Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Hili swali ni zuri sana msikitini na kanisan au hata polisi,alikuwa anahofia nin?,watu wengi wanapopotea au kufika sehemu ngeni kimbilio lao ni msikitini
Msikitini huswali mara 4 kwa siku,asubuhi mchana jioni na usiku,hata ungeenda na jina lako la kikristo kuwaomba msaada hawatakufukuza maana ni dhawabu kumsaidia mgeni.Watu wengi sana tunawasaidia
 
Stori ya jamaa imenifanya niende nikafukue ofisini namba ya simu ya dada fulani pale makete ili nimlipe fadhila, bahati mbaya namba alishapewa mtu mwingine.

Imagine huyu dada nilifika pale makete nilikuwa sina hata mia na ishakuwa jioni. Nikaenda gesti kwa sababu chimbo nililopanga kulala palikuwa na baridi kali sana. Yule dada mhudumu wa gesti nilivyoanza kumpiga sound tu akanikatisha, akasema usiendelee kuongea akasema nifate.
Akanionesha chumba nililala bure kabisa nilipewa na maji ya moto japo sikuoga.
Wanaume tunapitia mengi jamani asikwambie mtu.
 
-------SEHEMU YA KUMI - - - - - - -

Aiponiambia nirudi halafu wale wageni wakiondoka ataniita mm nikamwambia Sina simu utaniita vp? Akasema basi niwe namuuliza mara kwa mara lakini bado sikuweza kukubali kirahisi maana nikahisi labda wananichezea akili hawa japo sio kweli mpaka ilifika mda ikabidi nimuulize kwanini huyo kijana alikubali ilihali anajua atapokea wageni, mkuu alijibu kuwa hakupata mawasiliano na yeye maana huyo kijana anakaa kwenye Vyumba viwili na wiki chache alisema tukipata mwalimu chumba kipo ila baada ya hapo Jana usiku kumpa taarifa akasema anaugeni na hajui watatoka lini pale. Nilimwambia ukweli kwamba nimechukia na mdaa sielewi naenda wapi maana huku mimi ni mgeni.

Baada ya kuonyesha uso wa simanzi nikaona kachukua simu yake akampigia mwalimu mmoja hivi shule inaitwa Mwitero sekondari kama sijakosea kwa mjibu wa maelezo yake ila huyo mwalimu akasema shida ni accommodation. Akampigia tena mkuu wa shule flani inaitwa CHINONGWE SEKONDARI nikasikia anasema mwambie aje maana hapa nina mwalimu mmoja tu waphysics, nilisikia maana alikuwa ameweka loud speaker, baada ya hapo nikamwambia siendi mpaka anihakikishie asilimia mia kuwa nikifika siondoki halafu amwambie na level yangu ya elimu kuwa ni form six. Mkuu wa shule akachukua simu akampigia tena akamwambia kila kitu akasema niende.

Baada ya hapo nikiwa nimechoka sana ilibidi nimuage mkuu wa shule ya sekondari kineng'ene kuwa naondoka namtakia kila raheli. Akasema nimsamehe kwa usumbufu hivyo nikachukua namba ya yule mwalimu wa shule ya sekondari CHINONGWE nikaondoka zangu. Huyu mkuu wa kineng'ene alisema CHINONGWE sio mbali sana ipo wilaya ya RUANGWA kwakina Kassim majaliwa Kassim sikuleta ubishii kwa kuwa sipajui. Ikanibidi niende mpaka pale barabarani nikasema hapana hapa lazima Niite bodaboda kwakweli inipeleke mpaka main road yaani mtange. Kuna dogo mmoja akapita na pikipiki nikamuuliza kijanja unaenda wapi akasema mtange nikamwambia nipe lift basi dogo akasema nimpe buku tu, nikamwambia poa tuondoke. Huu mda nilikuwa na hasira za ghafla sana kutokana na mambo tu ya hovyo yanavyoniandama, mda si mwingi tukafika mtange nikashuka.

