurukuru sio sehemu ya makazi ya watu ni barabarani ambapo mabus huwa yanasimama kwa mda ili abiria wapumzike, wale na kuchimba dawa kwa hiyo kama sitapata usafiri inabidi nitafute hotel na kwa mazingira yale lodge hata ya buku ten hupati labda kuanzia na 20000.

Sina hili wala lile nikaona gari Aina ya Noah imesimama pale Majamaa chapu wakaongea nae wakaja Kwangu oyaa wahi mpe huyu elfu kumi na mbili sisi 2000 tu inatosha, nikasema Sina nina 7000 tu Sina hata pesa ya ganji hapa nilipoongea tu jama mwenye gari akaondoka kuendelea na safari yake ya Lindi.

Wale Majamaa wakaniambia ukweli kuwa bila 10000 sipati usafiri Kuna Lori moja hivi la Dangote lilipita pale Majamaa ya kasema juu kwa juu tunae wa buku saba tu, dreva akasepa, mpaka inafika saa tano sikuona bus lolote.

Ile nimetulia zangu nikiwa na stress nikasema hapa lazima nitoboke mfuko vinginevyo naumbuka, sijakaa Sawa Gari Aina ya Kosta hiyooo ilikuwa imebeba msiba wakapita pale kununua samaki na kuchimba dawa wale Majamaa wakamfata dreva na kuongea nae sikujua waliongea nini ila Majamaa yakaja chapu yakasema toa hiyo 7000 tukamshawishi, nikawapa Ile kuwapa tu yakasema nenda kapande mm nikaenda dreva alipokuja akasema wewe ndo unaenda Lindi??

Nikawaambia ndio akasema nikae nyuma kabisa tubanane maana Gari siti zipo full nikaenda kukaa nyuma uzuri waliokuwa pale ni wembamba kwahiyo tulifit nikakaa kwa uhuru. Nilikuja kujua Ile pesa dreva hakuchukua hata Mia na yule dreva alikuwa ni paroko au muhudumu flani wa kanisa kutokana na nguo alizovaa ni zawale wachungaji lakini pia wale Majamaa kwa nini hawakuomba hata buku tu ya kahawa na kipindi dreva anaingia aanze safari hakuonana tena baada ya wale Majamaa kuchukua mkwanja, kwa hiyo nikawa nimeliwa za kichwa lakini kwakuwa lengo langu limetiki sikuwaza sana wala kuiletea tamaa hiyo buku 7.

Safari ya kutoka Nangurukuru kwenda Lindi mjini ikaanza usiku wa saa tano na nusu hivi huku nyimbo za kuabudu na maombolezo zikitawala kwenye Costa zikiwemo zile za parapanda. Nilikaa na watu sio wanyama kwahiyo ilinibidi niwe mstarabu wa kuwauliza chanzo cha msiba, wapi wanaenda kuzika na kuwapa pole za kutosha, wengi wao walikuwa wakitafuna samaki wengine wakitoa machozi ya mpendwa wao roho ilipoacha mwili, wengine wakipashana Habari za hapa na pale.

Nilipouliza msiba unaelekea wapi wao wakasema wanaenda Masasi nikasema ni bora maana Masasi ni mbele ya Lindi kwahiyo itanifikisha Lindi mjini. Baada ya hapo sikujua kilichoendelea tena maana nilishikwa na usingizi mzito mpaka nikawa naota matukio ya nyuma nilikuja kukurupuka ghafla nikawauliza wenzangu Tupo wapi wakasema tumepita lindi mjini muda si mwingi halooo nilibwata kwa nguvu maana hali yangu ya uchumi haiko Sawa nikasema dreeevaaaa simamaaaa, yule dreva akasimama Ile kutazama sura yangu akasema duh mtumishi nisamehe nimejisahau kabisa kuwa nina mtu anashuka lindi mjini ila sio mbali na hapa kwahiyo shuka upande hata pikipiki. Nikashuka zangu wao wakaendelea na safari.

Ni usiku mzito sikujua ni saa ngapi ila umbali wa Nangurukuru to Lindi town ni zaidi ya masaa matatu kwahiyo ilikuwa ni saa tisa usiku nipo peke angu nje kidogo ya mji wa lindi na ubovu nikuwa niliachwa kwenye pori flani hivi Kuna mambwawa mengi ya kuchimba chumvi.

Niliposhuka nilijilaumu sana ni kwanini nimekubali kushuka kwenye hili pori na nitaamini vipi ni karibu na mjini na saizi ni giza nene vipi juu ya usalama wangu, for sure ni zaidi ya dk 30 au 40 sikuona gari lolote linapita wala chombo chochote cha moto, nikaona kujianika barabarani ni hatari zaidi bora niingie kwenye vichaka nijifiche tu maana huu mji mm ni mgeni kabisa. Nikaangalia mazingira ya kwenda kujificha kama dk 3 hivi nikaona gari Aina ya Dabo kibini imefika pale nikasema mungu wangu hawa mbona wapo kikamanda nipo salama kweli??

Walisimama kwa dakika chache bila kufungua kioo nikaona haoooo wamesepa nikasema asante yesu, huenda waliniona pia nimejichokea kwahiyo hawataambulia chochote. Nikaingia porini fasta ndani kidogo ya yale mambwawa ya chumvi nikatulia huku nikimwomba sana Mungu anilinde, pamoja na kelele za wadudu na wanyama wadogo wadogo pia kuhisi kama Kuna mtu anakuita au anakunyemelea nyuma sikujali ilibidi nijikaze tena saa zingine Kuna mti uliniogopesha nikajua ni mtu. Mida ya saa tisa na nusu hivi nipo porini ndani ya msitu wenye giza.

........ Inaendelea usichoke......
 
Back
Top Bottom