Sitosahau siku nilipomuona mwalimu wangu anatoa machozi baada ya kupokea barua ya kufukuzwa kazi!

Sitosahau siku nilipomuona mwalimu wangu anatoa machozi baada ya kupokea barua ya kufukuzwa kazi!

inaweza kuwa kampuni na ikasajiliwa brela na wizara ya elimu. Ishu ni mishahara yao kwa walimu ni midogo tena hakuna mikataba ya kueleweka. Watu wa idara ya kazi wakienda kukagua huzugwa tu kuwa hao walimu wanajitolea bure ili kuficha ukweli kuwa ni waajiriwa wao wasiopelekewa fedha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii
Walimu wengi hawana exposure, huwa hawakubali kukatwa NSSF kwa kigezo cha udogo wa mshahara na wanaokatwa huwq hawafuatilii kama michango yao inapelekwa ama laah!.
 
👉Kuachishwa kazi, ni mtihani mkubwa sana
😭😭😭💪🏿🙏🏾
Mimi ndio maana nilijijengeaga utaratibu wa kuacha kazi mwenyewe mapemaa mahala poote nilipopita kufanya kazi kabla sijaamua kujisimamia mwenyewe .
Sijui hii habit niliitoa wapi lakin hime walikua wananiona kama mimi nina pepo wenyewe wakalipa jina "pepo la kutanga tanga". 😂😂
 
Kazi ya ualimu ina changamoto sana,kwanza walimu hawapendan...kuna walimu wachawi kichizi yan..kama hauko vizuri ualimu hautoboi....
niseme ukweli tu kwa hili, nilijikuta nimekwa kati na staff nzima iko kinyume nami, wacha tuvaane na mkuu wa shule aliyeonekana ni baba yangu kabisa wa kunizaa tukakwidana kisha nikamfuata makamu wake nikamkunjia ngumi. Ilikuwa ni vita kubwa iliyoishia kuamuliwa na wanafunzi walioona naonewa na wenzangu. Kuna majungu sana maofisini, wivu na fitna zipo sana tu
 
Kwakweli hakuna kitu kinaumiza kama unaamka kila siku asubuhi na Huna pakwenda, Huna mchongo hata wa kuusikilizia na familia inakuangalia wewe, kama hujawahi pitia hii hali usiombe kabisa ikutokee..
 
Back
Top Bottom