Nikataka kupanda hiace za kwenda town ili nikadake gari za kwenda luangwa lakini nikasema ngoja niulize huenda njia nihiihii. Nikamwomba yule dogo tuliekuja nae kwenye pikipiki aniazime simu yake nimpigie huyo mkuu wa shule ya sekondari CHINONGWE anipe maelekezo ya kutosha nafikaje huko. Nikapiga simu akasema shule ipo wilaya ya RUANGWA lakini nisipande Costa zakwenda huko maana shule ipo mbali sana na wilaya badala yake nipande Gari za MASASI nishukie NDANDA halafu baada ya hapo nimpigie simu atanipa maelekezo. Baada ya hapo dogo akasema nisubiri hapa hapa gari za masasi zitapita, kweli baada ya dk chache ikaja Costa ya kwenda masasi nikauliza nauli konda akasema 4000 nikaguna kidogo nikamwambia nashukia NDANDA akasema ni 4000 nikaona isiwe tabu nikapanda safari ikaanza. Masaa mawili hivi baadae tukafika ndanda nikashuka. Nikawa nimebakiwa na buku teni tu mfukoni (10000).kufika ndanda nikamfata jamaa mmoja alikuwa anauza mahindi ya kuchoma kandokando ya barabara Nikamwomba simu yake nimpigie huyo mkuu wa shule ya CHINONGWE anipe maelekezo jamaa akasema simu yake haina salio ila bahati nzuri kulikuwa Kuna mteja anasubiri hindi pale akadakia akasema taja namba tumpigie. Nilipompigia akasema Kuna dreva bodaboda anamtuma mda si mwingi yupo hapa ndanda aje kunichukua kwa hiyo nisubiri kwa huyu muuza mahindi nanimwambie nimevaaje ili amuelekeze huyo bodaboda ila nisiondoke kwa huyu muuza mahindi atanikuta.

Kweli baada ya nusu saa jamaa akatokea alivyofika tu akasema Kuna jamaa nimekuja kumchukua anaenda kijiji kinaitwa CHINONGWE nikamwambia ni mimi hapa. Tukapanda kuelekea CHINONGWE, huko ni mbali sana halafu barabara niyavumbi usafiri ni shida maana ipo Costa moja tu inayopita njia hiyo kwenda nachingwea na ikipita hakuna tena usafiri zaidi ya bodaboda, kwa mujibu wa huyo bodaboda alivyosema. Ilikuwa ni safari ndefu mno yenye mabonde mengi Sana lakini mida ya saa kumi na moja jioni tulifanikiwa kufika chinongwe sekondari. Baada ya kufika mkuu wa shule akapigiwa simu na bodaboda ili apewe malipo yake yule mkuu akasema mwambie huyo kijana akupe mm hapa niko mbali na pesa Sina pia. Yani hapa ndonilichoka bodaboda akasema huwa ni 10000 ila kwa huyu mwalimu huwa anamfanyia 7000 nikasema mm Sina pesa jamani huku nikionyesha uso wa huzuni na majanga. Jamaa akapiga simu tena, mkuu wa shule akasema nitoe 5000 elfu mbili watamalizana wao. Ikabidi nilipe 5000 nikabaki na buku tano tu mfukoni.

Nilipofika kumbe mkuu wa shule alikuwa amemwambia makamu wa shule aje anipokee. Makamu wa shule ya sekondari chinongwe aliyefahamika kwa jina la JAFE akaja kunipokea akasema tuingie ofisini. Huyu makamu alikuwa mbinafsi sana afu ana katisha tamaa lakini mbeleni nitaeleza alivyokuja kunisaidia. Makamu akaenda nje kumwita mwalimu flani alikuwa anasimamia ujenzi wa shule na mwalimu flani hivi ni mdada wakiiraki au wamburu wa babati, walipokuja makamu akasema jamani tuna mgeni lakini huyu mgeni atakuwa analipwa na nani hapa?. Mimi nikadakia nikamwambia mm staki malipo ila nipate pakula na kulala tu, wakacheka ila mm nilikuwa very serious maana sikutaka kabisa masihala tena. Yule makamu akawa anamlaumu mkuu wa shule akisema huyu kijana atatufedhehesha tu maana hana simu, pesa ya sabuni ataipata wapi, pesa ya mafuta na mengineyo na wewe unaogopaga kuchangisha wazazi kulinda nafasi yako. Mizozo ilipoanza nikaona yule madamu wakiiraki akasema jamani huyu mkaka anaonekana uso ni mzito kachoka sana na mda huu ni saa moja kasoro ebu tumtafutie sehemu ya kulala.

Yule madamu akaenda kufanya usafi nikatandikiwa nguo kwenye sakafu maana walisema hawakupewa taarifa mapema hivyo godoro hamna mm nikasema haina shida. Nikiwa nimelala njaa inaniponda usiku wa saa nne hivi naona makamu anasukuma mlango maana hauna komeo kutokana na kile chumba kina mda hakina mtu hivyo hakikufanyiwa matengenezo. Alipokuja akasema mimi nakushauri hapa uondoke kijana hii shule mm ndomkongwe hata huyu mkuu kanikuta, hii shule haina rasilimali yoyote utaishije humu bila pesa??. Sikutaka kumjibu zaidi ya kuwa kimya ghafla nikaona sauti ya pikipiki mjengoni makamu akaenda nje kupokea mzigo flani mwenye pikipiki akasepa. Kumbe zilikuwa CHIPSI YAI aliniagizia nikala nilipokula akasema nipumzike ila asubuhi nifanye mchakato kwingine pale hapanifai maana huyu mkuu wa shule anakurupukaga bila kuwashirikisha na hata hivyo nitafedheheka mbele ya wanafunzi maana ukiwa huna pesa unaonekana tu. Mimi nikalala kusubiri kesho yake tuzungumze yote mbele ya mkuu wa shule alienihakikishia kwa asilimia mia kuwa sitaondoka.

....... Inaendelea usichoke......
 
Stori ya jamaa imenifanya niende nikafukue ofisini namba ya simu ya dada fulani pale makete ili nimlipe fadhila, bahati mbaya namba alishapewa mtu mwingine.

Imagine huyu dada nilifika pale makete nilikuwa sina hata mia na ishakuwa jioni. Nikaenda gesti kwa sababu chimbo nililopanga kulala palikuwa na baridi kali sana. Yule dada mhudumu wa gesti nilivyoanza kumpiga sound tu akanikatisha, akasema usiendelee kuongea akasema nifate.
Akanionesha chumba nililala bure kabisa nilipewa na maji ya moto japo sikuoga.
Wanaume tunapitia mengi jamani asikwambie mtu.
Sorry, ulipoenda Makete ulikuwa umeshamaliza chuo kikuu/ulikuwa na elimu gani na umri gani?
 
Kwa nn ucngekubali kulala hata darasani unakubali kwenda afu utarud wagen wakiondoka?.....ila story ipo inspired mkuu
Madarasa ya wanafunzi wanawahi kuhesabu namba saa kumi na mbili na nusu asubuhi waje wasafishe madarasa yao mimi niwe nimelala humo?.au niwe nakurupushwa naamka mapema halafu kuoga na nguo zangu naweka wapi? Shida zipo ila fedheha sio sifa
 
Stori ya jamaa imenifanya niende nikafukue ofisini namba ya simu ya dada fulani pale makete ili nimlipe fadhila, bahati mbaya namba alishapewa mtu mwingine.

Imagine huyu dada nilifika pale makete nilikuwa sina hata mia na ishakuwa jioni. Nikaenda gesti kwa sababu chimbo nililopanga kulala palikuwa na baridi kali sana. Yule dada mhudumu wa gesti nilivyoanza kumpiga sound tu akanikatisha, akasema usiendelee kuongea akasema nifate.
Akanionesha chumba nililala bure kabisa nilipewa na maji ya moto japo sikuoga.
Wanaume tunapitia mengi jamani asikwambie mtu.
Sehem gan makete,kesho naenda huko nielekeze nikampe salam zako
 
Sorry, ulipoenda Makete ulikuwa umeshamaliza chuo kikuu/ulikuwa na elimu gani na umri gani?
Kuharakisha maisha tu, nyumbani sikuwa na shida yoyote ile kila kitu uhakika, na niliaga vizuri tu japo walisikitika kwa maamuzi yangu. Baada ya kumaliza fm 4 nikaona kula vya bure nyumbani inatosha, nikasema nitafute changamoto mpya.

Mambo yalivyokuwa magumu nikapiga simu kwa mama anitumie hela japo sikufanikiwa kuitoa kutokana na changamoto ya mawakala kutoka makete hadi ikonda sikuona wakala. Kutoka Makete hadi Ikonda nilitembea masaa matano kwa mguu.
 
Back
Top Bottom